KERO TTCL ni sikio la kufa! Haiwezekani kwa zaidi ya miezi sita nimeomba huduma ya fiber nyumbani wananizungusha tu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
CCM inaendelwa kuua nchi kupitia mashirika yake haya yanayofanya mambo pasipo tija yeyote...

Ukienda sasa pale makao makuu yao ukawaona utadhani wapo serious...
Naunga mkono hoja
 
Wazee wa kalenda hawa🤣,
 
Inategemea na ulipo, isije ikawa upo km 5 toka ilipopita ikawa ni gharama sana kukufikia. Sisi tuliopo dodoma tunaenjoy tu
Hii si kweli wote wanaolalamika sana wengi wao wapo karibu na hizo facility, ukitaka kuamini wewe soma comments tu, usipoona tatizo kwao hiyo itakua tatizo lingine
 
Walinchosha walipotoa gawio kwa mwenda zake ilhali wanajiendesha kihasara tu. Hawa watu wanapost mitandaoni ilo waonekana wanafanya kazi ila ukweli upo kwenye comments.
 
Walivyohama kutoka kupokea maombi Kwa fomu za kujaza kwa mkono kwenda kwenda kupokea maoni kwa njia ya mtandao, tuliona nia njema ya uongozi. Kwa sasa naamini wanaona maombi ya wateja na kupata ripoti za muda wanaotumia hadi kuwaunganisha. Tukiwapa benefit of doubt, pengine demand imekuwa kubwa kuliko mategemeo yao, na uwezo wa kitaasisi. Shida ni kwamba kama umeelewa, inakuaje marketing wanaendelea kutangaza watu waombe lakini hamna juhudi za hata kuwataarifu waliokwisha omba changamoto wanazolumbana nazo? Ni kama wamewekewa KPI za kuongeza wateja, bila kuangalia maeneo mengine ya kampuni yanayohitajika kufikia fulfiment yakoje. Kinachotokea sasa, kuna wateja wanarudia kuomba huduma, kuna wanaokata tamaa na kwenda kwa watoa huduma wengine, hamuoni kuna uwezekano mnapambana kuongeza capacity pamoja na vifaa kwa demand isiyo na uhalisia kwa tatizo mlilotengeneza wenyewe huku mkipoteza goodwill ya walioonyesha interest na huduma zenu?
 
Hii si kweli wote wanaolalamika sana wengi wao wapo karibu na hizo facility, ukitaka kuamini wewe soma comments tu, usipoona tatizo kwao hiyo itakua tatizo lingine
Nimeona mkuu, basi ni changamoto kwa kweli
 
Reactions: Lax
Nimeona mkuu, basi ni changamoto kwa kweli
hayo ndo mashirika ya umma mkuu, sasa wewe fikiria complain zote hizi mtaani , mitandaoni lakini hakuna juhudi za kueleweka wanachukua, na washindani nao wanakuja kwa kasi, Na raisi alisema hawa kwa hali waliyofikia wabaki tu kwenye intaneti na hali yao yenyewe ndo hii. ukireflect mbali unakuja kuona mwendokasi, ndege na yawezekana hat ile treni tukaja kukwama vilevile
 
Mashirika yamejaa Wazee walio foji umri,
Haya mashirika mengi ya umma yapo kisiasa zaidi.

Ni ujinga wa Mtanzania. Marekani mpaka inayofana na na Benki Juu, Federal Reserve, ni ya watu binafsi. Serikali wanawawekea sheria, sera na taratibu tu za kufata. Yaani ni facilitators tu.
. Hapa kwetu inabidi tubadilike, kwenye biashara iwe biashara,
 
Mm waliniambia hawaiapata vifaa nikawauliza mtapata lini wakasema hawajui ni mwaka wa pili sasa tangu tutume ombi la fiber.
 
Wewe nawe una mawazo ya kiarabu arabu muda wote. Mbona kuna nchi nyingi kabisa mashirika ya umma yanafanya kazi vizuri kabisa? N usimamizi wa serikali iliyopo madaraka tu na hamna cha zaidi. Mtu kama Samia na CCM yake tunaweza kutegemea ufanisi kwenye usimamizi wakati wao wenyewe ni mafisadi na wavivu wa grade one? Ngonya nikuambia: Haya mashirika yote ya umma yakipata serikali iliyo makini yanafanya vizuri tu. Kwa nini wasipewe ajira zao kwa mkataba wenye makubaliano? Kwa mfano hili la usambazani na ufungaji wa fiber wanaambiwa muda wa ku-process maombi usizidi muda fulani na kama hawafanyi hivyo mkataba unavunjika na wafanyakazi wote wanaondolewa na kuajiriwa wapya kwa mkataba mpya. Hili litafanya kila mfanyakazi aone umuhimu wa kujiwajibika kwani asipofanya hivyo anajua ajira itaisha.
 
Aisee! Pole sana. Nimeomba kwa njia ya mtandao ijumaa nilipigiwa simu kutoka kwao kwamba kuanzia leo wanaweza wakafika home kwaajili ya survey. Nitaleta mrejesho
 
unaombaje huduma kwa hao muflisi ambao hawajielewi kabisa, tafuta watu wengine hao umbwa unapoteza muda tu kwanza hata wakishafunga huduma zao utakuja kuniambia baadae.
 
Aisee! Pole sana. Nimeomba kwa njia ya mtandao ijumaa nilipigiwa simu kutoka kwao kwamba kuanzia leo wanaweza wakafika home kwaajili ya survey. Nitaleta mrejesho
Mwaka jana waliniambia vifaa vya kufanyia installation vimeisha hivyo nisubiri.

Nikala bunda nikaamua nichukue Router ya Airtel tu. Sasa hawa Airtel waliponiletea wizi wa internet Throttling nikapata ghadhabu nikaona niwapotezee.

Wakati nafikiria option gani nzuri wadau wakaniambia fiber ndio mpango mzima.

Nikakumbuka kuwa mwaka jana TTCL waliniambia vifaa vimeisha nikasema ngoja niwacheki.

Daaah ile kuwacheki si wakaniambia eti bado vifaa havijaja niendelee kusubiria.

Nikastaajabu nikawaambia hivi mnaelewa kuwa tangu mseme nisubiri hivyo vifaa ni mwaka sasa umepita?

Wakasema ndio tunajua kuwa ni mwaka ila ndio hivyo tunaomba tu uendelee kuwa mvumilivu.

Nikasema kama mwaka mzima haujatosha kufanya hivyo vifaa viweze kuja basi jibu la haraka hapo ni kwamba haiwekaniki hivyo vifaa kuja na hili ndio jibu ambalo mmeshindwa kuniambia.

Wakasema hapana sio hivyo inaweza kutokea hata hapa katikati vifaa vikaja na sisi tukakutaarifu.
 
Ofisi nyingi za serikali ili uhudumiwe vizuri unatakiwa uende na shati la mikono mirefu
Hao unaotaka wakuhudumie wengi wao walipata kazi baada ya kutoa rushwa
Sasa wewe wanakudumiaje bila kuwapa rushwa?
 
Mimi niliomba kufungiwa ofisni tu saizi ni miezi 36.
Wanachukua miezi 12 kuja kufanya survey
Alafu miezi 12 kusubiri vifaa
hiyo kumi na mbili iliyobaki unatakiwa kuwabembeleza.

CAG akisema shirika linaleta hasara ANALAUMIWA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…