KERO TTCL ni sikio la kufa! Haiwezekani kwa zaidi ya miezi sita nimeomba huduma ya fiber nyumbani wananizungusha tu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Wewe mbona hauko serious aisee. Miezi sita tu unalalama hivi wakati watu tuna miaka miwili na miezi tisa bado twawasubiria 😀 😀 😀 😀 😀 . Tuliomba huduma machi 2022 sasa piga hesabu.
 
Leo siku ya nne sina internet imekatika ukiwapigia simu wanakupa kiswahili tu, hili shirika tuwape wahindi tu sisi limetushinda ,uswahili mtupu, mbona haya makampuni binafsi kama tigo na voda hatusikii upuuzi kama huu
 
Leo siku ya nne sina internet imekatika ukiwapigia simu wanakupa kiswahili tu, hili shirika tuwape wahindi tu sisi limetushinda ,uswahili mtupu, mbona haya makampuni binafsi kama tigo na voda hatusikii upuuzi kama huu
Mkoa gan upo
 
Tayari unapata huduma
Yes napata huduma ila imekatika tangu juzi sipati ,nimereport sipati msaada wa haraka huku hela yangu inakatwa ,maana nalipia for thirty days na hili tatizo ni kila mwezi maana yake naibiwa pesa yangu
 
Hawa jamaa ni sawa tu na Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni, wako very useless kwa kweli
 
Inakaribia kufika mwaka, niliona niachane nao. Ubabaishaji mwingi
 
Taifa lina watu wanakula mishahara ya bure
 
Kuna mwaka nilipata changamoto, ya kulipia simu zao za mezani, land line phones. Nikawabembeleza nilipe nusu 35,000 wanifungilie incoming calls kwa watu wanaopiga peke yake, mimi nisipige mpaka nitakapomaliza deni lao 70,000, eti wakakataa hadi nilipe hela yote. Nilichofanya nikasajili line ya mkononi nikaachana nao jumla. Ni kama wanalihujumu shirika. Mwisho wa siku wakafunga makorokoro yao nikabaki na kichwa cha simu cha mezani cha kubonyeza kama ukumbusho.
 
Sisi (taasisi) tumeomba mwaka umeisha sasa hakuna dalili ya fundi wala ndugu yake fundi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…