Responded TTCL yafafanua hoja ya kuweka mnara Kibiti kisha kutoilipa familia husika

Responded TTCL yafafanua hoja ya kuweka mnara Kibiti kisha kutoilipa familia husika

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
UFAFANUZI KUHUSU HOJA YA MADAI YA FIDIA YA MAZAO KATIKA ENEO LA UJENZI WA MNARA WA TTCL – KIBITI

Kufuatia hoja iliyowasilishwa kupitia mtandao wa JamiiForums yenye kichwa cha habari “TTCL wameweka mnara eneo letu Kibiti, mazao yameharibika na hatujalipwa fidia,” Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limefanya ufuatiliaji.

Hoja ilipoanzia ~ TTCL wameweka mnara eneo letu Kibiti, mazao yameharibika na hatujalipwa fidia

Ukweli ni kuwa TTCL iliingia katika makubaliano rasmi na Serikali ya Kijiji cha Nyambili, ambapo eneo husika lilitolewa kwa ajili ya ujenzi wa mnara wa mawasiliano, pasipo haja ya malipo, ikiwa ni maamuzi ya Kijiji ili kuchochea maendeleo, kuzingatia umuhimu wa mradi katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo.

Aidha, Shirika lina nyaraka zinazothibitisha makubaliano hayo, zikiwemo nakala ya muhtasari wa kikao cha kijiji kilichojadili na kuridhia ombi la kutolewa kwa eneo hilo.

Taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano TTCL
 
ikiwa ni maamuzi ya Kijiji ili kuchochea maendeleo, kuzingatia umuhimu wa mradi katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo.
Blabla za kisiasa, ukienda kwenye makaratasi na account za benki utabaini fedha ilishachotwa kwenda kulipia eneo la mnara
 
Kuchochea maendeleo kivipi..?
Ttcl nao wakora, serikali ya kijiji nao wakora tu
Ttcl wanawezaje kwenda kuishinikiza serikali ya kijiji kwa porojo ya maendeleo....
Maendeleo gani italeta pale kijijini.

Ttcl ni wezi. Pesa wamekula,mwenye shamba anateseka
 
UFAFANUZI KUHUSU HOJA YA MADAI YA FIDIA YA MAZAO KATIKA ENEO LA UJENZI WA MNARA WA TTCL – KIBITI

Kufuatia hoja iliyowasilishwa kupitia mtandao wa JamiiForums yenye kichwa cha habari “TTCL wameweka mnara eneo letu Kibiti, mazao yameharibika na hatujalipwa fidia,” Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limefanya ufuatiliaji.

Hoja ilipoanzia ~ TTCL wameweka mnara eneo letu Kibiti, mazao yameharibika na hatujalipwa fidia

Ukweli ni kuwa TTCL iliingia katika makubaliano rasmi na Serikali ya Kijiji cha Nyambili, ambapo eneo husika lilitolewa kwa ajili ya ujenzi wa mnara wa mawasiliano, pasipo haja ya malipo, ikiwa ni maamuzi ya Kijiji ili kuchochea maendeleo, kuzingatia umuhimu wa mradi katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo.

Aidha, Shirika lina nyaraka zinazothibitisha makubaliano hayo, zikiwemo nakala ya muhtasari wa kikao cha kijiji kilichojadili na kuridhia ombi la kutolewa kwa eneo hilo.

Taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano TTCL
Mnaendaje kuweka mnara wenu kwenye eneo la mtu? Serikali ya kijiji ingewapa eneo la serikali. Hapo @ttcl mmekosea , lipeni fidia ya mazao ya wanyonge acheni uonezi
 
Wananchi wa JF porojo nyingi.

Eti wanauliza kuchochea maendeleo? Mitandao ikizimwa wanalalamika tupo nyuma kimaendeleo.
 
Aliyesaini mkataba anasemaje? DC amewashauri waende mahakamani

Yeye kama msomi katika familia asimamie hilo.
TTCL iliingia katika makubaliano rasmi na Serikali ya Kijiji

Twende polepole, hiyo ardhi haikuwa na wenyewe..? DC ndo mmiliki wa ardhi..?
 
Anayelalamika ni mmiliki? Au wazazi wake ndio wamiliki? Au ni mali ya urithi?

Au huyo ndugu ndiye aliwakaribisha hapo wazazi wao?
TTCL hawajawahi kuja kuzungumza na sisi wamiliki halali wa eneo, baada ya kuona kuwa kuna mawimbi (signal) mazuri eneo letu, walienda serikali ya kijiji kuomba eneo.

Viongozi wa kijiji walimtafuta ndugu yetu mmoja (ambaye hakuwa mmiliki wala hakuwa na uelewa wa kisheria), wakamshinikiza kusaini mkataba/muktasari wa kijiji kwa niaba yetu bila sisi wenyewe kutambua wala kushirikishwa.


Hiyo ni taarifa ya mwanafamilia, haya hadi hapo kuna sarakasi zimeanza, maeneo ya familia yapouzwa au kutolewa kunakua na kikao, mukhtasari unaandaliwa na saini ya kila mmoja inakuwepo

Hizo taratibu zilifatwa..?
 
Wananchi wa JF porojo nyingi.

Eti wanauliza kuchochea maendeleo? Mitandao ikizimwa wanalalamika tupo nyuma kimaendeleo.
Ukiwa ni mfuasi wa CCM unakuwa umeingia mkataba wa kutetea hata upuzi wa wazi?
Wananchi wanalalamika mazao yameharibiwa bila fidia wewe unaleta habari ya mitandao kuzimwa kama kutetea uvunjifu wa sheria ya fidia kwa waathirika!
 
Jitahidini kuwa watu wa Haki.
Duniani tunapita.

Hizi Dhuruma ni mambo ya kishamba sana.
 
Back
Top Bottom