Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Blabla za kisiasa, ukienda kwenye makaratasi na account za benki utabaini fedha ilishachotwa kwenda kulipia eneo la mnaraikiwa ni maamuzi ya Kijiji ili kuchochea maendeleo, kuzingatia umuhimu wa mradi katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo.
Mnaendaje kuweka mnara wenu kwenye eneo la mtu? Serikali ya kijiji ingewapa eneo la serikali. Hapo @ttcl mmekosea , lipeni fidia ya mazao ya wanyonge acheni uoneziUFAFANUZI KUHUSU HOJA YA MADAI YA FIDIA YA MAZAO KATIKA ENEO LA UJENZI WA MNARA WA TTCL – KIBITI
Kufuatia hoja iliyowasilishwa kupitia mtandao wa JamiiForums yenye kichwa cha habari “TTCL wameweka mnara eneo letu Kibiti, mazao yameharibika na hatujalipwa fidia,” Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limefanya ufuatiliaji.
Hoja ilipoanzia ~ TTCL wameweka mnara eneo letu Kibiti, mazao yameharibika na hatujalipwa fidia
Ukweli ni kuwa TTCL iliingia katika makubaliano rasmi na Serikali ya Kijiji cha Nyambili, ambapo eneo husika lilitolewa kwa ajili ya ujenzi wa mnara wa mawasiliano, pasipo haja ya malipo, ikiwa ni maamuzi ya Kijiji ili kuchochea maendeleo, kuzingatia umuhimu wa mradi katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo.
Aidha, Shirika lina nyaraka zinazothibitisha makubaliano hayo, zikiwemo nakala ya muhtasari wa kikao cha kijiji kilichojadili na kuridhia ombi la kutolewa kwa eneo hilo.
Taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano TTCL
Wenye maeneo yao wamelipwa..?Wananchi wa JF porojo nyingi.
Eti wanauliza kuchochea maendeleo? Mitandao ikizimwa wanalalamika tupo nyuma kimaendeleo.
Aliyesaini mkataba anasemaje? DC amewashauri waende mahakamaniWenye maeneo yao wamelipwa..?
Anayelalamika ni mmiliki? Au wazazi wake ndio wamiliki? Au ni mali ya urithi?Wenye maeneo yao wamelipwa..?
TTCL iliingia katika makubaliano rasmi na Serikali ya KijijiAliyesaini mkataba anasemaje? DC amewashauri waende mahakamani
Yeye kama msomi katika familia asimamie hilo.
TTCL hawajawahi kuja kuzungumza na sisi wamiliki halali wa eneo, baada ya kuona kuwa kuna mawimbi (signal) mazuri eneo letu, walienda serikali ya kijiji kuomba eneo.Anayelalamika ni mmiliki? Au wazazi wake ndio wamiliki? Au ni mali ya urithi?
Au huyo ndugu ndiye aliwakaribisha hapo wazazi wao?
Ukiwa ni mfuasi wa CCM unakuwa umeingia mkataba wa kutetea hata upuzi wa wazi?Wananchi wa JF porojo nyingi.
Eti wanauliza kuchochea maendeleo? Mitandao ikizimwa wanalalamika tupo nyuma kimaendeleo.