Responded TTCL yafafanua sababu za Mdau wa Goba kukosa huduma ya Faiba licha ya kulipia

Responded TTCL yafafanua sababu za Mdau wa Goba kukosa huduma ya Faiba licha ya kulipia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Baada ya andiko la Mdau alilozungumzia Huduma ya Faiba kutoka TTCL, andiko hili hapa ~ TTCL wamepokea malipo yangu ya Faiba kisha wanasema huduma haijafika Goba - Mageti

Ufafanuzi umetolewa kutoka TTCL 👇🏼

Tunamshukuru mteja kwa kuwasilisha hoja yake na kutupa fursa ya kufuatilia suala hili.

Baada ya kufanya uhakiki, tumebaini kuwa eneo lililoainishwa wakati wa kujaza taarifa kwenye mfumo halikuendana na eneo halisi alipo mteja. Kwa sasa, huduma ya Faiba Mlangoni Kwako (FTTH) bado haijafika katika eneo lake halisi, hivyo haijawezekana kukamilisha uunganishaji wa huduma hiyo.

Kuhusu malipo ya kifurushi yaliyofanyika, mfumo huruhusu mteja kuendelea hadi hatua ya kupata namba ya malipo pale anapochagua eneo ambalo huduma ya Faiba inapatikana. Katika maombi haya, eneo lililowasilishwa lilionesha kuwa huduma inapatikana, hivyo mfumo uliruhusu mchakato wa malipo kuendelea. Changamoto ilibainika baada ya uhakiki wa eneo halisi linalohitaji kuunganishiwa huduma.

Tunawasihi wateja wanaoomba huduma ya TTCL Faiba Mlangoni kwako kuhakikisha wanaingiza taarifa sahihi za eneo ambalo huduma inahitajika, ili mfumo uweze kuthibitisha upatikanaji wa huduma kabla ya kuendelea na hatua zinazofuata.

Tunamshukuru mteja kwa kutufikishia suala hili na tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza. TTCL itaendelea kuboresha mifumo na taratibu zake ili kuhakikisha wateja wanapata uzoefu bora zaidi katika kuomba na kutumia huduma zetu.
 
Hela yake karudishiwa au ndio hadi aandike barua hamsini na asambaze kwa kila mfanyakazi wenu?
 
Mbona sasa hawajatolea ufafanuzi kuhusu Hela ya mteja Hawa nyumbu kama itarudishwa au ni gudubayi??
 
TTCL Fiber wana huduma mbovi mfano hakuna...

Binafsi nimenunua kifurushi kinachoambatana na SIM card inayopaswa kuwekwa kifirushi cha 20GB...

Lakini hadi leo hawajawahi toa hiyo SiM card wala kifurushi...

Fiber yenyewe kuwekewa ilikuwa ni baada ya kupiga simu kama 200, baada ya kuwekewa huduma ilikuja kupatikana wiki 2 mbele, hapo washakuja mafundi kama 10...

Fundi wa mwisho ilibidi nianze kumuelekeza namna ya kufanya ili huduma ipatikane...
 
Hela yake karudishiwa au ndio hadi aandike barua hamsini na asambaze kwa kila mfanyakazi wenu?
Wee uliona wapi hela inarudishwaa atapelekewa huduma aliyoomba
 
Tanzania husipoteseka kwa hili,utateseka kwa lile... ilimrad kila mtu apate mateso
 
Back
Top Bottom