Tuache kudanganyana hakuna gesi iliyowahi kuuzwa na kusafirishwa kwa bomba kwenda nje ya Tanzania

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Unapo zungumzia gesi ni tofauti sana na mafuta katika swala zima la uhifadhi na usafirishaji.

Ili kuweza kuisafirisha gesi nje ya nchi unahitaji miundo mbinu ya kuweza kuibadilisha kuwa kimiminika.

Ikiwa katika hali ya kimiminika ndipo unaweza kuipakia kwenye meli ikiwa kwenye mitungi maalumu na kuisafirisha hadi nje ya nchi.

Mbaya zaidi huwezi kujenga bomba la gesi kutoka Tanzania hadi ulaya. Pesa utakayotumia itakua kubwa sana kuliko faida utakayoipata.

Mara nyingi mabomba ya kuisafirisha gesi asilia hujengwa katika umbali mfupi mfano mkoa hadi mkoa au wilaya hadi wilaya.

Sasa unapomsikia mtu anasema bomba zimechimbwa kutoka Mtwara hadi Ulaya unawaza hivi inawezekanaje? Unakuja kugundua labda kunatatizo katika elimu hii ya mafuta na gesi.

Gesi ya Mtwara bado ipo zaidi itaanza kuzalishwa mpaka LNG plant itakapokua imejengwa.

Hii inayozalishwa sasa ni kiasi kidogo tu.

Karibuni kwa maswali sasa

Mengineyo:
Kwa ushauri kuhusu maswala ya gesi na mafuta pia karibuni.

Nakukumbusha nyumba yako itakua salama endapo kama mtungi wa gesi ya kupikia (LPG) utahifadhiwa mahali penye hewa ya kutosha nje ya nyumba yako, na kupitisha mpira wa gesi kupitia ukutani au dirishani mpaka kwenye jiko lako jikoni.

Pika salama lala kwa amani bila hofu.

Mawasiliano: 0747744895

Agiza gesi ya kupikia mahali ulipo kupitia hapa: Campus City Shopping Mall - Online Shopping for Popular Electronics, Fashion, Home & Garden, Toys & Sports, Automobiles and More.
 
Meli ngapi za kuvua samaki zinavua kiharamu huko bahari kuu nani anaziona ?? Kwani gesi ambayo tumekuwa tukiitumia miaka mingi kabla hata ya kugunduliwa hiyo ya mtwara ilikuwa inasafirishwa kwa kutumia njia zipi mpaka zitufikie hapa TZ ??
 
Shukran kwa kutujuza, naomba kujua tuna aina ngapi za gas Mtwara ? Nasikia ipo LNG, kama ulivyotaja je hii inayojazwa kwenye magari huku Dar CNG inatoka wapi ? ni nini uhusiano wake LNG na CNG ?
Inaitwa gesi asilia (Natural Gas).

Mtwara tuna aina moja ya gesi asilia yenye kiwango kikubwa cha kampaundi ya methane. LNG sio aina ya gesi. Kwanza tambua kwamba LNG kirefu chake ni Liquefied Natural Gas (Gesi asilia iliyo badilishwa kuwa kimiminika).

Tambua kwamba ni gesi iliyobadilishwa kuwa kimiminika ili iwe rahisi kuifadhi na kuisafirisha kwa wingi katika umbali mrefu sana sana nje ya nchi. Ukiibadilisha gesi kuwa kimiminika ndipo unaweza kuisafirisha kwa wingi zaidi. Kipimo kimoja cha gesi asilia kinakua mara 600 ikiwa katika hali ya kimiminika.

Bado LNG haijaanza kuzalishwa Mtwara. Ili kuizalisha LNG kinatakiwa kijengwe kiwanda kinacho gharimu Trillion 70 Tsh.

Hivyo kazi kubwa ya kiwanda hicho itakua ni kuibadilisha gesi asilia kuwa LNG.

CNG kirefu chake ni compressed natural gas yaani gesi asilia iliyo kandamizwa au shindiliwa. Nayo bado ni gesi asilia ila yenyewe imeshindiliwa kwa kutumia mashine ili itumike kwenye magari.

LNG na CNG zote ni gesi asilia na zote zina kampaundi ya methane. Isipokua LNG ipo katika katika mfumo wa kimiminika na CNG katika muundo wa kukandamizwa. Lengo kuu ni kuweza kuifadhi na kusafirisha.
 
Shukran sana kwa hiyo elimu nimekuelewa vema
Pia nimeona huko kwingineko dunian yapo magari ya LNG na CNG Je wale waliobadili gari kutumia CNG na baadae hiyo mitambo ya LNG kukamilika hayo magari yataweza kutumia hizo zote gas ? au itabidi kubadili tena kwenda LNG ?
Na ni ipi yenye better efficiency kwa matumizi ya magari kwa hizo mbili ?

Sorry nisikusumbue nimepata jibu;
LPG performance is better than CNG because its combustion is fast than CNG. Thats why Maruti's DUO car is on LPG not on CNG. Secondly, weight of CNG cylinder is double than the weight of LPG cyclyder. Also the cost of CNG is almost double than LPG.
 
Ila naomba tena usichanganye LNG na LPG.
LPG ni liquefied petroleum gas na imeundwa kwa kampaundi za propane na butane.
LPG huwa inazalishwa wakati wa kuchakata mafuta ghafi (crude oil) au wakati wa kuchakata gesi asilia yenye kiwango kikubwa cha butane na propane.
LPG haipo Tanzania, huagizwa kutoka nje ya nchi. LPG ndio gesi tunayotumia kupikia majumbani (Oryx, Mihani, Taifa n.k).

Ili kupata LPG tunazikandamiza butane na propane katika mgandamizo mdogo tu (low pressure). Baada ya hapo butane na, propane zinakua kimiminika.

Ili kupata CNG tunaikandamiza gesi asilia (methane) katika pressure kubwa.

Ili kuipata LNG tunaipoza gesi asilia (methane) katika joto la (-163 °C)
 
Meneja unaupiga mwingi.
 
Meli ngapi za kuvua samaki zinavua kiharamu huko bahari kuu nani anaziona ?? Kwani gesi ambayo tumekuwa tukiitumia miaka mingi kabla hata ya kugunduliwa hiyo ya mtwara ilikuwa inasafirishwa kwa kutumia njia zipi mpaka zitufikie hapa TZ ??
Bila shaka umefuatilia mada, maswali yako yametolewa majibu mujarab kabisa katika mawasilisho ya ndugu yetu Meneja Wa Makampuni

Suala la sisi kama nchi "kuibiwa" na meli za uvuvi katika bahari kuu (EEZ) naona liko nje kidogo ya mawanda ya mada hii.
 
Inaitwa gesi asilia (Natural Gas).

Mtwara tuna aina moja ya gesi asilia yenye kiwango kikubwa cha kampaundi ya methane. LNG sio aina ya gesi. Kwanza tambua kwamba LNG kirefu chake ni Liquefied Natural Gas (Gesi asilia iliyo badilishwa kuwa kimiminika).

Tambua kwamba ni gesi iliyobadilishwa kuwa kimiminika ili iwe rahisi kuifadhi na kuisafirisha kwa wingi katika umbali mrefu sana sana nje ya nchi. Ukiibadilisha gesi kuwa kimiminika ndipo unaweza kuisafirisha kwa wingi zaidi. Kipimo kimoja cha gesi asilia kinakua mara 600 ikiwa katika hali ya kimiminika.

Bado LNG haijaanza kuzalishwa Mtwara. Ili kuizalisha LNG kinatakiwa kijengwe kiwanda kinacho gharimu Trillion 70 Tsh.

Hivyo kazi kubwa ya kiwanda hicho itakua ni kuibadilisha gesi asilia kuwa LNG.

CNG kirefu chake ni compressed natural gas yaani gesi asilia iliyo kandamizwa au shindiliwa. Nayo bado ni gesi asilia ila yenyewe imeshindiliwa kwa kutumia mashine ili itumike kwenye magari.

LNG na CNG zote ni gesi asilia na zote zina kampaundi ya methane. Isipokua LNG ipo katika katika mfumo wa kimiminika na CNG katika muundo wa kukandamizwa. Lengo kuu ni kuweza kuifadhi na kusafirisha.
Salute uko vizuri sana kwenge maswala ya gas....
Ningependa kufahamu gas inayotumika pale Kinyerezi Power Plant kuzalisha umeme inasafirishwa katika hali gani? CNG au?
 
Meli ngapi za kuvua samaki zinavua kiharamu huko bahari kuu nani anaziona ?? Kwani gesi ambayo tumekuwa tukiitumia miaka mingi kabla hata ya kugunduliwa hiyo ya mtwara ilikuwa inasafirishwa kwa kutumia njia zipi mpaka zitufikie hapa TZ ??
Hiyo gesi ambayo tumekua tukiitumia kabla ya kugunduliwa gesi ya Mtwara inaitwa Liquefied Petroleum Gas (LPG). LPG imeundwa kwa kampaundi za propane na butane. LPG ndio gesi inayouzwa na akina Mihani, Oryx, Taifa, Lake n.k.
LPG unaweza kuihifadhi nyingi kwenye mtungi katika mgandamizo mdogo (low pressure) kisha ukaweza kuisafirisha popote duniani ikiwa kwenye mtungi.

Gesi yetu ya Mtwara imeundwa kwa kampaundi ya methane. Ili uweze kuisafirisha nje ya nchi katika mataifa ya mbali njia pekee yenye faida ni kuibadilisha kuwa kimiminika kwanza kwa kuipoza katika joto la (-163 °C) kisha iweke kwenye mitungi yenye kuweza kuhifadhi hilo joto pakia kwenye meli. Ila katika umbali mfupi njia pekee yenye faida ni kutumia bomba tu.
Na mbaya zaidi huwezi kupikia gesi asilia ikiwa kwenye mtungi. Ili uweze kupikia gesi asilia unatakiwa kupikia ikiwa ndani ya bomba. Hivyo kwa Tanzania ili tuweze kupikia gesi asilia tunatakiwa kusambaza mabomba kwenye nyumba zote zenye uhitaji.

Hivyo tatizo kubwa la gesi asilia lipo kwenye uhifadhi na usafirishaji.

Kwa umbali mrefu ukitumia bomba ni hasara. Maana yake ujenge bomba kutoka Mtwara mpaka ulaya (dhana potofu).
Otherwise ujenge kiwanda cha kuzalisha LNG (ambacho kama kingekuwepo tungekiona tu)
 
Ila naomba tena usichanganye LNG na LPG.
LPG ni liquefied petroleum gas na imeundwa kwa kampaundi za propane na butane.
LPG huwa inazalishwa wakati wa kuchakata mafuta ghafi (crude oil) au wakati wa kuchakata gesi asilia yenye kiwango kikubwa cha butane na propane.
LPG haipo Tanzania, huagizwa kutoka nje ya nchi. LPG ndio gesi tunayotumia kupikia majumbani (Oryx, Mihani, Taifa n.k).

Ili kupata LPG tunazikandamiza butane na propane katika mgandamizo mdogo tu (low pressure). Baada ya hapo butane na, propane zinakua kimiminika.

Ili kupata CNG tunaikandamiza gesi asilia (methane) katika pressure kubwa.

Ili kuipata LNG tunaipoza gesi asilia (methane) katika joto la (-163 °C)
Kweli tayari nimeshachanganya naomba majibu sahihi ya maswali yangu kuhusu CNG na LNG ni ipi bora zaidi kwa magari ? gharama na pia magari ya CNG yataweza kutumia LNG ?
 
Wabongo wameshazoea uongo uongo kudanganywa danganywa.

Huu uongo alianza nao Dr Slaa mwaka fulani kwenye kampeni eti kuna gas inaibiwa inapelekwa ulaya kwa bomba kupita baharini, toka siku hiyo nilimdharau sana Dr Slaa.

Yaani kwa akili ya kawaida kabisa, Project ya kujenga bomba baharini from mtwara to Europe inaweza kuwa project ya kitoto?
 
Hilo la kusema kuna bomba limechimbwa kutoka Mtwara hadi ulaya wala sishangai kwa Mtanzania kuamini maana Watanzania ni mabingwa wa kuamini visivyoaminika.

Kama unaweza kuwaaminisha nusu ya Watanzania kuwa kuna Mti ukikatwa unainuka tena, au kuna kaburi limegoma kuhamishwa ni lipi limebakia?.
 
Back
Top Bottom