Mgagaa na Upwa
JF-Expert Member
- Sep 30, 2013
- 13,481
- 28,116
Huyo dada ni mbobezi kwenye sekta ya hii inavyoonekanaMijadala mizuri na yenye kutuelimisha sisi "laymen" wa nyanja hii ya gesi asilia. Safi sana waungwana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo dada ni mbobezi kwenye sekta ya hii inavyoonekanaMijadala mizuri na yenye kutuelimisha sisi "laymen" wa nyanja hii ya gesi asilia. Safi sana waungwana.
LNG ni gesi asilia iliyo katika kimiminika. CNG ni gesi asilia iliyo gandamizwa. Utofauti mkubwa wa LNG na CNG upo kwenye uzito katika ujazo (density). Kipino kimoja cha nishati ya LNG ni mara 3 chini ya ujazo kuliko kipimo kimoja cha CNG. Hii inamaanisha kuwa LNG ni nzito zaidi (yaani ina density kubwa), na hivyo hutoa nishati (energy) kubwa zaidi kwenye injini ikilinganishwa na CNG.Kweli tayari nimeshachanganya naomba majibu sahihi ya maswali yangu kuhusu CNG na LNG ni ipi bora zaidi kwa magari ? gharama na pia magari ya CNG yataweza kutumia LNG ?
Karibu kwenye hii elimuHii elimu ya masuala ya gesi nimeipenda sana. Asante sana mkuu Meneja Wa Makampuni
Karibuni kwenye hii elimuHuyo dada ni mbobezi kwenye sekta ya hii inavyoonekana
Hilo la kusema kuna bomba limechimbwa kutoka Mtwara hadi ulaya wala sishangai kwa Mtanzania kuamini maana Watanzania ni mabingwa wa kuamini visivyoaminika.
Kama unaweza kuwaaminisha nusu ya Watanzania kuwa kuna Mti ukikatwa unainuka tena, au kuna kaburi limegoma kuhamishwa ni lipi limebakia?.
Nishakaribia naokota yaliyo mazuri,swali nje ya mada mkuu,oil,gas and ernegy quantity surveyor kibongo anaweza akawa anachukua Tzs ngapi kwa mwezi?Karibuni kwenye hii elimu
Inategemeana na kampuni au taasisi. Kama ni private company mfano zilizopo Kurasini huko nadhani wanaanzia 800k mpaka 1000k. Lkn kwa government itakua zaidi ya hapo tena sana.Nishakaribia naokota yaliyo mazuri,swali nje ya mada mkuu,oil,gas and ernegy quantity surveyor kibongo anaweza akawa anachukua Tzs ngapi kwa mwezi?
Shukran mkuu,ila mmh 🤔Inategemeana na kampuni au taasisi. Kama ni private company mfano zilizopo Kurasini huko nadhani wa 800k mpaka 1000k. Lkn kwa government itakua zaidi ya hapo tena sana.
Ndio hivyo, kwa government nadhani unaelewa hapo itakua EWURA na TBS.Shukran mkuu,ila mmh 🤔
Nimekusoma kiongozi,shukranNdio hivyo, kwa government nadhani unaelewa hapo itakua EWURA na TBS.
Ila kwa private itakua ni Intertek, BV, SGS, nk
Mkuu unawashangaa wanasiasa kwa kuwalisha matangopori Watanzania?Kwahiyo hizi story za kuwa gesi ya Mtwara imeuzwa itakuwa ni uzushi tu...
Ni hadithi tu hizo, iliwapasa wazungumzie kwa hali ya mkataba tulioingia production sharing agreement (PSA) ambao sisi hatuchangii hata shilingi kwenye uwekezaji.Kwahiyo hizi story za kuwa gesi ya Mtwara imeuzwa itakuwa ni uzushi tu...
Shukran kwa kutujuza, naomba kujua tuna aina ngapi za gas Mtwara ? Nasikia ipo LNG, kama ulivyotaja je hii inayojazwa kwenye magari huku Dar CNG inatoka wapi ? ni nini uhusiano wake LNG na CNG ?
KabisaKama anasafishika acha asafishwe
Kivipi tena boss, mbona elimu ipo wazi kabisa.
Shukrani.Hiyo gesi ambayo tumekua tukiitumia kabla ya kugunduliwa gesi ya Mtwara inaitwa Liquefied Petroleum Gas (LPG). LPG imeundwa kwa kampaundi za propane na butane. LPG ndio gesi inayouzwa na akina Mihani, Oryx, Taifa, Lake n.k.
LPG unaweza kuihifadhi nyingi kwenye mtungi katika mgandamizo mdogo (low pressure) kisha ukaweza kuisafirisha popote duniani ikiwa kwenye mtungi.
Gesi yetu ya Mtwara imeundwa kwa kampaundi ya methane. Ili uweze kuisafirisha nje ya nchi katika mataifa ya mbali njia pekee yenye faida ni kuibadilisha kuwa kimiminika kwanza kwa kuipoza katika joto la (-163 °C) kisha iweke kwenye mitungi yenye kuweza kuhifadhi hilo joto pakia kwenye meli. Ila katika umbali mfupi njia pekee yenye faida ni kutumia bomba tu.
Na mbaya zaidi huwezi kupikia gesi asilia ikiwa kwenye mtungi. Ili uweze kupikia gesi asilia unatakiwa kupikia ikiwa ndani ya bomba. Hivyo kwa Tanzania ili tuweze kupikia gesi asilia tunatakiwa kusambaza mabomba kwenye nyumba zote zenye uhitaji.
Hivyo tatizo kubwa la gesi asilia lipo kwenye uhifadhi na usafirishaji.
Kwa umbali mrefu ukitumia bomba ni hasara. Maana yake ujenge bomba kutoka Mtwara mpaka ulaya (dhana potofu).
Otherwise ujenge kiwanda cha kuzalisha LNG (ambacho kama kingekuwepo tungekiona tu)
Hayati Magufuli aliposema gesi ya Mtwara tumeshapigwa alikuwa amekusudia nini ?? Je hakuwa well informed na watu wake. ?? Inawezekana Rais akadanganywa namna ile. ??Ni hadithi tu hizo, iliwapasa wazungumzie kwa hali ya mkataba tulioingia production sharing agreement (PSA) ambao sisi hatuchangii hata shilingi kwenye uwekezaji.
Kawaida ya PSA humtaka mwekezaji azalishe gesi na kuuza mpaka atakapo rudisha gharama alizotumia kwenye uwekezaji ambayo huchukua muda fulani. Akisha rudisha ndipo mnaanza kugawana faida inayopatikana kutokana na mauzo ya gesi.
Na kiukweli mkataba tulioingia ndio mzuri zaidi ukilinganisha na mikataba mingine kama Joint Venture na Concession. Pia tunaangalia na hali ya uchumi wetu, mfano mkataba kama wa joint Venture ambao hutaka nawewe uchangie kwenye mtaji kiukweli kwa taifa lenye uchumi mdogo kama wakwetu ni risk endapo kama hatutoweza ipata gesi tuliyotarajia.
LNG plant pekee inahitaji Trillini 70 Tsh. Maana yake kama ukiamua kuingia moja kwa moja kushiriki join venture maana yake nawewe utoe Trillioni 30 au 20 kutoka kwenye bajeti yetu. Hapo ukiangalia ni risk kwa uchumi wetu.