Tuache kudanganyana hakuna gesi iliyowahi kuuzwa na kusafirishwa kwa bomba kwenda nje ya Tanzania

Ni CNG, huko inakotoka mpaka kufika Kinyerezi inapitia kwenye compressor stations zinazofanya kazi hiyo ya kuigandamiza kuwa CNG
Pamoja na maelezo yako mazuri huko nyuma, hapa naongeza yafuatayo;
Kiasili gesi asilia Ina pressure kutoka ardhini (visima vina msukumo wa kutosha). Compressor hutumika tu pale ambapo gesi imepungua (kuelekea kuisha) na hivyo pressure iliyokusudiwa kuendesha mitambo kutoka kwenye kisima kutofikiwa.
 
Ndio kusema LNG haina soko nje kutokana na gharama zake na uwepo wa LPG. LNG Mataifa ya nje hawaitaki coz ina gharama ya kuichakata na pia uwepo wa LPG ya kutosha kwahiyo Gas yetu haiwezi kutupatia pesa za kigeni na ndio maana hata JPM akaona aikaushie tu na hata mataifa ya nje kutokua na shobo nayo
 
Na wewe umedanganya, Dr.Slaa alisema ni mafuta na siyo gesi na wala hakusema kuna bomba la gesi kwenda ulaya.
 
Hayati Magufuli aliposema gesi ya Mtwara tumeshapigwa alikuwa amekusudia nini ?? Je hakuwa well informed na watu wake. ?? Inawezekana Rais akadanganywa namna ile. ??
Alikuwa na maana ya kwamba mikataba tulioingia ya uchimbaji wa gesi hainufaishi nchi badala yake inawanufaisha zaidi waliowekeza kuchimba hiyo gesi maana wataendelea kutuuzia hiyo gesi kwa bei kubwa hadi warudishe gharama na faida kwa miaka mingi. Wakati wa JPM nia yake ilikuwa kuharakisha ujenzi wa bwawa la JNHPP ili ujenzi wake ukamilike mapema na kuua biashara ya kuiuzia nchi gesi na umeme unaozalishwa na gesi kwa bei kubwa. Kumbuka Serikali ina mkataba na Songas ya kutuuzia umeme unaozalishwa na gesi hadi 2024.
 
Usichokijua ni kwamba maeneo au visima vyenye gesi vimeshauzwa kwa makampuni vya nje Enzi za kikwete ndo maana magufuli anasema hatuna chetu tumebakiwa na visima vichache.lakini maeneo yenye gesi nyingi yameshauzwa.
 
Kwa hiyo Kikwete ameshauza maeneo au visima vyenye gesi na inasemekana pia Katoa mengine kwa wachina ili amuokoe kijana wake alipokamatwa na madawa ya kulevya.
 
Kumbee !! Tunaumizana sisi kwa sisi halafu tunasema wengine ni wajanja wa mjini !! Salaaleeh !!
 
Lakini bandugu Kwa Mzungu akitaka jambo lake huwa hashindwi !!
 
Meli ngapi za kuvua samaki zinavua kiharamu huko bahari kuu nani anaziona ?? Kwani gesi ambayo tumekuwa tukiitumia miaka mingi kabla hata ya kugunduliwa hiyo ya mtwara ilikuwa inasafirishwa kwa kutumia njia zipi mpaka zitufikie hapa TZ ??
Unachozungumza kuhusu samaki ni kweli ila sio kwa gesi asilia. Ili uweze kusafirisha gesi asilia unahitaji kuwa na bomba kutoka mahali inapozalishwa gesi hadi huko ulaya. Kujenga bomba hadi ulaya ni gharama zaidi ya faida utakayoipata ukiuza hiyo gesi. Njia ya pili ni kuibadilisha hiyo gesi kuwa kimiminika (LNG) kisha unaiweka kwenye mitungi na kuisafirisha hadi nje ya nchi kuiuza. Kufanya hivyo lazima ujenge kiwanda cha kuipoza hiyo gesi ili iwe kimiminika. Hicho kiwanda ni ghali sana (70Trillion Tsh). Hapo inahitaji utafute wawekezaji wakubwa. Kwa serikali zetu zenye bajeti ndogo, kufanya uwekezaji wa 70T kwa mambo ya gesi na, mafuta inaweza kuwa ni risk. Kwa hiyo lazima uwaachie wazungu wajichange wenyewe.

Gesi ambayo huwa inatufikia hapa Tanzania inaitwa LPG, hiyo huwa sio kazi kuisafirisha. Kwasababu kwanza kuibadilisha kuwa kimiminika na kuiweka kwenye mitungi unahitaji mgandamizo (pressure) kidogo sana.
 
Kwa hiyo Kikwete ameshauza maeneo au visima vyenye gesi na inasemekana pia Katoa mengine kwa wachina ili amuokoe kijana wake alipokamatwa na madawa ya kulevya.
Usiwaseme viongozi kwa mambo usiyoyajua rafiki. Ni vyema tujikite kuelimishana tu na sio kusambaza taarifa tusizo zijua.
 
Hayati Magufuli aliposema gesi ya Mtwara tumeshapigwa alikuwa amekusudia nini ?? Je hakuwa well informed na watu wake. ?? Inawezekana Rais akadanganywa namna ile. ??

Mara tu gesi asilia inapochimbwa, huuzwa kwa serikali na hayo makampuni ya wazungu...

Mkataba uliopo ni huo wa manunuzi na bila shaka JPM alilenga kwenye mktaba huo...
 
Mara tu gesi asilia inapochimbwa, huuzwa kwa serikali na hayo makampuni ya wazungu...

Mkataba uliopo ni huo wa manunuzi na bila ahka JPM alilenga kwenye mktaba huo...
Na hiyo inafuatana na mkataba mlio ingia. Mwanzoni huwa hivyo mpaka mwekezaji arudishe gharama zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…