Tuache kudanganyana hakuna gesi iliyowahi kuuzwa na kusafirishwa kwa bomba kwenda nje ya Tanzania

Tuache kudanganyana hakuna gesi iliyowahi kuuzwa na kusafirishwa kwa bomba kwenda nje ya Tanzania

Sijui hata nianzie wapi kwa aina hii ya ufahamu ulionao na hao wengine pia.

Kuna sehemu hadi nimeona aibu uliposema mradi wa Kinyerezi ni gesi kutoka songosongo na mnazi bay. Hivi hata songosongo unaoajua kweli?
Boss sijasema songosongo nilisema Songo Songo. Rekebisha uandikaji wa Songo Songo. Aya sasa eleza kwa utaratibu ili jamii forum ipate uo ufahamu boss.
Mimi binafsi nataka nijifunze kutoka kwako.
 
Inaitwa gesi asilia (Natural Gas).

Mtwara tuna aina moja ya gesi asilia yenye kiwango kikubwa cha kampaundi ya methane. LNG sio aina ya gesi. Kwanza tambua kwamba LNG kirefu chake ni Liquefied Natural Gas (Gesi asilia iliyo badilishwa kuwa kimiminika).

Tambua kwamba ni gesi iliyobadilishwa kuwa kimiminika ili iwe rahisi kuifadhi na kuisafirisha kwa wingi katika umbali mrefu sana sana nje ya nchi. Ukiibadilisha gesi kuwa kimiminika ndipo unaweza kuisafirisha kwa wingi zaidi. Kipimo kimoja cha gesi asilia kinakua mara 600 ikiwa katika hali ya kimiminika.

Bado LNG haijaanza kuzalishwa Mtwara. Ili kuizalisha LNG kinatakiwa kijengwe kiwanda kinacho gharimu Trillion 70 Tsh.

Hivyo kazi kubwa ya kiwanda hicho itakua ni kuibadilisha gesi asilia kuwa LNG.

CNG kirefu chake ni compressed natural gas yaani gesi asilia iliyo kandamizwa au shindiliwa. Nayo bado ni gesi asilia ila yenyewe imeshindiliwa kwa kutumia mashine ili itumike kwenye magari.

LNG na CNG zote ni gesi asilia na zote zina kampaundi ya methane. Isipokua LNG ipo katika katika mfumo wa kimiminika na CNG katika muundo wa kukandamizwa. Lengo kuu ni kuweza kuifadhi na kusafirisha.
Wewe mtu mbona unaongea uongo Sana? Huu Uzi nilikuwa wapi sikuona huu uongo hapa

LNG haijaanza kuzaliswa mtwara? Kile kinachozalishwa mnazi bay na madimba ni nn?
 
Ni hadithi tu hizo, iliwapasa wazungumzie kwa hali ya mkataba tulioingia production sharing agreement (PSA) ambao sisi hatuchangii hata shilingi kwenye uwekezaji.
Kawaida ya PSA humtaka mwekezaji azalishe gesi na kuuza mpaka atakapo rudisha gharama alizotumia kwenye uwekezaji ambayo huchukua muda fulani. Akisha rudisha ndipo mnaanza kugawana faida inayopatikana kutokana na mauzo ya gesi.

Na kiukweli mkataba tulioingia ndio mzuri zaidi ukilinganisha na mikataba mingine kama Joint Venture na Concession. Pia tunaangalia na hali ya uchumi wetu, mfano mkataba kama wa joint Venture ambao hutaka nawewe uchangie kwenye mtaji kiukweli kwa taifa lenye uchumi mdogo kama wakwetu ni risk endapo kama hatutoweza ipata gesi tuliyotarajia.

LNG plant pekee inahitaji Trillini 70 Tsh. Maana yake kama ukiamua kuingia moja kwa moja kushiriki join venture maana yake nawewe utoe Trillioni 30 au 20 kutoka kwenye bajeti yetu. Hapo ukiangalia ni risk kwa uchumi wetu.
LNG plant pekee inahitaji trillion 70?? Wewe unaelewa kweli unachoongea?
 
Hiyo gesi inayotumika kufua umeme Kinyerezi Dar es Salaam ni gesi asilia pia inayozalishwa katika vitalu vya Songo Songo na Mnazi Bay.

Kitalu cha Mnazi Bay kinasimamiwa na kampuni inaitwa PanAfrican Energy Tanzania Ltd lakini pana ubia makampuni mengine.

Na kitalu cha Mnazi Bay kinamilikiwa na Maurel & Prom (hisa 48.06%), TPDC (hisa 20%) na Wentworth Resources PLC (hisa 31.94%). Hivi vitalu viwili viligunduliwa zamani kidogo na gesi yake inapatikana kwenye maji ya kina kifupi na nyingine nchi kavu kabisa.

Lakini gesi inayozungumziwa kuwa itabadilisha uchumi wa Tanzania ni ile iliyogunduliwa kwenye maji ya kina kirefu katika kitalu cha Block 2 Offshore Field. Hiyo ndio gesi nyingi ambayo haiwezi kuzalishwa bila uwepo wa kiwanda cha kuibadilisha hiyo gesi nyingi kuwa kimiminika (LNG) ili isafirishwe kuuzwa nje ya nchi.
Wewe hujui kabisa unachoongea. Toka lini umeme wa Kinyerezi ni gesi ya songosongo? Unajua hata lolote kuhusu Ubungo I power plant?
 
Boss sijasema songosongo nilisema Songo Songo. Rekebisha uandikaji wa Songo Songo. Aya sasa eleza kwa utaratibu ili jamii forum ipate uo ufahamu boss.
Mimi binafsi nataka nijifunze kutoka kwako.
Unataka utaratibu upi? Kinyereza toka lini ikazalisha umeme kutoka gesi ya songo songo?? Ndio maana nikakuuliza unajua hata songo songo ilipo? Unajua hata bomba la mtwara limatoa wapi gasi?
 
Ule mradi sio reliable
Huenda hujui unachoongea. Gas inayozalisha umeme plae kinyerezi tunanunua kutoka tpdc ambao nao wananunua kutoka kwenye makampuni yaliyowekeza, ambapo haujulikani lini watarudisha pesa yao ya uwekezaji na kuanza kupata faida. Ni bora kuendelea kununua gesi kutoka kwa hayo makampuni au kuwa na chanzo chako? Unajua sababu ya nchi za ulaya sasa hivi kusuffer ni nn?
 
Unataka utaratibu upi? Kinyereza toka lini ikazalisha umeme kutoka gesi ya songo songo?? Ndio maana nikakuuliza unajua hata songo songo ilipo? Unajua hata bomba la mtwara limatoa wapi gasi?
Boss watu humu wanafuatilia unachokiandika eleza kile unachokielewa wewe usijali. Eleza unavyoelewa mwenyewe nahitaji kuelewa hicho ulichonacho.
 
Unataka utaratibu upi? Kinyereza toka lini ikazalisha umeme kutoka gesi ya songo songo?? Ndio maana nikakuuliza unajua hata songo songo ilipo? Unajua hata bomba la mtwara limatoa wapi gasi?
Boss tunahitaji mchango wako katika hii mada.
 
Zote ni natural gesi (gesi asilia) na zinatajwa hivyo kutegemea na namna zilivyohifadhiwa...

LNG - Liquefied Natural Gas, yaani gesi ya asili imebadilishwa na kuwa kimiminika na kuhifadhiwa kwenye mitungi midogo au mikubwa,

CNG - Compressed Natural Gas, yaani ni gesi ya asili nyingi iliyokandamizwa ili iweze kuenea ndani ya mtungi au tanki, hali yake haijabadilishwa na kuwa kimiminika

Kama ulisoma somo la fizikia ya form 1 nadhani unaweza ukawa unakumbuka kuwa "matter can never be destroyed nor created, but it can be transformed in different forms" - Law of Conservation of Mass

Ni kama vile tu unapoweza chemsha maji yakawa mvuke au ukayagandisha yakawa yabisi, lakini mwisho wa siku ni maji yale yale au ukaupooza mvuke na ukawa maji...(Hii ulifundishwa katika somo la Sayansi ukiwa darasa la tano)
Ah Ah Ah Ah .....Hapana
Usituchanganye na kutuchanganyia habari
Hapa Meneja wetu ameshatuelezea na tumemueleewa....
 
Unataka utaratibu upi? Kinyereza toka lini ikazalisha umeme kutoka gesi ya songo songo?? Ndio maana nikakuuliza unajua hata songo songo ilipo? Unajua hata bomba la mtwara limatoa wapi gasi?
Angalia hii ramani kwa umakini boss. Inaonyesha mchoro wa bomba la gesi (rangi nyekundu) kutoka kitalu cha Mnazi Bay. Ukitazama kwa umakini hapo katikati kuna bomba la gesi (rangi nyekundu) linalotokea kitalu cha Songo Songo kuungana na hilo bomba linatokea Mnazi Bay kuelekea Kinyerezi Dar es Salaam.
images (4).jpeg

Lakini pia unaweza kusoma maelezo ya Kinyerezi power plant. Kama kuna kitu nimekisahau unaweza kuongezea boss. Karibu
Screenshot_20220923_000912.jpg
 
LNG plant pekee inahitaji trillion 70?? Wewe unaelewa kweli unachoongea?
Boss mradi wetu wa LNG unagharimu pesa nyingi kidogo ni Trillioni 70.

Jaribu kusoma hili andiko hapa linaonyesha gharama za mradi ni dolla billions 30.
Screenshot_20220923_012439.jpg


USD 1 = 2332 Tsh
USD Billioni 30 =?
Screenshot_20220923_013007.jpg

USD 30B = 69.9 × 10^12 Tsh = 70 Trillioni
~
Ni pesa ndefu kidogo boss.
 
Ahsante sana kwa shule ya gesi Meneja Wa Makampuni meneja wa makampuni,

Kuna hawa wachina wa Anric gas company CNG hapo awali waliingia mkataba na DIT( Dar Institute of Technology) kutengeneza na kufanya installation ya mifumo ya gesi ya CNG kweny magari, je, serikali haiwezi kutumia makampuni yake kufanya hizo installation na kusaidia kupunguza gharama za maisha kwa wananchi hata kwa magari ya serikali na umma?

Je, ile kampuni ya pan Africa energy pale ubungo maziwa ni ya nani inahusika na kujaza CNG?

Nimeona magari ya Dangote yamefungwa mifumo ya gesi CNG je anapata wapi gesi asilia? Anamiliki mitambo yake mwenyewe?

Kwanini vituo vya gesi ni kimoja tu kipo ubungo tu? Kwanini visiwepo sehemu nyingine mikoani n.k?

Je, miradi mikubwa kama hiyo kwa nini wasipewe taasisi Kama JWTZ kwa mikakati kutokana na credibility ya taasisi zetu?

Ukiacha EWURA na mamlaka zingine, idara yetu ya usalama wa Taifa ( TISS) ina nguvu gani au uelewa gani na mamlaka na uwezo wa kushauri mambo muhimu ya rasilimali Kama gesi? Je, kuna au tuna vijana wangapi mpaka sasa katika Taifa letu waliosoma ndani na nje ya nchi na kubobea kwenye taaluma ya gesi?

Serikali inakwama wapi kubadilisha mifumo yote ya mafuta na kuweka iwe ya gesi mpaka pikipiki Kama gharama za mafuta ni kubwa?

Kwanini gesi isitumike kuzalisha umeme kurahisisha kukua kwa uchumi wa viwanda?

Ahsante sana nitaendelea kuuliza na kijifunza hapa.
Ahsante sana kwa maswali mazuri na yenye kuongeza ufahamu.

Tatizo kubwa lililopo kwenye uwekezaji katika fursa zilizopo kwenye sekta ya gesi asilia ni mtaji, ujuzi, uzoefu na utaalamu. Hapa ndipo penye tatizo, sasa ili kuweza kutatua hilo mara nyingi kampuni au taasisi zetu za wazawa zimekua zikiingia mikataba na makampuni ya kigeni ili kuunganisha nguvu ya kifedha, ujuzi, uzoefu na utaalamu. Lengo kubwa ni kupata uzoefu alafu baadaye wanajitegemea wenyewe. Ni kweli tunao mafundi wenye uwezo wa kuzibadili injini za petroli na dizeli zitumie gesi asilia na wanaofanya hiyo kazi sana sana ni wataalamu wa DIT. DIT pia wanatoa mafunzo kwa watanzania wanaotaka kujifunza fani hiyo ya kubadili injini zitumie gesi.

PanAfrican Energy Tanzania (PAET) ni kampuni tanzu ya Orca Energy. Orca Energy ni kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi iliyowekeza Tanzania. Kampuni inajishughulisha na uendelezaji na usambazaji wa gesi asilia nchini Tanzania kupitia kampuni tanzu ya PanAfrican Energy Tanzania Limited. Hivyo ndio kampuni inayo miliki na kuendesha kitalu cha gesi cha Songo Songo.

PAET iliwekeza zaidi ya TZS 14.3 bilioni kabla ya gesi ya kwanza kuuzwa, na zaidi ya TZS 219 bilioni katika uchimbaji visima, miundombinu na miradi ya mitaji tangu wakati huo. PAET inasambaza gesi inayotumika kufua umeme Tanzania na kuendeleza viwanda vikubwa jijini Dar es Salaam. Kampuni pia inasambaza gesi asilia iliyokandamizwa au shindiliwa (CNG) kwaajili ya kutumia kwenye magari.

Ni kweli kabisa magari ya Dangote yamefungwa mifumo ya CNG.
Dangote anamiliki kituo cha CNG kinachogharimu Sh billioni 21 kilichopo maeneo ya kijiji cha Hiyari Mkoani Mtwara. Imejengwa ndani ya eneo la kiwanda cha Saruji cha Dangote na ina uwezo wa kuhudumia magari 250.

Hiki kituo cha CNG cha Dangote kilijengwa mahsusi kwa ajili ya kuhudumia magari yanayomilikiwa na kiwanda cha Saruji cha Dangote. Kampuni hiyo inamiliki magari zaidi ya 2,000, mengi yakiwa ni malori yanayotumika kusambaza saruji kutoka kiwandani kwenda mikoa mbalimbali. Hivyo wanatumia CNG kama nishati ya kuendesha magari hayo.

Mbali na matumizi ya gesi kwenye malori, kiwanda hicho pia kinatumia mfumo wa gesi kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo ya kuzalisha saruji na kuzalisha umeme wa wati 750. Gesi inayonunuliwa na Dangote inatoka kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba kilichopo Mtwara. Kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba ni kiwanda kinachochakata gesi kutoka kitalu cha gesi cha Mnazi Bay.

Ni kweli kabisa vituo vya kujaza gesi asilia ni vichache. Sababu kubwa ni ukosefu wa fedha za kujenga vituo vingine. Lakini Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linampango wa kujenga vituo vitano zaidi vya kujaza Gesi Asilia iliyokandamizwa (CNG) jijini Dar es Salaam. Ahadi ya TPDC ya kuongeza vituo vya kujaza gesi hadi saba, imekuja wakati nchi ilikuwa inakabiliwa na mahitaji makubwa ya vituo kutokana na kuongezeka kwa magari yanayotumia mfumo wa gesi. Vituo vipya vya kujaza gesi asilia vinavyotarajiwa kuchochea na kuongeza upatikanaji wa CNG itakayotumiwa na magari vitajengwa kando ya Barabara ya Sam Nujoma, Feri, Muhimbili, Kibaha na Ubungo.

Serikali kupitia TPDC imewakaribisha watu wa sekta binafsi ikiwemo nawewe kuwekeza katika ujenzi wa vituo vingi vya gesi asilia katika maeneo mbalimbali nchini ili kuongeza usambazaji wa gesi na ili watanzania waweze kunufaika na sekta ya gesi asilia katika mikoa yote ya Tanzania.

Lakini pia katika kituo kipya cha kujaza gesi cha Ubungo, serikali kupitia TPDC imepanga kujenga karakana itakayofanya kazi ya kubadilisha magari kutumia mfumo wa gesi.

Kwa sasa, ubadilishaji wa magari kutumia mfumo wa gesi unafanywa na DIT pekee. Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kiasi cha zaidi ya Sh.bilioni 100 kwa ajili ya kuiwezesha DIT kujenga vituo vya umahiri ambavyo vitakuwa chachu ya kupika watalaamu wa kada mbalimbali wakiwemo watalaamu wa kufunga mifumo ya gesi kwenye magari yanayotumia mafuta ya petroli na dizeli.

Changamoto kubwa inayosababisha watu taasisi za ulinzi na usalama wasitumike nadhani ni ukosefu wataalamu wa mafuta na gesi kwenye hizo taasisi hizo. Kwasasa taasisi za TPDC, PURA na EWURA ndizo zilizopewa mamalaka kikatiba kushughurika na masuala ya mafuta na gesi kwasababu ya uwepo wa wataalamu wenye ujuzi na uzoefu katika taasisi hizo.

Kuhusiana na TISS sina taarifa kiukweli kwasababu hii ni taasisi nyeti ya serikali inayofanya kazi zake kwa siri.

Kuhusu vijana waliosomea fani za mafuta na gesi Tanzania na nje ya nchi. Sina data za idadi ya waliosomea fani hizi kwasasa. Ila kuna vijana waliosomea uhandisi wa mafuta na gesi, uhandisi wa petroli, jiolojia ya petroli, kemia ya petroli, kemia ya mafuta na gesi, uchumi wa petroli, usimamizi wa mafuta na gesi, sheria ya mafuta na gesi na uhasibu wa mafuta na gesi. Na naweza kusema kwasasa idadi ya wasomi wa mafuta na gesi Tanzania ni kubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma hivyo tunategemea watafanya mapinduzi makubwa katika sekta hii mpya.

Kiukweli ili magari yote ya watanzania yatumie gesi asilia tunatakiwa kutengeneza miundo mbinu ya kusafirisha gesi kwenda mikoa yote ya Tanzania na pia vituo vya kujaza gesi asilia vijenjwe maeneo yote ya Tanzania ili watu wenye magari waweze kujaza gesi pale wanapoishiwa. Swala la kubadilisha magari yatumie gesi lilisharuhusiwa na tayari yapo magari yaliyobadilishwa na yanatumia gesi asilia.

Kwa upande wa gesi kutumika kuzalishia umeme. Asilimia 63 (63%) ya umeme tunao tumia Tanzania kwasasa unazalishwa kwa kutumia gesi iliyo gunduliwa Tanzania. Unaweza kuona jinsi gesi asilia ilivyo saidia sekta ya nishati nchini na kupunguza matatizo ya umeme katika taifa letu.

Ahsante sana na karibu sana boss.
 
Back
Top Bottom