Tuache kufarijiana; Umasikini ni Laana, tuupige Vita

Tuache kufarijiana; Umasikini ni Laana, tuupige Vita

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
TUACHE KUFARIJIANA; UMASIKINI NI LAANA!

Anaandika, Robert Heriel

Angalizo; Kama hutaki ukweli pita kushoto sio lazima usome, Kama hutaki andiko refu pita kushoto. Kama unapenda maneno matamu matamu! Pita kushoto, leo sina hayo maneno ya uongo uongo!

Ukweli usemwe! Ukweli ndio utakaotuweka Huru! Kuna watu wanaweza nichukulie kuwa Nina Dharau, au kejeli, au dhihaka Kwa Masikini. Kisa kusema Ukweli huu. Kama vile baadhi ya Feminist wanaonipigia simu na kuniambia niache kuwasakama Wanawake. Ati ninawanyanyasa. Tangu lini Taikon awaseme wanawake wema, wenye tabia njema, wanaoheshimu miili na jinsia zao, wanaoheshimu Waume zao, tangu lini!

Ukweli ni Dawa ya kuponya watu. Uwe ukweli huo unanihusu Mimi mwenyewe, Wazazi wangu, wewe au wazazi wako, au yeyote Yule. Ukweli usemwe utusaidie.

Laana ni Tamko au Kauli inayotolewa Kwa mtu aliyeasi au kuvunja kanuni Fulani ya miungu, ili kuleta madhara, maangamizo, maumivu, majanga n.k. Kwa kifupi Laana ni adhabu itolewayo na miungu.

Laana inahusu zaidi mambo ya kiimani.
Kinyume cha Laana ni baraka.
Baraka ni zawadi kutoka Kwa miungu.

Mtu hawezi kupa Laana au Baraka bila idhini ya Miungu. Mzazi anaweza kukupa Laana Kwa sababu amepewa sehemu ya mamlaka na miungu. Ila Inategemea na sababu au kisa ulichomfanyia.

Mzazi hawezi kujiamulia tuu kukupa laana ikashika au hawezi kukupa baraka tuu ikashika pasipo idhini ya miungu.

Ndio maana mzazi hata akubariki vipi baraka zake sio chochote Kama hazijaidhinishwa na miungu.

Ili upate Laana sharti uvunje sheria Fulani ya miungu. Hiyo weka Akilini. Nilishasema awali Laana ni adhabu ya miungu.

Kuna Aina za Laana kulingana na muda na makundi ya watu. Kama;
1. Laana ya muda Mrefu/ maisha yote
2. Laana ya Muda Mfupi
3. Laana ya Watu wote
4. Laana ya Watu Fulani

1. Laana ya Muda Mrefu/maisha Yote.
Hii ni laana ambayo ukiipata itadumu mpaka mwisho wa kiumbe. Laana hii mara nyingi inaingiliana na Aina ya laana iitwayo laana ya Watu wote.
Mfano wa laana hiyo Kifo, uzee

2. Laana ya Muda Mfupi.
Hii ni laana au adhabu apewayo mtu au kundi la watu kutokana na makosa Fulani wafanyayo. Mfano Njaa, Umasikini, vita, n.k. Laana hii inaendana na Aina ya laana iitwayo laana ya kundi Fulani la watu.

Mtu unapomkosea ukampa laana yaani ukataka miungu imuadhibu basi adhabu ikitolewa inaweza kuwa Kwa muda Fulani tuu kulingana na Kosa, zipo laana za siku, wiki, miezi, miaka na zipo laana za Milele.

Kimaandiko laana za Awali zilikuwa;
1. Mauti
2. Njaa
3. Kuzaa Kwa uchungu
4. Kuishi maisha magumu
5. Mifarakano na vita.
Vita vya kindugu, kifamilia, kiukoo au kitaifa na kimataifa ni sehemu ya Laana.
6. Maradhi
Magonjwa pia ni adhabu/laana aliyopewa mwanadamu.
Ukisoma kwenye kitabu cha Kutoka na kumbukumbu la Torati inaeleza Kwa wazi Kabisa jinsi Maradhi na magonjwa kuwa ni laana.
7. Umasikini.

Ukisoma kitabu cha kumbukumbu la Torari 28, utaelewa kuwa umasikini ni laana/adhabu.

Yaani kila unachokifanya haupati, na ukipati unadhulumiwa. Kumbuka kutokupata ni laana/adhabu na kupata ni baraka. Kumbuka Biblia inasema kudhulumiwa ni laana/adhabu. Yaani utachuma Mali alafu utanyang'anywa na Mgeni/mtu mwingine.

Ayoub alikuwa Amebarikiwa Utajiri, watoto wazuri, na kila aina ya Dalili za Utajiri, lakini Mungu akamruhusu Shetani kwenda kumjaribu Ayoub, akamtia umasikini Kwa;
I. Kuharibu Mali zake na kumfilisi.
2. Kuua watoto wake na mifugo yake
3. Kumpiga Kwa Maradhi.

Yaani huo ndio umasikini OG. Kimsingi hata waliomzunguka walimuambia kuwa Ayoub anapewa adhabu na miungu kutokana na makosa aliyoyafanya ambayo hata wao hawayajui.

Unaposema Umasikini Kwa watu wenye Imani moja Kwa moja unazungumzia Laana au adhabu kutoka Kwa miungu. Hiyo ipo hivyo.

Hayo majaribu Kwa watu hutokea Kwa nadra Sana. Tena Kwa watu Wakamilifu Kama Ayoub.

Kuna watu wanasema Kuna matajiri pia Wamelaaniwa, ndio ni kweli wapo!
Kwani laana/adhabu ipo Moja. Yaani kwani umasikini ni laana/adhabu pekee zioo adhabu/laana nyingi Sana.

Miongoni mwa Laana/adhabu zingine
1. Magonjwa
Kumbukumbu la Torati 28:20
BWANA atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo.

Kumbukumbu la Torati 28:21
BWANA atakuambatanisha na tauni, hata atakapokwisha kukuondoa katika nchi uingiayo kwa kuimiliki.

Kumbukumbu la Torati 28:22
BWANA atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie.

Kumbukumbu la Torati 28:27
BWANA atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa.

2. Kugongewa Mkeo yaani kuibiwa Mke. Pia ni sehemu ya Laana.
Kumbukumbu la Torati 28:30

Utaposa mke na mume mwingine atalala naye; utajenga nyumba usiikae; utapanda mizabibu usitumie matunda yake.

3. Kukemewa na kudharauliwa na kuwa na mashaka na kutojiamini. Pia ni laana. Kwa nini udharauliwe na ukemewe kemewe unaishi Kwa hofu Kama Panya. Yaani kila ufanyalo unazomewa😀😀 yaani kwako hakuna kizuri hata kimoja hata kama unajitahidi.

Kumbukumbu la Torati 28:20
BWANA atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo.

4. Utakuwa Mkia wewe au watoto wako, na utakopeshwa na kuwa na madeni.
Kuwa mkia sio darasani tuu hata kwenye Maisha, yaani utapitwa na Fasheni😂😂, utatumia mitumba vitu Used, Daah! Hiyo ni laana tosha. Kwa nini utumie Mtumba,
Kushika Mkia ndio huko sasa, yaani huwezi tumia kitu kipya mpaka watumie watu wengine ndio utumie wewe. Avae Kwanza mwingine ndio uvae wewe.

Hiyo ni laana.

Kumbukumbu la Torati 28:44
Yeye atakukopesha, wala wewe usimkopeshe; yeye atakuwa ni kichwa, wewe utakuwa mkia.

5. Kudhulumiwa na kuonewa.
Mara hulipwi mishahara, mara unyang'anywe kiwanja au mashamba, mara umeachwa na mchumba wako sababu hazieleweki😀😀 Hilo ni tatizo usichukulie simple😊. Huwezi onewa hivihivi Kama huna Laana.

Kumbukumbu la Torati 28:29
utakwenda kwa kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.

Kumbukumbu la Torati 28:31
Ng’ombe wako atachinjwa mbele ya macho yako, usile nyama yake; utanyang’anywa punda wako mbele ya uso wako kwa jeuri, usirudishiwe; kondoo zako watapewa adui zako, usipate mtu wa kukuokoa.

6. Kuwa Malaya wa miungu.
Mara Leo upo msikitini, kesho upo Kwa Kakobe, mara mtondogoo upo Kwa waganga WA kienyeji, mwezi ujao upo Kwa Mwamposa. 😂😂 Hiyo ni laana. Yaani unahangaika Kama unawazimu.
Mtu aliyebarikiwa hawezi kuhangaika hivyo.

Mfalme Sauli baada ya kukataliwa na Mungu naye alianza kuhaha, kupagawa na kuanza kuranda randa huku na Huku. Mpaka akaenda Kwa Mganga wa Kienyeji. Ni laana ndio ilikuwa inamsumbua licha ya kuwa alikuwa mtumishi wa Mungu.

Kumbukumbu la Torati 28:29
utakwenda kwa kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.

Kumbukumbu la Torati 28:31
Ng’ombe wako atachinjwa mbele ya macho yako, usile nyama yake; utanyang’anywa punda wako mbele ya uso wako kwa jeuri, usirudishiwe; kondoo zako watapewa adui zako, usipate mtu wa kukuokoa.

7. Njaa na kiu na kutumikia Adui zako.
😀 Yaani wale unaowachukia ndio utakaokuwa unawatumikia na utakuwa unawaomba Chakula na maji ili unywe. Hiyo ni laana.

Kumbukumbu la Torati 28:48
kwa hiyo utawatumikia adui zako atakaowaleta BWANA juu yako, kwa njaa, na kwa kiu, na kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote; naye atakuvika kongwa la chuma shingoni mwako, hata atakapokwisha kukuangamiza.

Kwa kumaliza, Umasikini ni Laana tena adhabu nzito ambayo ni laana ambayo mtu anaweza kujitahidi kuiondoa Kwa sababu sio laana au adhabu ya muda wote au adhabu ya milele Kama Kifo.

Umasikini sio dhambi Ila ni laana.
Kama ilivyo Kifo sio dhambi Ila ni laana.

Umasikini ni matokeo ya makosa Kama vile uvivu, uzembe, ujinga, Maradhi, na dhulma n.k.

Vinavyosababisha umasikini ni dhambi ila umasikini wenyewe sio dhambi.
Yaani ili uwe masikini basi lazima kuna mambo uyafanye tena Kwa kujirudia rudia mambo hayo ndio huwa dhambi mfano, Kupenda ANASA kupita kiasi, uvivu, uzembe, Kuruhusu kudhulumiwa kipumbavu, Kuruhusu uonevu kijinga, ujinga n.k.

Ingawaje upo umasikini ambao ni Fungu la mtu ambao huo upo Kwa wachache Sana. Yaani kuna watu hata aonyeshe juhudi gani yeye atabaki kuwa Masikini tuu Ila Watu HAO ni wachache sana.

Na hawa wapo Kwa ajili ya kuonyesha kuwa Mungu ndiye mtoaji hata Kama utafanya juhudi gani. Zingatia, watu hao ni wachache Sana.

Namna Bora ya kupambana na Laana ya umasikini ni Kumjua MUNGU.
Kumjua Mungu na kumcha ni chanzo cha maarifa. Na watu wanaangamia Kwa kukosa Maarifa (hawamjui na kumcha Mungu)

Kwenda kanisani au msikitini kila siku sio kumjua na kumcha Mungu.
Kumjua Mungu ni kujua nature ikoje na inataka ufanye Nini Kwa wakati upi.

Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Unaweza kuwa sahihi au usiwe sahihi kutegemea na hali, mazingira na uwezo wa watu wengine kufikiri!

Kuna umaskini wa mtu mmoja mmoja na umaskini wa taifa. Maskini ni mhitaji ambaye hana uwezo wa kutatua hitaji lake. Tofauti ya maskini na tajiri ni vitu vinavyoonekana kwa macho kama vile nyumba nzuri, magari, fedha nk.

Kuna aina nyingi za umaskini.
Umaskini wa fikra au kukosa maarifa, ni mbaya kuliko aina nyingine zote.

Hata mimi pia naamini umaskini ni laana hasa ninaposoma kumbukumbu la torati sura ya 28:1...
Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana Mungu wako...., Baraka hizi zitaambatana nawe....

Sasa kama sisi ni wasikivu na watendaji wa maagizo ya aliyetuumba, kwanini tuwe maskini???
 
Ndipo yesu akawaambia ''Ni rahisi kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa mungu''
hivi alimaanisha nini hapa??

Ndipo yesu akawaambia ''Ni rahisi kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa mungu''
hivi alimaanisha nini hapa??

Zingatia Aya ya 24

Marko 10:17
Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?

Marko 10:18
Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu.

Marko 10:19
Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.

Marko 10:20
Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu.

Marko 10:21
Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.

Marko 10:22
Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

Marko 10:23
Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu!

Marko 10:24
Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, jinsi ilivyo shida wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu!


Marko 10:25
Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.

Hapo ishu ni kutegemea Mali,
Mtu anaweza akawa Tajiri lakini asiutegemee Utajiri wake. Akawa mtu wa HAKI.
Japo watu wa hivyo ni wachache.

Mtu anayetegemea Utajiri wake ni Wale ambao hupenda Rushwa, hawataki kukaa foleni au kufuata utaratibu kisa yeye anapenda au anamamlaka.
 
Mimi ni Taikon Master
Mwafyale mbon sasa ume quote Bible verse ikiwa hauna sehemu ya kufanyia ibada?

First of all (foa)..

Poverty is not the curse that Christ died for,

Umasikini sio laana ambayo Yesu Kristo alifia pale juu Msalabani

Soma:
Wagalatia 3:13-14;
Kumbukumbu la Torati 27:26; 28:15-68

Rather, this is the general curse on Adam and the land

Soma:
Mwanzo 3:17b-19a.

Kisha akamwambia huyo mwanamume, “Kwa kuwa wewe umemsikiliza mkeo, ukala matunda ya mti ambayo nilikuamuru usile; kwa hiyo, kwa kosa lako ardhi imelaaniwa. Kwa jasho utajipatia humo riziki yako, siku zote za maisha yako."

Christ died for sin, not for material wealth.

The claim that Jesus was a rich man is patently false.

Jesus wasn't a rich man.

Soma:
Luka 8:1-3;

Yohana 12:6; 13:29
 
Unaweza kuwa sahihi au usiwe sahihi kutegemea na hali, mazingira na uwezo wa watu wengine kufikiri!...

Kama vile kuwa Tajiri kunavyohitaji Musa mrefu ndivyo hivyohivyo kuuondoa umasikini kunahitaji muda mrefu.

Soma kisa cha Mfalme Daudi huyo awe Role model wako.
Jamaa ni Hustler haswa.
Mpaka kuwa Mfalme na Tajiri haikuchukua mwaka mmoja. Ni zaidi ya miaka 10.

Kumpiga kwake Goliath haikuwa ticket ya kupewa ufalme kienyeji, bado alisota na kuhenyeshwa na Mfalme Sauli akiponea chuplichupli zaidi ya mara nyingi kuuawa
 
Mwafyale mbon sasa ume quote Bible verse ikiwa hauna sehemu ya kufanyia ibada?...

Wapi nimesema Kristo amefia laana ya umasikini?

Nimeshakuambia laana zipo nyingi,
Mission ya Yesu ni tofauti na nilichokiongelea.

Yesu alikuja kukomboa Laana ya mauti ya kiroho, hilo ulijue tena uliweke akilini.
Laana ya mauti ya Kimwili hakufanya lolote.
 
Mwafyale mbon sasa ume quote Bible verse ikiwa hauna sehemu ya kufanyia ibada?

First of all (foa)..

Poverty is not the curse that Christ died for,

Umasikini sio laana ambayo Yesu Kristo alifia pale juu Msalabani

Soma:
Wagalatia 3:13-14;
Kumbukumbu la Torati 27:26; 28:15-68

Rather, this is the general curse on Adam and the land

Soma:
Mwanzo 3:17b-19a.

Kisha akamwambia huyo mwanamume, “Kwa kuwa wewe umemsikiliza mkeo, ukala matunda ya mti ambayo nilikuamuru usile; kwa hiyo, kwa kosa lako ardhi imelaaniwa. Kwa jasho utajipatia humo riziki yako, siku zote za maisha yako."

Christ died for sin, not for material wealth.

The claim that Jesus was a rich man is patently false.

Jesus wasn't a rich man.

Soma:
Luka 8:1-3;

Yohana 12:6; 13:29

Umasikini sio laana?😂😂
Umasikini Kwa Uelewa wako ni nini?
 
Wapi nimesema Kristo amefia laana ya umasikini?

Nimeshakuambia laana zipo nyingi...
Ndio maana kuna Agano la Kale na Agano Jipya,

Laana ya mauti ya Kimwili hakufanya lolote.

Wewe Bible unaisomaje unaielewa kweli au unaishabikia tu?
 
Na Ili laana ikuathiri au ikupate ni lazima uifungulie mlango.
 
Back
Top Bottom