Tuache kumlaumu Refa Kayoko kama kichaka cha kufichia Udhaifu wa Simba SC, kuanzia kikosi chake na aina ya uongozi wake

Wewe ungeongea kiswahili tu ama nawe ni diaspora😀
kwenye hii lugha napenda kukosolewa halafu ajabu wabongo wengi mnajikuta mnaijua hii lugha kumbe vikapuku tupu kwenye hii lugha!..
English haijawahi kuwa na mwenyewe hata Kiswahili watu wanakosea sana sema sisi tunajiona tupo sawa lakini ukifuatisha Kiswahili sanifu chenyewe makosa ni mengi mno!..

nachokiandika nakijua.
 
NIlitarajia kukuona ukicoment sana kwenye jukwaa la kiingereza pekee sasa wewe umeleta ugai gai hapa huoni kama hicho ni kiherehere kwenye lugha za watu kujifanya mnajua kingereza kuliko wenye nacho
 
Pamoja na Yanga kutuzidi uwezo, refa wa jana alikua tatizo mkuu...

Siwezi kulaumu sana maana haibadilishi chochote ila kuna clear penati mbili alipeta...

Tujipe muda naona kikosi kinaimarika, tujitahidi tu dirisha kubwa Mutale na Mukwala wasibaki.
We uliona Clear kwa sababu ulikuwa unaangalia kwenye TV
 
Pamoja na Yanga kutuzidi uwezo, refa wa jana alikua tatizo mkuu...

Siwezi kulaumu sana maana haibadilishi chochote ila kuna clear penati mbili alipeta...

Tujipe muda naona kikosi kinaimarika, tujitahidi tu dirisha kubwa Mutale na Mukwala wasibaki.
Lakin tukubali Refa angekua sahihi kwa asilimia 100 pande zote zingefaidika. Nafikiri Yanga angepata zaidi ya alichokipata.
 
Ni vitu vya kawaida Magori itakuwa alibeti siyo bure....!! Camara alikuwa anatimiza majukumu yake ilikuwa ni bahati mbaya tu.Hakuna wa Kumlaumu.
 
Una mtania au uko serious maana Kwa Communication skills yangu naona hapo kuna makosa mengi Sana grammatically.
Wallah Wabillah tena! Nipo serious eti!! Mimi naona jamaa anafaa kabisa kumrithi Rasi Simba!
 
Pamoja na Yanga kutuzidi uwezo, refa wa jana alikua tatizo mkuu...

Siwezi kulaumu sana maana haibadilishi chochote ila kuna clear penati mbili alipeta...

Tujipe muda naona kikosi kinaimarika, tujitahidi tu dirisha kubwa Mutale na Mukwala wasibaki.
Oky sawa, vipi umeishajiuliza ile ya Hamza na Dube kama refa angetoa nyekundu kwa Hamza alafu dakika ya 50, hali ingekuwaje kwa Simba?
 
Oky sawa, vipi umeishajiuliza ile ya Hamza na Dube kama refa angetoa nyekundu kwa Hamza alafu dakika ya 50, hali ingekuwaje kwa Simba?
Hivi, uwanjani refa anatakiwa kutumia sheria au busara?

Yaani tunyimwe penati kisa alipeta kutoa kadi nyekundu kwetu?

Tujiulize marefa husomea sheria 17 za mpira au hufunzwa busara?
 
Hakuna siku itatokea refa awe sahihi kwa asilimia 100, kwa kiasi kikubwa Kayoko kajitahidi kutenda haki. Viongozi wa Simba imarisheni tu timu vinginevyo mtapigwa tena na tena kwasababu kwa mtanzamo wangu Yanga ingekuwa gari tungesema walikuwa kwenye gia namba 2 tu.
 
Akili za kindezi ndezi ni hizi ulizoandikia hapa. We hauna kitu positive unaweza kwenda na Mo head to head ukamuongoza kusema kweli.

Ni uvunjifu mkubwa wa heshima na utovu wa nidhamu kwa mtu kama wewe kumuongelea Mo hivyo.
Vijiwe na makelele visikufanye utake kuwashusha watu na heshima wanazostahili kiasi hicho
Simba wamecheza vizuri, mwamuzi ana mapungufu yake.
Jamaa kaandika kifupi, ka review youtube uone zile penati au sio penati n.k

Unasema anajiita Dr Mo, na amesoma vyuo reputable, he earned it kijana.
 
We nae huna sense of reasoning, kama VAR ingekuwepo na refa akaamua Kwa usahihi Bado yanga angefaidika na kushinda...unawaza penalty yenu lkn ile ya musonda na Camara huioni, ile red card dakika ya 50 ya hamza huioni.
 
Unaweza ukasoma na ukakosa akili, kusoma sio busara Wala hekima, uyo Mo unayemtetea anamlaumu mwamuzi kwanini akutoka kumlaumu mwamuzi aliyeifaidisha timu yake kule Zanzibar dhidi ya Azam? Kwanini akumlaumu mwamuzi aliyewapa ushindi dhidi ya Dodoma Jiji? Ile penalty ilikuwa ni halali? Tungepima kiwango chake cha elimu yake iyo unayotuwekea hapa kama angekuwa fair kutaja pia maamuzi yaliyoinufaisha timu yake!
Unawafanyia wengine ujinga yakikukuta unatoa milio ya Kila aina!
Mechi ya ngao yule Elly sasii aliwanyima yanga magoli mangapi? Mbona yanga aikunyanyua mapanga?
Uyo Mo anasukumwa na mihemko ya kishabiki oya oya na wengine wakiamua kufufua makaburi kumjibu atokuwa na hoja yoyote ya maana zaidi ya hisia za kipuuzi!
 
Mkuu dunia ndio iko hivyo? Mi ninavyojua katika mambo ya ushindani baina ya pande mbili unaangalia manufaa yako, na ukiona haiko sawa, unadai haki yako sehemu husika.

We unataka mpira au michezo ya kimashindano iendeshwe kama dini 😆

Yani kama hapo Yanga waseme jamani hizi pointi tatu, ni makosa ya refa hata sisi tumeona, tunakata rufaa kuomba tukate hizi pointi? au mechi irudiwe? Unaona itakuwa inaleta mantiki kweli?
 
kiingereza ungeachana nacho
 
Nakubali Simba bado haijaimarika kufikia kiwango Cha miaka minne iliyopita lakini sio sababu ya kutokulalamikia maamuzi ya refa. Refa alikuwa na makosa lazima aambiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…