Uchaguzi 2020 Tuache kutetea Ujinga: Kubadili maneno ya wimbo wa Taifa na kuweka uvyama siyo sahihi

Uchaguzi 2020 Tuache kutetea Ujinga: Kubadili maneno ya wimbo wa Taifa na kuweka uvyama siyo sahihi

NDUGU CONSIGLIERE (MAFIA). NINAKUSHUKURU SANA KWA HII VIDEO, MIMI NI MWANA CCM NINAKIPENDA CHAMA CHANGU, NA KILA NAJISIFIA NACHO. LAKINI WANAPOFANYA MAKOSA SIWAUNGI MKONO NA NINA KEMEA WAZIWAZI, NISIKIKE AU NISISIKIKE. CHADEMA WAMEKOSEA SANA KUBADILI NYIMBO YA TAIFA, LAKINI MSAJILI WA VYAMA KUWA FAIR, CHADEMA HAWAKUANZA WAO , CCM NAO WAPEWE ONYO, NA USHAHIDI NI KAMA HUU NA KAMA SIO PHOTO AND VOICE EDITING.

SWALI LENGINE, HII NYIMBO NI DUA YA KUMUOMBA MUNGU, JEE WATU,TAASISI AMA HATA NCHI WANA HATI MILIKI YA MANENO YA DUA KWA MUNGU? JEE MUNGU IBARIKI CHADEMA, HAIMAANISHI WATANZANIA WABARIKIWE? JEE MUNGU MBARIKI MAGUFULI, SIO MTANZANIA ABARIKIWE?

MUNGU NIBARIKI NA IBARIKI TANZANIA
Umeongea vyema sana. Kuna hatari watu waliopo madarakani kama huyo msajili ndiyo wakawa chanzo cha vurugu kwa kauli na hatua zao. Watu hawapaswi kumuomba Mungu kwa sauti ya wimbo wa taifa, hii ni hatari sasa
 
Mkuu mbona haya maoni yako umetoa kama Mmawia?

Yani kwa vile wananchi hawakwaziki basi chadema wanaweza kufanya lolote kwenye huo wimbo?

Huwa kila mara tukidai mambo kadhaa, majibu huwa ni kuwa hayo madai hayagusi wananchi wengi. Rushwa inaathiri wananchi tena kwa uwazi, juzi wagombea karibia wote wa ccm, hasa walioongoza kwa kura wametoa rushwa, je kuna yoyote yuko mahakamani? Au huo wimbo una madhara sana ukiwekwa vikolombwezo vya jukwaani, kuliko viongozi watoa rushwa? Umeona huyo msajili wa vyama vya siasa akikemea hali hiyo?
 
Nimeona onyo la Msajili wa vyama akiwaonya CHADEMA kwa kitendo chao cha kubadili maneno ya wimbo wa Taifa na kuweka mengine.

Mwanzo sikuchukulia serious, lakini kitendo cha kuona kuwa kumbe ni kweli CHADEMA wamebadili wimbo wa Taifa na kuweka maneno yao ya uvyama vyama kwa kweli, hicho siyo kitendo cha busara na uungwana kwa Taifa.

Sote tunaisema CCM kuwa CCM ni Chama dola, kumbe kuna Chama kingine ambacho kinawaza na kuota kuwa chenyewe kiwe ndiyo Taifa Kabisaa!!. Absurd!!

Mistake kama hizi ndizo zinazoweza kuwafanya wananchi wawaone Wapinzani kama watu Fanatic, waleta vurugu, wasioheshimu alama na nembo za Taifa.

Na kwa kweli vitendo kama hivi vikionyeshwa kwa wananchi wengi, wanakuwa pissed off kwa kuwaona Wapinzani kama watu ambao ni immature!

Kuna sababu gani kwa mfano kubadili maneno ya Taifa na kuweka mengine ndani ya wimbo huo?. Kwa nini wasiimbe wimbo wa Taifa kama ulivyo ndani ya vikao vyao, kuna tatizo gani kuuchukua wimbo wa Taifa kama ulivyo?

Katika hili siwezi kuwatetea Chadema hata kidogo, Lazima waonyeshe maturity, wasiwe watu wa ushabikishabiki na bila sababu.

Hebu tazama hapa chini CHADEMA wakidistort wimbo wa Taifa na kuweka maneno yao.

Mwenyekiti Mbowe Shame on you
Katibu Mkuu wa Chadema Shame on you
Tundu Lissu Shame on you

Mmetukosea wananchi wote wenye vyama na wasio na vyama kwa kuleta mzaha kwenye wimbo unautuunganisha taifa zima kwa kuleta uvyamavyama(partsanship) kwenye suala hilo

Siku nyingine tumieni busara kwenye kufanya mambo, hakuna haja ya kutafuta unnecessary troubles!

Hebu tazama hapa wanavyoimba:

View attachment 1527225



Nilitaka kusema pia hihv hivi kuna mambo ya kubeza na yasio ya kubeza iweje wimbo wa taifa uwabilishwe maneno? Iwe sheria ipo au haipo WAMEKOSEA!

Tunapiga kelele muda wote kuwatetea harafu wanaleta issue ya hv?
 
Yani hapa na uwakika hata kura hapati yani bora kura iyaribike ila sio kumpatia mtu anaetaka sympathy na kuchafua wimbo wa taifa. Yeye ni nani kufanya ivo? Any credible persons especially going for the highest position like this hapaswi ku entertain jambo kama hili, Yan ange kuwa raisi hata ndotoni mwake inaonekana anavuruga kila kitu.

TAIFA halina kosa kama ni biff na jamaa wamalizane sio kutuharibia mambo mengine. This guy is good and damaged has to remain as a polical weapon against his political foes other than that this is wasting his time and everybody's.
 
Mleta hoja umeona hii iliyofanywa na watu wa ccm?
Hiyo unasemaje? au haina shida kwa kuwa imefanywa na ccm?
Ni vyema kabla hamjapeleka lawama ktk upande mwingine mjikague vyema ktk 'nyumba yenu'
 
Makosa yanajirudia mara mbili ndan ya wiki uwanja wa taifa walikiuka itifaki

Mkutano wao wamenajisi wimbo wa taifa


Watetez wao wanakuambia eti sio msitali ya biblia au msaafu

Huu ni utetezi wa watu wasio jua nembo yao ya taifa ni pamoja na wimbo wa taifa

Siku mkipewa nchi si mtabadili na rangi ya bendera mnaweka yenu ndio iwe ya taifa

Tuwe makini na vitu tunavyo tetea
Mtahangaika sana nyie ccm mliyofanya nyie ndio haki lkn wengine ni makosa!
 
Hio nyimbo sisi wenyewe tumeiba nyimbo ya watu na tumechomeka Tanzania tu.
 
Mleta hoja umeona hii iliyofanywa na watu wa ccm?
Hiyo unasemaje? au haina shida kwa kuwa imefanywa na ccm?
Ni vyema kabla hamjapeleka lawama ktk upande mwingine mjikague vyema ktk 'nyumba yenu'

Huko CCM limefanywa kwenye kikao gani cha Chama?

Hao waliofanya hivyo huko CCM wana taswira ya kuwakilisha chama chote au ni kakundi kadogo tu ka vijana wa UVCVM wilaya kasikojielewa?

Umewahi kusikia Msajili kaiandikia barua Chadema nzima kwa kitendo alichofanya Nusrat Hanje wa Chadema ambaye sasa hivi yuko ndani kwa kubadili maneno ya wimbo wa Taifa?

Msajili kaipa onyo Chadema kwa sababu kosa lumefanywa ndani ya vikao halali vya Chadema tena ngazi ya Taifa, na limefanywa na viongozi wake wakubwa!
 
Asante
Linapokuja suala la Taifa na tunu zake pamoja na alama zake, lazima tusimame wote kama Watanzania kuzilinda na kuzitetea bila kujali vyama vyetu.

Walichokifanya CHADEMA siyo sawa!
Wanaweza kutengeneza wimbo wao wa chama wakawa nao lakini siyo kuchukua wimbo wetu wa Taifa na kuufanyia distortion.

Ule wimbo ni Dua kwa Taifa zima, haifai kuuchezeachezea!
Acha unafiki. Leo hii huu wimbo umekuwa masahafu.
 
Huo wimbo uliacha kua wa Taifa pale walipoingiza komedi zao.

Hata mimi ninaona ilikuwa hivo. Waliamua kuomba wimbo wenye melody kama wimbo wa taifa. Labda kama waliutambulisha kama wimbo mpya wa taifa, ingekuwa issue. Tulisema melody na maneno, tunaweza kuwalaumi SA kuwa wameharibu wimbo wetu wa taifa.

Mambo mengine ni madogo sana kujali!
 
Huko CCM limefanywa kwenye kikao gani cha Chama?

Hao waliofanya hivyo huko CCM wana taswira ya kuwakilisha chama chote au ni kakundi kadogo tu ka vijana wa UVCVM wilaya kasikojielewa?

Umewahi kusikia Msajili kaiandikia barua Chadema nzima kwa kitendo alichofanya Nusrat Hanje wa Chadema ambaye sasa hivi yuko ndani kwa kubadili maneno ya wimbo wa Taifa?

Msajili kaipa onyo Chadema kwa sababu kosa lumefanywa ndani ya vikao halali vya Chadema tena ngazi ya Taifa, na limefanywa na viongozi wake wakubwa!
Msajili atakuwa amekosea kama yeye anaona kosa ni kitendo hiki kufanywa na viongozi tu. Labda angemkemea Nusrat na wale vijana wa CCM tusingefika hapa. Aidha, kama alivyoambiwa, kifungu alichotumia hakikuwa sahihi kwa sababu wimbo wa taifa sio nembo ya taifa. Pia, nchi yetu haina hati miliki ya wimbo ambao sisi wenyewe tuliutoa Afrika Kusini kama vile wenzetu wa Zambia, Namibia na Zimbabwe walivyofanya walipopata uhuru ( Namibia na Zimbabwe wameacha kuutumia). Huu wimbo unaimbwa kanisani maana ulitungwa kama wimbo wa kanisani. Kwa sababu hiyo, CDM wanaweza kusema kuwa hawakubadilisha maneno ya wimbo wa taifa wa Tanzania bali walibadili maneno wa wimbo wa kanisani, wa taifa wa Afrika Kusini n.k. Msajili angeweza kusema tu kuwa hakufurahishwa kama mtanzania na kitendo hicho na kuasa vyama vingine visifanye hivyo. Alikosea alipoongeza vitisho.

Amandla...
 
Naiona ccm ikuungana na kina UPC, na KANU
Yes asee huwa nachukia sana nikiusikiaga kule ilitakiwa wawaombe wanajeshi wawapigie kitaalam sio ule upuuzi waliofanya namna ile ndio vinapunguza hata hiyo heshima ya wimbo wenyewe
 
Wewe pambana na kutafuta wafuasi wa kuiongezea kura ACT yako na Membe wako
Kwa hiyo leo Baraza kuu la Chadema lilosheheni viongozi wa Chama kama vile Mwenyekiti, Katibu mkuu, viongozi wa Kanda wameamua kujitoa ufahama kwa sababu kuna vijana wa UVCCM wamejitoa ufahamu?

Hebu tuficheni aibu
Kosa likifanywa na vijana wa CCM wa Temeke haiwi sahihi kufanywa na Uongozi mkuu kabisa wa Chadema tena vikaoni.

Leo Role Models wa Baraza kuu la Chadema wamekuwa ni vijana hao wa UVCCM wa Temeke?

Acheni utani!
 
Pambana na ACT yako mkuu, habari za cdm wachana nazo maana cdm sasa hivi ipo hatua nyingine zaidi.
Halafu hao vijana wa UVCCM Temeke hawawakilishi CCM nzima maana ni kitawi kidogo, na hakuna ushahidi kitendo chao kina baraka za vikao vya Chama. Hao kesi yao ingeweza kushughulikiwa na BASATA au jeshi la polisi.

Ndiyo maana Msajili wa vyama vya siasa hakuionya Chadema nzima pale Nusrat Hanje alipobadili mabeno ya wimbo wa Taifa na kuweka Uchadema ndani yake, bali kesi yake imeshughulikiwa na polisi na ndiyo maana yuko Lupango hadi hivi sasa.

Lakini hili la uongozi mzima wa Chadema kubadili maneno ya Taifa tena wakiwa vikaoni hili linahusu Chama chote, kwa hiyo Msajili anaowajibu wa kuwapa onyo Chadema waache mchezo wao huo!
 
Back
Top Bottom