Uchaguzi 2020 Tuache kutetea Ujinga: Kubadili maneno ya wimbo wa Taifa na kuweka uvyama siyo sahihi

Umeongea vyema sana. Kuna hatari watu waliopo madarakani kama huyo msajili ndiyo wakawa chanzo cha vurugu kwa kauli na hatua zao. Watu hawapaswi kumuomba Mungu kwa sauti ya wimbo wa taifa, hii ni hatari sasa
 
Mkuu mbona haya maoni yako umetoa kama Mmawia?

Yani kwa vile wananchi hawakwaziki basi chadema wanaweza kufanya lolote kwenye huo wimbo?

Huwa kila mara tukidai mambo kadhaa, majibu huwa ni kuwa hayo madai hayagusi wananchi wengi. Rushwa inaathiri wananchi tena kwa uwazi, juzi wagombea karibia wote wa ccm, hasa walioongoza kwa kura wametoa rushwa, je kuna yoyote yuko mahakamani? Au huo wimbo una madhara sana ukiwekwa vikolombwezo vya jukwaani, kuliko viongozi watoa rushwa? Umeona huyo msajili wa vyama vya siasa akikemea hali hiyo?
 



Nilitaka kusema pia hihv hivi kuna mambo ya kubeza na yasio ya kubeza iweje wimbo wa taifa uwabilishwe maneno? Iwe sheria ipo au haipo WAMEKOSEA!

Tunapiga kelele muda wote kuwatetea harafu wanaleta issue ya hv?
 
Yani hapa na uwakika hata kura hapati yani bora kura iyaribike ila sio kumpatia mtu anaetaka sympathy na kuchafua wimbo wa taifa. Yeye ni nani kufanya ivo? Any credible persons especially going for the highest position like this hapaswi ku entertain jambo kama hili, Yan ange kuwa raisi hata ndotoni mwake inaonekana anavuruga kila kitu.

TAIFA halina kosa kama ni biff na jamaa wamalizane sio kutuharibia mambo mengine. This guy is good and damaged has to remain as a polical weapon against his political foes other than that this is wasting his time and everybody's.
 
Mleta hoja umeona hii iliyofanywa na watu wa ccm?
Hiyo unasemaje? au haina shida kwa kuwa imefanywa na ccm?
Ni vyema kabla hamjapeleka lawama ktk upande mwingine mjikague vyema ktk 'nyumba yenu'
 
Mtahangaika sana nyie ccm mliyofanya nyie ndio haki lkn wengine ni makosa!
 
Hio nyimbo sisi wenyewe tumeiba nyimbo ya watu na tumechomeka Tanzania tu.
 
Mleta hoja umeona hii iliyofanywa na watu wa ccm?
Hiyo unasemaje? au haina shida kwa kuwa imefanywa na ccm?
Ni vyema kabla hamjapeleka lawama ktk upande mwingine mjikague vyema ktk 'nyumba yenu'

Huko CCM limefanywa kwenye kikao gani cha Chama?

Hao waliofanya hivyo huko CCM wana taswira ya kuwakilisha chama chote au ni kakundi kadogo tu ka vijana wa UVCVM wilaya kasikojielewa?

Umewahi kusikia Msajili kaiandikia barua Chadema nzima kwa kitendo alichofanya Nusrat Hanje wa Chadema ambaye sasa hivi yuko ndani kwa kubadili maneno ya wimbo wa Taifa?

Msajili kaipa onyo Chadema kwa sababu kosa lumefanywa ndani ya vikao halali vya Chadema tena ngazi ya Taifa, na limefanywa na viongozi wake wakubwa!
 
Acha unafiki. Leo hii huu wimbo umekuwa masahafu.
 
Huo wimbo uliacha kua wa Taifa pale walipoingiza komedi zao.

Hata mimi ninaona ilikuwa hivo. Waliamua kuomba wimbo wenye melody kama wimbo wa taifa. Labda kama waliutambulisha kama wimbo mpya wa taifa, ingekuwa issue. Tulisema melody na maneno, tunaweza kuwalaumi SA kuwa wameharibu wimbo wetu wa taifa.

Mambo mengine ni madogo sana kujali!
 
Msajili atakuwa amekosea kama yeye anaona kosa ni kitendo hiki kufanywa na viongozi tu. Labda angemkemea Nusrat na wale vijana wa CCM tusingefika hapa. Aidha, kama alivyoambiwa, kifungu alichotumia hakikuwa sahihi kwa sababu wimbo wa taifa sio nembo ya taifa. Pia, nchi yetu haina hati miliki ya wimbo ambao sisi wenyewe tuliutoa Afrika Kusini kama vile wenzetu wa Zambia, Namibia na Zimbabwe walivyofanya walipopata uhuru ( Namibia na Zimbabwe wameacha kuutumia). Huu wimbo unaimbwa kanisani maana ulitungwa kama wimbo wa kanisani. Kwa sababu hiyo, CDM wanaweza kusema kuwa hawakubadilisha maneno ya wimbo wa taifa wa Tanzania bali walibadili maneno wa wimbo wa kanisani, wa taifa wa Afrika Kusini n.k. Msajili angeweza kusema tu kuwa hakufurahishwa kama mtanzania na kitendo hicho na kuasa vyama vingine visifanye hivyo. Alikosea alipoongeza vitisho.

Amandla...
 
Naiona ccm ikuungana na kina UPC, na KANU
Yes asee huwa nachukia sana nikiusikiaga kule ilitakiwa wawaombe wanajeshi wawapigie kitaalam sio ule upuuzi waliofanya namna ile ndio vinapunguza hata hiyo heshima ya wimbo wenyewe
 
Wewe pambana na kutafuta wafuasi wa kuiongezea kura ACT yako na Membe wako
 
Pambana na ACT yako mkuu, habari za cdm wachana nazo maana cdm sasa hivi ipo hatua nyingine zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…