Uchaguzi 2020 Tuache kutetea Ujinga: Kubadili maneno ya wimbo wa Taifa na kuweka uvyama siyo sahihi

Hivi kwa nini mnapenda kutanguliza matusi kuficha ujinga wako? Huu wimbo ulitokana na wimbo wa Nkosi Sikelel iAfrika uliotungwa 1897 na Padri Enoch Sontoga kama wimbo wa kanisani wa ki Xhosa. Kama kuna maneno ya kiingereza yalikuja baadae. Wimbo huu ulitumiwa na ANC kama wimbo wao na baadae kama mojawapo wa nyimbo za taifa za Afrika Kusini, mwingine ulikuwa Die Stem van Suid Afrika. Sasa hivi Afrika Kusini wameunganisha nyimbo hizo na kuongeza maneno kutoka makabila mengine. Kwa sababu hii, utaona kuwa watu wamekuwa wakiongeza na kubadilisha maneno ya wimbo kukidhi mahitaji yao toka utungwe na Sontoga. CDM sio wa kwanza na hawatakuwa wa mwisho.
Usipende kuwaita wenzako wapumbavu kwenye vitu ambavyo hata wewe hauvijui.

Amandla...
 
Sina hakika Wimbo wa Taifa siyo moja ya nembo za Taifa!
 
Komrade hawa Bavicha wasikupotezee mda wako wao wamefundishwa kukariri tu maneno ya DJ
 
Upo sahihi kiasi fulani, lakini hebu ongelea upande wa msajiri sasa yupo sahihi kuwa buyers?
 
Huu wimbo wa Taifa sio sawa na maandiko matakatifu.
Jamaa wanafanya msahafu!! Haya mambo yanaongeleka lakini si kwa panic hii as if Taifa limeigizwa kwenye vita.

Mbona wakati mtu anakiuka katiba wasiwazi ya kupiga marufuku shughuli zote za kisiasa nchini mbona Mtungi anayejiita mlezi wa vyama hatukumwona kifua mbele akiwaonya hao viongozi hao.
Ama wakati uhuni unafanyika zile chaguzi wa marudio mbona hayukuona hata kauli yeyote ile...au ndiyo ule msemo Kunya anakunya bata....wengine wanajisaidia..!!
 
Acha ujinga kule radio mawingu wanaupiga kila siku mbaya zaidi hauimbiki unavyotakiwa unaimbwa na wabana pua Nani anasimama
Ujinga unao wewe si ajbu ni uzao wa shule za kata ambapo huelewi nini maana ya wimbo wabTaifa
 
Kumbe ulikuwa wimbo wa kanisani 🤣🤣
Nyimbo za kanisani hususani Tenzi za rohoni na ZABURI hizi ni nyimbo ambazo zinaimbwa kila pahali na kwa lugha mbali mbali, sasa huyu kimeo Mutungi yaweza kuwa katumwa na CCM Ili kupitisha dumu la petrol katika moto 😂😂
Kesha anza kupata mrejesho
 
CCM Mbona hawakupewa onyo walipo badili
Hata walipozuia wengine kufanya siasa hatukuwaona mnakemea.
Unafiki wenu ni kama wa mafarisayo.
Unafiki utawapa mafanikio kwa muda tu, ila utakuachia aibu ya milele.
We shall overcome
 
Umeona nembo ya 'Adam na Hawa'' ya mbao?
Kama umeiona anzia hapo.
 
Mkuu Mimi naomba kusaidiwa,hivi ni nani mmiliki wa wimbo wa taifa? Ili ikitokea mtu akataka kuufanyia remix au kuucopy kwa matumizi Kama haya yakifanywa na Chadema Basi akaombe kibari hiko
 
..na mkutano wenyewe vyombo vya habari vilizuiwa kuutangaza hivyo hata wananchi hawakuwa na habari na kilichotokea.

Hili nalo jambo. Sasa wajue kuwa wanapobana media kutangaza mikutano ya CHADEMA wanazuia pia “makosa” yanayofanywa katika mikutano hiyo kuonekana kwa wananchi!

Hii sasa imebakia kuwa “siri” yao wao wanaofuatilia mambo ya CHADEMA kwa umakini mkubwa. Wananchi wengi hawasomi mitandao; wamebaki kushangaa mtungi analalamika nini?
 
Wimbo wa Taifa unaosemwa na mleta mada unatakiwa uimbwe wapi, wakati gani na na nani?Kama wimbo wa Taifa unatakiwa uimbwe popote, wakati wowote na mkusanyiko wowote, kosa liko wapi kama maneno mawili matatu yakiongezwa kukithi mazingira ya hali iliyopo? Wimbo wa Taifa kama unavyofahamika ukaimbwa na wananchi pale harusini au kilabuni au hata Kanisani kiongozi wa Serikali akiwepo ni sawa? Bendera ni nembo muhimu ya nchi yoyote pomoja na ya kwetu lakini viongozi wetu wa Serikali ya CCM utakuta wako danguro wamevaa mavazi yenye bendera ya Taifa kuwatambulisha lakini hakuna anayekemea. Sumu ni sumu wote wasile!
 
We kuku kwani hujaona wimbo wa CCM walioigiza wimbo wa taifa?
 
Mtahangaika sana nyie ccm mliyofanya nyie ndio haki lkn wengine ni makosa!
Mkuu kuwa mpinzani hakukupi nafasi ya kuharibu ili uzungumzwe

Unatakiwa uwe mfano kwa unao wakosoa sasa vitu vidogo tu hivyo vinaonyesha makosa je mkipewa vikubwa si mtaharibu kabisa
 
.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…