Uchaguzi 2020 Tuache kutetea Ujinga: Kubadili maneno ya wimbo wa Taifa na kuweka uvyama siyo sahihi

Uchaguzi 2020 Tuache kutetea Ujinga: Kubadili maneno ya wimbo wa Taifa na kuweka uvyama siyo sahihi

Ila Peter Msechu akibadiri nyimbo ya Dini kuweka maneno ya kumsifia magufuli iyo sawa???

Acheni double standard walichofanya chadema wala si kosa kisheria na hata pia kimaadili
Sasa wimbo wa dini unalinganisha na wa taifa?
 
Ndiyo maana Mkapa aliwaita wapumbavu na malofa.

Vitu kama hivi ndo vinafanya wananchi waone upinzani kama watu wasiojielewa

Mkapa ni nani boss, sisi wengine tunamuona ni kada wa ccm ambaye wakati fulani aliwahi kukaa rais wa nchi hii, hana maana yoyote ya kusema eti tunamchukulia kwa uzito unaoudhania ww. Ni mtu gani wa kawaida aliye nje ya madaraka ambaye anaona huo wimbo wa taifa una uzito huo? Ni kweli ni wimbo wa taifa, lakini haimaanishi chochote kwa mwananchi wa kawaida kwenye maisha yake. Hao wanaopakia maVX ya umma ndio wanaona huo wimbo wa taifa una uzito huo.
 
Wimbo wetu wa Taifa umetokana na wimbo Nkosi Sikeleli Afrika uliotungwa 1897 na Enoch Sontonga (msauzi) kama wimbo wa ANC Umetoholewa kuwa wimbo wa Taifa wa Zambia, Zimbabwe, Namibia na Tanzania Sisi wenyewe tumebadili maneno ya wimbo na copyright si yetu
 
Kiuhalisia Chadema kuna kitu wanakitafuta mana mara lisu kasema atapeleka watu road mara wimbo wa Taifa kwa maana ya nembo ya taifa wamefanyia remix juz kwenye kumpokea lisu wakasema kuna kitu sio bure mbona hawajapigwa mabomu sababu walijiandaa nikasikia tena wakajichelewesha kwenda Taifa kwenye kumuaga Mkapa ili wanachi wajue wamenyimwa kuingiza kumbe walifanya makusudi sasa yote haya wanafanya hamna mtu anajishughulisha nao kutoka serikali basi ndo inawaumiza Chadema waone kama wanakosea kuratibu mipango yao NI BORA WAJIPANGE NA SERA ZA KUJENGA NCHI NASIO MAMBO AMBAYO YANAASHIRIA UGOMVI NA CHUKI
 
kuna mambo yafuatayo

1. Si sahihi Wapinzani kufanya ya hovyo eti. kwa kuwa CCM huwa wanafanya ya hovyo

2. wapinzani ili waheshimike na wakubalike kwa wananchi inabidi wawe humble zaidi, wafanye vitu ambavyo ni modest ili kuvutia umma usiwaone watu wasiofuata taratibu na kuheshimu tunu ambazo tumeshazipokea kuwa ni tunu au alama za taifa.
CCM wanaweza kufanya upuuzi, na wakaweza kujiclear easily kwa sababu wana dola, wana all bullying pulpits za kuweza kutwist matendo yao na kushape public opinion in their favor. Wapinzani hawana hiyo luxury ndiyo maana inabidi wawe exemplary.

3. Makosa mawili hayafanyi kosa moja lisiwe kosa

4. Haifai wapinzani kuwapa CCM ammunition ya kuwaondolea credibility mbele ya wananchi. Matendo kama haya yaweka ukuta baina ya wananchi wazalendo kwa taifa lao ambao wamekua toka nursery school wakiimba wimbo wa Taifa kwa heshima zote. Leo ukireplace Tanzania ukaweka Chadema, wananchi hawa hawawezi kuwa comfortable

5. Ni makosa sana kubase argument za "mbona na CCM. hivi, au mbona CCM vile", hizo hazisaidii wapinzani. Ni tofauti sana vijana wa Temeke wasio na chama chochote cha siasa kufanya jambo fulani baya na Baraza kuu la Chadema kufanya jambo hilohilo tofauti yake ni.bingu na ardhi!

Ni kweli usemayo, lakini hakuna mwananchi wa nchi hii atawadharau cdm kisa wameimba wimbo wa taifa na kuweka neno cdm. Usije ni mihemko vya kiccm. Zaidi ya asilimia 90% ya watanzania hakuna anayekwazika kwa matumizi yoyote ya huo wimbo wa taifa, hata huo wimbo ukaupigie guest no body cares. Usitake kuja kuleta utetezi wa wasimamizi wa siasa chafu, kwa kutaka kujifanya mzalendo kumbe tapeli tu. Kawaambie ACT waimbe wakiwa wamepiga magoti ili waaminike na wananchi kisha wapewe nchi.
 
Nakuhakikishia, CCM wakiichukua hiyo clip kisha wakaiwashitaki Chadema kwa wananchi kuwa ni watu wasioheshimu alama za Taifa, wananchi wengi hawatopenda hicho kitendo.

Hapa tunajaribu kurekebisha mambo, hatufanyi haya kwa kuwa tunawachukia Chadema bali tunataka iache kufanya makosa unnecessary kama haya.. Yanaweza kuwaallaniate watu
 
Asante
Linapokuja suala la Taifa na tunu zake pamoja na alama zake, lazima tusimame wote kama Watanzania kuzilinda na kuzitetea bila kujali vyama vyetu.

Walichokifanya CHADEMA siyo sawa!
Wanaweza kutengeneza wimbo wao wa chama wakawa nao lakini siyo kuchukua wimbo wetu wa Taifa na kuufanyia distortion.

Ule wimbo ni Dua kwa Taifa zima, haifai kuuchezeachezea!
Hautaeleweka mkuu lakini usichoke kuusema ukweli.
Siyo kila mtu anaweza kuuona ukweli katikati ya mihemko ya kimakundi.
 
Nakuhakikishia, CCM wakiichukua hiyo clip kisha wakaiwashitaki Chadema kwa wananchi kuwa ni watu wasioheshimu alama za Taifa, wananchi wengi hawatopenda hicho kitendo.
Hapa tunajaribu kurekebisha mambo, hatufanyi haya kwa kuwa tunawachukia Chadema bali tunataka iache kufanya makosa unnecessary kama haya.. Yanaweza kuwaallaniate watu

Narudia tena, ni kweli cdm wanaweza kuchukiwa ila sio kwa huo wimbo wa taifa, na wala watu wengi hawaoni heshima wala fahari ya huo wimbo, bali wanaona ni wimbo kama wimbo mwingine. Asilimia 80+ ya watanzania hawawezi kuimba huo wimbo wa taifa kwa usahihi. Na watu wengi wanaona kama ni wimbo wa watu wenye mafungamano ya serikali au siasa. Simply hauna maana au uzito wowote kwenye maisha yao. Usitake kuufanya ni wimbo ambao jamii inaona fahari ya kuuheshimu, wakati sio kweli.
 
Nakuhakikishia, CCM wakiichukua hiyo clip kisha wakaiwashitaki Chadema kwa wananchi kuwa ni watu wasioheshimu alama za Taifa, wananchi wengi hawatopenda hicho kitendo.

Hapa tunajaribu kurekebisha mambo, hatufanyi haya kwa kuwa tunawachukia Chadema bali tunataka iache kufanya makosa unnecessary kama haya.. Yanaweza kuwaallaniate watu

Hahah yaani watu waache kusikitia mafao yao kucheleweshwa,ajira tangu 2015 hazitolewi kwa vijana wanaotoka mavyuoni,nyongeza za mishahara hakuna eti waje waonyeshwe clip ya wimbo wasikitike?

Hahah Nimecheka kifalaaa aisee.
 
Hicho kitendo hakipendezi, ila nitakushangaa sana kama unawashushia cdm pekee yao!

Kama umeamua kulaumu basi laumu na ccm walio anzisha hiyo tabia za kuongeza maneno kwenye huo wimbo wa taifa.

Nafikiri ni wakati muafaka kwa vyama vyetu kujali afya ya taifa letu badala ya kuangalia afya ya vyama tu.
Nimeona onyo la Msajili wa vyama akiwaonya CHADEMA kwa kitendo chao cha kubadili maneno ya wimbo wa Taifa na kuweka mengine.

Mwanzo sikuchukulia serious, lakini kitendo cha kuona kuwa kumbe ni kweli CHADEMA wamebadili wimbo wa Taifa na kuweka maneno yao ya uvyama vyama kwa kweli, hicho siyo kitendo cha busara na uungwana kwa Taifa.

Sote tunaisema CCM kuwa CCM ni Chama dola, kumbe kuna Chama kingine ambacho kinawaza na kuota kuwa chenyewe kiwe ndiyo Taifa Kabisaa!!. Absurd!!

Mistake kama hizi ndizo zinazoweza kuwafanya wananchi wawaone Wapinzani kama watu Fanatic, waleta vurugu, wasioheshimu alama na nembo za Taifa.

Na kwa kweli vitendo kama hivi vikionyeshwa kwa wananchi wengi, wanakuwa pissed off kwa kuwaona Wapinzani kama watu ambao ni immature!

Kuna sababu gani kwa mfano kubadili maneno ya Taifa na kuweka mengine ndani ya wimbo huo?. Kwa nini wasiimbe wimbo wa Taifa kama ulivyo ndani ya vikao vyao, kuna tatizo gani kuuchukua wimbo wa Taifa kama ulivyo?

Katika hili siwezi kuwatetea Chadema hata kidogo, Lazima waonyeshe maturity, wasiwe watu wa ushabikishabiki na bila sababu.

Hebu tazama hapa chini CHADEMA wakidistort wimbo wa Taifa na kuweka maneno yao.

Mwenyekiti Mbowe Shame on you
Katibu Mkuu wa Chadema Shame on you
Tundu Lissu Shame on you

Mmetukosea wananchi wote wenye vyama na wasio na vyama kwa kuleta mzaha kwenye wimbo unautuunganisha taifa zima kwa kuleta uvyamavyama(partsanship) kwenye suala hilo

Siku nyingine tumieni busara kwenye kufanya mambo, hakuna haja ya kutafuta unnecessary troubles!

Hebu tazama hapa wanavyoimba:

View attachment 1527225
 
Back
Top Bottom