Uchaguzi 2020 Tuache kutetea Ujinga: Kubadili maneno ya wimbo wa Taifa na kuweka uvyama siyo sahihi

Uchaguzi 2020 Tuache kutetea Ujinga: Kubadili maneno ya wimbo wa Taifa na kuweka uvyama siyo sahihi

Kupitia hizo nyimbo mbili, hivyo vyama viwili vinastahili viwajibishwe. Ikiwezekana vifutwe kabisa 😡😡😡😡😡
 
Wacha kujiapiza wewe hakuna kitu hapo maana hata cdm tunayo clip ya ccm wakiimba wimbo wa taifa na kuweka majina ya mwenyekiti wao.

Hakuna kutishana wao wakimwaga ugali na cdm wanamwaga mboga tu.
Nakuhakikishia, CCM wakiichukua hiyo clip kisha wakaiwashitaki Chadema kwa wananchi kuwa ni watu wasioheshimu alama za Taifa, wananchi wengi hawatopenda hicho kitendo.

Hapa tunajaribu kurekebisha mambo, hatufanyi haya kwa kuwa tunawachukia Chadema bali tunataka iache kufanya makosa unnecessary kama haya.. Yanaweza kuwaallaniate watu
 
Hautaeleweka mkuu lakini usichoke kuusema ukweli.
Siyo kila mtu anaweza kuuona ukweli katikati ya mihemko ya kimakundi.

Wanaoona umuhimu au thamani ya huo wimbo wa taifa ni wale wanaofaidi keki ya taifa huko serikalini na taasisi zake, lakini sio watu wa kawaida. Kamata vijana randomly ambao ni wengi, waambie wakuimbie wimbo wa taifa uone hata kama wanaweza zaidi ya ule ubeti mama. Au hata uwaulize heshima ya huo wimbo uone kama wanaelewa, au kuona fahari ya huo wimbo. Wangalau watu waliozaliwa kabla ya mwaka 80 ndio wanajua thamani ya huo wimbo wa taifa, lakini sio kizazi hiki cha kuvaa vimini na suruali chini ya makalio, na wavulana kuvaa hereni. Msitake kukuza jambo lisilo na uzito huo kwa jamii husika.
 
Hii video uliyoweka, hawa wanaoimba wana nafasi gani ndani ya CCM, Je kitendo chao kilikuwa endorsed na CCM, au ni rogue elements tu zimeamua kuimba?

Anyway,. makosa mawili hayafanyi kosa lisiwe kosa.

hebu linganisha kosa lifanywe na Baraza kuu zima la Chadema, Mwenyekiti akiwepo, katibu mkuu yupo na mgombea uraisi yupo nao wanashiriki kudistort wimbo wa Taifa.

Yaani Baraza kuu zima la Chadema, mbele ya mwenyekiti, na katibu mkuu wake pamoja na wajumbe wanashiriki kudistort wimbo wa Taifa

Hizi video mbili hazilingani aisee!
Zamani tulikuwa hatuvai bendera, siku hizi tunachambia bendera, na maisha yanasonga usikariri dogo, vitu vyote chini ya jua Ni ubatili tu
 
Anza na kuwalaani ccm walio anzisha huo utaratibu wa kuongeza maneno ya kumsifu mwenyekiti wao ndiyo uje kuitolea mapovu cdm
Kuna watu hawajui kwanini wimbo wa taifa ukiimbwa watu wanasimama chadema wanaweza wakaona hawajafanya kosa kama akili zao zinavyowatuma ila ni kosa kubwa wamelifanya kuelekea uchaguzi mkuu kama ni kick imebuma
 
Clip zimewekwa mitandaoni kibao, nenda Instagram utachoka mwenyewe sema tu mimi sasa hivi laptop [emoji335] yangu imezima natumia simu ningekuwekea hapa ili ujionee!
Ni viongozi gani wa CCM au ni kwenye kikao gani cha CCM walibadiri maneno ya wimbo wa Taifa?
 
Hili lichama lahovyo Sana,pindi nikiwa chuoni na baada ya kutoka nilikuwa mpenzi Sana wa cdm,
Baadae nikaja kugundua kuwa akili za kuambiwa changanya nazakwako
 
Hawa wao hawajakosea sio?
 
Kuna watu wako neutral aisee , hawazuzuliwi na sisiem hata kwa maneno au vitendo ambavyo mwenye akili anajua vinafanywa kama hadaa wapate kura, lkn pia wanaangalia Upinzani kama watu wanaostahili kupewa nchi na wala si Mamluki .

Fikiria leo wanabadili Wimbo wa Taifa, halafu wanaona haina madhara . Ni kweli kuuimba au kutoimba haubadulishi hali ya barabara zetu , au mfumo wa elimu lkn huo ndio nembo ya NCHI

Ipo siku watabadili bendera kuwa ina shida, watabadili taratibu za nchi, watabadili tamaduni na utaifa. Na kweli WATABADILI

Je Ujasiri huu unatoka wapi?
Waliona weakness ya Katiba na Sheria za Nchi. Na ZIPO NYINGI
Wanapata Ujasiri kusema kashtaki ,maana wajua hakuna kifungu kinawatia hatiani.
Lkn ukwelu HAWAFAI
Kutokomaa kisiasa kuliko pitiliza nadhani wataomba msamaha maisha yaende hakuna MKAMILIFU chini ya Jua ila WAMETELEZA

Lkn ukisiakia wanasema liwalo na liwe. Basi wenye akili watajua. Je UJASIRI HUU UNATOKA WAPI?
NANI YUPO NYUMA YAO?
Wengine sijui wamesingizia kuwa safari hii hakuna kumsubiri Mungu wananchi WATAINGIZWA BARABARANI. Ok sawa

Vyombo vyetu vya Usalama angalieni NDANI na NJE huenda seemu kinatokea Kiburi.

Tujenge vyama kama Simba na Yanga
Ushabiki Mzuri wa Vicheko mnakwaruzana uwanjani hata kurushiana mikojo lkn mnacheka mnapeana zawadi kwa kumfunga mwenzako.

Ova.
 
Ila Peter Msechu akibadiri nyimbo ya Dini kuweka maneno ya kumsifia magufuli iyo sawa???


Acheni double standard walichofanya chadema wala si kosa kisheria na hata pia kimaadili
tafakari ukiwa unaandika
hata wewe unaweza mtungia wimbo lissu
 
Mi naona kama kuna watu nyuma ya Lisu kumuhujumu tu. Haiwezekani kuwa hayupo wa kujua kitu ambacho si cha uchama halafu kishangiliwe, awe na mtu wa kumsaidia wasimharibie hapa kampeni bado.
 
Kuna watu hawajui kwanini wimbo wa taifa ukiimbwa watu wanasimama chadema wanaweza wakaona hawajafanya kosa kama akili zao zinavyowatuma ila ni kosa kubwa wamelifanya kuelekea uchaguzi mkuu kama ni kick imebuma

Ni madhara gani jamii ya watanzania watapata kwa kutokusimama wakati wimbo wa taifa unaimbwa? Juzi ccm wamegawa rushwa kama njugu na jamii inaona ni sawa tu, huku rushwa ikiwa na madhara ya moja kwa moja kwenye maisha yao. Ndio wataona kosa kutokusimama huo wimbo ukiimbwa?

Ww unajua umuhimu wa huo wimbo wa taifa, kwanini usijue umuhimu wa kuweka koma ama nukta kwenye hii post yako, ili tupime uelewa wako wa mambo?
 
Back
Top Bottom