Tuache kuvumilia wazembe, wajinga na wapumbavu makazini, wapo watanzania wengi uraiani hawana ajira

Tuache kuvumilia wazembe, wajinga na wapumbavu makazini, wapo watanzania wengi uraiani hawana ajira

samurai

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2010
Posts
11,495
Reaction score
24,223
Kama kichwa kinavyojieleza

Ni ujinga na upumbavu kuendelea kulea wazembe, wajinga, wapumbavu, wezi nk huko makazini huku mtaani kuna malaki ya vijana kwa wazee hawana ajira.

Ni wakati wa Serikali, taasisi zake, na mashirika yote yaliopo Tanzania kulibeba hili na kutolea wazembe, wajinga na wapumbavu... Taifa linazidi kuwa na watu wajinga kwa sababu ya kuleanaleana tu.

Makampuni yote ya kigeni na wawekezaji waambiwe kabisa marufuku kulea wajinga, wapumbavu na wazembe...walijue hili wanapokuja Tanzania.

Tunahitaji sasa Taifa la wakakamavu, majasiri, mahodari, wachapa kazi, watu wenye nguvu na sio blah blah zilizojaa kila kona.
 
Kama kichwa kinavyojielea..

Ni ujinga na upumbavu kuendelea kulea wazembe, wajinga, wapumbavu, wezi nk huko makazini huku mtaani kuna malaki ya vijana kwa wazee hawana ajira..

Ni wakati wa Serikali, taasisi zake, na mashirika yote yaliopo Tanzania kulibeba hili na kutolea wazembe, wajinga na wapumbavu... Taifa linazidi kuwa na watu wajinga kwa sababu ya kuleanaleana tu..

Makampuni yote ya kigeni na wawekezaji waambiwe kabisa marufuku kulea wajinga, wapumbavu na wazembe...walijue hili wanapokuja Tanzania..

Tunahitaji sasa Taifa la wakakamavu, majasiri, mahodari, wachapa kazi, watu wenye nguvu na sio blah blah zilizojaa kila kona.
Utaambiwa wewe sukuma gang,

Hiii kitu hainogi bila kusema habr za mwenda sake alivyokuwa akisimamamia kuhakikisha kila mtanzania anaishi kwa jasho lake na sifa yake ni kuwa mchapakazi

Alichukia wazembe na wavivu, alimchomoa kila aliyeonyesha uzembe kazini, kwa sasa acha turudi kwenye kukwepwa kuajiriwa na kampuni za kigeni na wakenya kuchukua nafasi zetu
 
Na kama UMEME ukikatika hovyohovyo, nani atakuwa mzembe achomolewe kazi?
........Kama mtu hakufuata taratibu za kugombea nafasi ya USPIKA na mwishowe akateuliwa kuwa SPIKA, Nani atakuwa mzembe wa kazi ili tumchomoe ktk nafasi yake?
 
Nchi ngumu sana hii.. wengi wanaostahili kuajiriwa na serikali wapo vijiweni DAAH
 
Mkuu punguza jaziba siku zako za kupata kazi zinakuja

Chief nashukuru Mungu binafsi naweza kusurvive, shida yangu ipo pale tunapolea uzembe huku kuna vijana wengi wanabrain, good altitude, more powerfully, nk wako mtaani hawatumiki.... Kuna mijitu mipumbavu, mijizi, mimalaya, miongo na kila aina ya dhambi ipo tu tunailea...
 
Nchi ngumu sana hii.. wengi wanaostahili kuajiriwa na serikali wapo vijiweni DAAH

Tunapolea wazembe, wajinga na wapumbavu ndio wao wanavyodhidi kujijengea himaya ndani ya mifumo matokeo yake smart brains wengi wanazagaa zagaa mitaani..
 
Taifa haliwezi kujengwa na watu legelege, wavivu, wazembe, wezi,waongo, wanafiki, wapumbavu, wala rushwa, watoa rushwa, malaya malaya nk..

Ipo haja sasa yakujenga jamii imara inayoishi na kuamini katika fact, jamii ya watu waelevu, watu wakakamavu nk..
 
Watu wa hivyo huogopwa na kukatwa wenye mfumo wanaogopa challenge hivyo wanataka watu dhaifu wawacontroo
 
Chief nashukuru Mungu binafsi naweza kusurvive, shida yangu ipo pale tunapolea uzembe huku kuna vijana wengi wanabrain, good altitude, more powerfully, nk wako mtaani hawatumiki.... Kuna mijitu mipumbavu, mijizi, mimalaya, miongo na kila aina ya dhambi ipo tu tunailea...

Serikalini watu wangefanya kazi kwa contract na target tungepunguza hizi mambo
 
Back
Top Bottom