Wengi wetu tumeshuhudia jinsi baadhi ya celebrities hasa wasanii na wanamuziki walivyokuwa wakishiriki si tu kwa kuonyesha mapenzi yao ya kisiasa kwa upande flani, bali pia wakivuka mstari kudhalilisha na kukebehi wananchi walio upande wa upinzani.
Hata hivyo, kuna kundi la celebrities ambao wamejizuia kuvuka mstari huo wakionekana wapo neutral, na kati yao ni Millard Ayo, mmoja wa wanahabari maarufu nchini.
Huyu Millard amekuwa akishutumiwa sana kwa kutoandika habari za machafuko na hali ya kisiasa inayoshuhudiwa. Hii imekuwa sababu ya kumshambulia kwa ukosoaji, lakini watu wanapaswa kujiuliza, je, ni rahisi kufanya wanayotaka ?
Hebu tujiingize kwa sekunde kwenye viatu vya Millard. Anapochagua kutokuwa sehemu ya kuposti habari za machafuko, kwanza kabisa akifanya hivyo tayari kaanzisha bifu na system, pili atakuwa peke yake, bila ya backup ya wanahabari wenzake wala vyombo vya habari rasmi, Hii ni hatari kubwa kwa sababu unapohusiana na habari za utata kama hizo, unaingia kwenye hatari ya kushitakiwa kwa uchochezi, kufungiwa, kuitwa polisi, n.k.
Hiki mnachotaka Millard afanye ni kuwa Mwanaharakati, tunapaswa kutambua kwamba kuwa miongoni mwa wanaharakati ni jambo lingine kabisa. Ni hatua inayoweza kuathiri maisha yake, uhuru wake, kazi yake na hata watu wa karibu anaowahudumia
Kwa hiyo, kama tunataka kumuona akifanya kazi nzuri, tuwe na ufahamu wa hali halisi na tuzingatie kwamba si kila mtu ana nafasi ya kuchukua hatua zinazoweza kumletea matatizo makubwa kwa jina la uhuru wa kusema.
Na asilimia zaidi ya 95 wanaopiga hizi kelele ni "KEYBOARD WARRIORS", ni wale watu ambao wapo active kwenye ku comment ila ni waoga sana.
Kuwa mwanaharakati ni jambo rahisi kulisema lakini kwa vitendo ni tofauti kabisa, ni kipawa.