Tuache siasa kwa maisha ya watu, Rais Samia hajaondoa tatizo la maji Dar na Pwani

Tuache siasa kwa maisha ya watu, Rais Samia hajaondoa tatizo la maji Dar na Pwani

sifi leo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
5,182
Reaction score
8,948
Watanzania tuache siasa za ngiriba ngiba hizi,

Hivi mnasema ameondoa tatizo, mnajua kuna sehemu ndani ya wilaya Ubungo tufanye wilaya ya Kinondoni ya zamani hazina maji kabisa?

Mfano eneo kama King'azi? Kifuru na Hali ya hewa haya maeneo zamani yalikuwa wilaya ya Kinondoni, kwa ngiriba za mwendazake za kutafutia watu ajira zisizo na tija wakaamua kuongeza wilaya ya Ubungo kwa kuimega wilaya ya Ubungo..

Huwezi amini haya maeneo niliyoyataja wananchi wanakunywa maji ya visima na ya chumvi.

Then Kuna jitu linamdanganya mama eti kaupiga mwingi Dar na Pwani hakuna shida ya maji? Aweso ni mchapa kazi ila ni mchongo kama wengine.
 
Hamna Rais aliotupotezea muda kama Magafuli, hiyo hela ya flyover ya Ubungo angetusambazia maji Kinondoni yote, tungemuona wa maana kwa kweli, kuliko flyover wakati unaondoa na stendi kuu ya ma Ubungo elio kua inaleta foleni pale kukurupuka ndo uliokuwa mpango mzima wa Magufuli.
 
Afadhali hayo maji ya chumvi kuliko vinyesi vya ng’ombe huku Mara.
 
Korogwe Tanga maji hayajatoka unaenda mwezi wa pili na hata siku ambazo yanatoka hua yanatoka kila baada ya siku nne kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa nne asubuhi.

Nilikua najiuliza kwanini hii sehemu ni potential kwa vitu vingi ila ipo nyuma mno angalau sababu zinajionyesha.
 
Atajuaje ikiwa kila kitu anasubiri kuletewa ofsini? Anachotaka ni sifa za kuupiga mwingi kutoka kwa wapambe wake, hana muda wa kuhakikisha hizo sifa anazopewa.
 
Wewe ndo mpuuzi maji na foleni kipi kingekua priority kwa raia, yule mzee wenu alipenda sifa sana
Kwako wewe mkaa nyumbani ukisubiri kuletewa kila kitu usingeweza kuoma adha ya foleni wakati wa asubuhi na jioni.

Utajuaje wewe?
 
na sidhani kama kuna kiongozi anaweza kuondoa tatizo lolote kwa [emoji817]
 
Back
Top Bottom