Tuache Siasa, Riba ya Mabenki ya biashara kukopesha Raia ni suala la Vihatarishi na sio maamuzi ya Serikali

Hii ni negotiable, unakaa mezani wanaangalia vigezo, Hakuna Bank utaenda sasa kichwa kichwa watakukopesha kwa asilimia 9%au 10% Tanzania

Hakuna Bank hiyo kwa sasa Tanzania, Hiyo riba ni Personal ya majadiliano sio kwa kila mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa wateja ni wachache mnoo kwenye portifolio za bank,lakini huwezi kuja na akili timamu ukasema riba za sasa sokoni ni 9% wakati zipo offered kwa kundi ambalo ni less than 1% ya wateja wote-It's a joke
 
Haitafanya kazi hilo unaloliongea labda Serikali iamue kufanya biashara

Je Chanzo kikubwa cha pesa za Bank ni kitu gani?

Chanzo kikuu cha pesa Bank ni dhamana za wateja yaani Deposits

Hawa wateja wakubwa hawaweki pesa zao Benki bure wanahitaji riba pia kutoka kwenye pesa zao

Itawezaje Bank kutoa riba kwenye deposits kwa asilimia 11 %mpaka 16% Halafu wao wanunue hati fungani za muda mfupi wapate asilimia chini 7%.Hii Itakuwa biashara kichaa

Policy zipo, Yes lakini ni ngumu kufanya kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee bank gani wanatoa deposit interest rate ya 16% kwa mtu anayeweka chini 100m ? Ukienda kuweka fixed utapewa rate za chini ya 10% per annum ila ukienda kuomba mkopo utaambiwa 18% ? Biashara ya bank bongo ni wizi uliohalalishwa kisheria tu.
 
Inaonekana wewe ni mfanyakazi wa bank hapa Tz, je serikali kushusha hiyo lending rate haiwapi ahueni yoyote kwenu mabank? Inflation Tz imekuwa stable na chini at 3-4% kwa miaka mitano sasa, lending rate government imeshusha mbona hakuna ahueni yoyote sasa? Nchi nyingine zinawezaji commercial banks zao kutoa mikopo kwa 6% na chini ya hapo tena bila longo longo yoyote.
Mimi ni mwana ccm hapa JF, Nimeandika nyuzi zingi sana za kutetea chama changu hapa JF cha CCM

Sema mzazi alinipeleka shule nzuri kusoma, Alipoteza pesa juu yangu since my early ages. Hata mimi siwezi poteza kwa mtoto wangu kama mzazi alivyochoma pesa kwangu, I say thanks to my Parents

Nayafahamu mambo kwani ninayaishi, Ila kuna wakati Tunaweka akili mfukoni kutetea chama chetu cha ccm na ndio siasa hiyo ambayo nimesema kwenye uzi Tuache siasa tujadili ukweli

Nani kasema Inflation ni Stable?

Wewe binafsi gharama za maisha unaonaje, Bei za vitu unaonaje, Ndio maana nimesema tuacha siasa

Angalia uhalisia wa maisha achana na siasa za Inflation ni stable

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tz mizinguo sana, eti hiyo ni kwa special customers walio na minimum risks ya ku default the likes of Bakhresa na Asas. Serikali inabidi itafute solution ya mikopo iwe kwa riba rafiki, riba za Tz ni wizi mtupu, mtu anapewa mkopo riba 18% halafu non reducing rate, after 5yrs analipa 90% ya mkopo kama riba so kama alichukua 100m, atalipa riba 90m, jumla aliyolipa 190m, huu kama sio wizi ni nini kwa kweli ?
Hakuna uwizi wowote, Kwenye soko huru yaani Free Market ni nguvu ya soko Inaamua, Forces of Demand and Supply

The higher the risk of default, The higher the interest adjustable to the given risk

Tanzania mikopo mfu/isiyolipika ni mingi sana pia

Kumbuka hao Special customers wana Deposit kubwa Benk pia

Mtu anaweza jadiliana na Bank mezani kama na yeye kuna kitu anakipa Bank mfano huge Deposit

Mwenye Deposit Bank Bilion 15 anaweza kunegotiate na Bank husika kuhusu rate ya mkopo na riba kwenye pesa zake

Wewe huna kitu Bank utanegotiate nini? Utashawishi nini Bank?

Weka Deposit zako uone kama hutapewa nafasi ya kujadili nao riba nzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee bank gani wanatoa deposit interest rate ya 16% kwa mtu anayeweka chini 100m ? Ukienda kuweka fixed utapewa rate za chini ya 10% per annum ila ukienda kuomba mkopo utaambiwa 18% ? Biashara ya bank bongo ni wizi uliohalalishwa kisheria tu.
Ngoja tuone-Ingawa naona baadhi wameshashusha mpaka 14%
 
Mimi ni mwana ccm hapa JF, Nimeandika nyuzi zingi sana za kutetea chama changu hapa JF cha CCM

Sema mzazi alinipeleka shule nzuri kusoma, Alipoteza pesa juu yangu since my early ages. Hata mimi siwezi poteza kwa mtoto wangu kama mzazi alivyochoma pesa kwangu, I say thanks to my Parents

Nayafahamu mambo kwani ninayaishi, Ila kuna wakati Tunaweka akili mfukoni kutetea chama chetu cha ccm na ndio siasa hiyo ambayo nimesema kwenye uzi Tuache siasa tujadili ukweli

Nani kasema Inflation ni Stable?

Wewe binafsi gharama za maisha unaonaje, Bei za vitu unaonaje, Ndio maana nimesema tuacha siasa

Angalia uhalisia wa maisha achana na siasa za Inflation ni stable

Sent using Jamii Forums mobile app
Data za World bank, IMF na BOT zote zinasema inflation rate is stable at 3-4%, mimi na wewe tuna utaalamu gani wa kubishia taasis zote hizo kubwa na makini ? Banks za Tz zinawachukulia wateja wao poaaa sababu ya serikali zetu ni dhaifu na ina mifumo dhaifu. Nitashangaa sana kama matajiri wetu wakubwa kama Mo Dewji na Bakharesa na wenyewe wanakopa hapa hapa kwa riba ya 9% uliyosema wakati wana uwezo wa kwenda kukopa hata 2-6% kwa nchi nyingi zinazojielewa.
 
Mtanzania, 🤣 🤣 🤣 Tanzania kunapikwa data hataree,IMF wenyewe walishaanza ku-smell trouble Tanzania,Unakumbuka MEKO alikuwa anatwambia uchumi ulikuwa unakua kwa kasi?Sasa hivi unamsikia Mama anasema uchumi umeanguka? Jiulize tu-Is it ok exchange rate ya 1US=2340 kuwa hivyo hvyo for years kabla na baada ya corona?
 
Inaonekana wewe ni mfanyakazi wa bank hapa Tz, je serikali kushusha hiyo lending rate haiwapi ahueni yoyote kwenu mabank? Inflation Tz imekuwa stable na chini at 3-4% kwa miaka mitano sasa, lending rate government imeshusha mbona hakuna ahueni yoyote sasa? Nchi nyingine zinawezaji commercial banks zao kutoa mikopo kwa 6% na chini ya hapo tena bila longo longo yoyote.
Yaani hawa jamaa wanapenda over profit tu hawana hoja ya msingi
 
Kwa ukubwa wa riba zetu-Ni mwizi pekee anayeweza kuziona ni za kawaida.Ukifanya analysis-Riba zetu ni kubwa East Africa na ndiyo chanzo kikubwa cha kufanya watu wakimbie kulipa mikopo
 
Riba ni kubwa sana ndio maana mikopo mingi inalipwa kwa tabu sana, biashara haiwezi kuwa nzuri na kushindana na nchi zinazojielewi kwa hizi riba za wizi wizi tu, kwanza serikali iweke sheria mikopo yote iwe na riba at a reducing rate, nilishangaa sana kuambiwa baadhi ya banks wanaweka non reducing rate, yaani Mwalimu amekopa 10m, riba 18%, mwaka wa kwanza kalipa 3M badala ya mwaka unaofuata achajiwe riba kutoka salio la 7m bado wanamtandika riba kutoka kwa 10m, huu kama sio wizi ni nn?
 
Binafsi nakuelewa sana.
 
Mtanzania, 🤣 🤣 🤣 Tanzania kunapikwa data hataree,IMF wenyewe walishaanza ku-smell trouble Tanzania,Unakumbuka MEKO alikuwa anatwambia uchumi ulikuwa unakua kwa kasi?Sasa hivi unamsikia Mama anasema uchumi umeanguka? Jiulize tu-Is it ok exchange rate ya 1US=2340 kuwa hivyo hvyo for years kabla na baada ya corona?
Uchumi wa Tz ulikuwa kwa 4.7% mwaka ulioisha wa kibajeti, hii figure ukilinganisha na nchi za Africa Tz ilikuwa ndani ya top 3, ukilingalinisha na nchi za EA tz ilikuwa ya kwanza Ila vilevile ukilinganisha na miaka iliyopita ambapo Tz ilikuwa inakuwa kwa 6-7% hiyo figure ni chini, hivyo Rais alichomaanisha apambane na madhara ya Corona turudi kwenye 6-7% , hakuna aliyedanganya ila binadamu tunatafsiri tofauti tu takwimu.
 
Tanzania wametoa Report inayoonyesha uchumi wa Tanzania unakuwa kwa 4.7%
-IMF wana estimate uchumi wa Tanzania unakua kwa 2%
-WB wao wanasema uchumi wa Tanzania unakua kwa 1%
Unaweza ukajionea mwenyewe huo mkanganyiko
 
Uchumi wa Tz ulikuwa kwa 4.7% mwaka ulioisha wa kibajeti, hii figure ukilinganisha na nchi za Africa Tz ilikuwa ndani ya top 3, ukilingalinisha na nchi za EA tz ilikuwa ya kwanza Ila vilevile ukilinganisha na miaka iliyopita ambapo Tz ilikuwa inakuwa kwa 6-7% hiyo figure ni chini, hivyo Rais alichomaanisha apambane na madhara ya Corona turudi kwenye 6-7% , hakuna aliyedanganya ila binadamu tunatafsiri tofauti tu takwimu.
Principles za Analysis and presentation ya Takwimu za kiuchumi ni zile zile ambazo zinatumika kote duniani,based on principles of official statistics-UN
 
World wide.
Sina uzoefu wa nadharia za uchumi wa siasa ( Political economy), IMF na WB ni mashirika ya kijasusi, Yakiamua nchi yako kuiporomosha kiuchumi huwa wanafanya hivyo, Kuna nchi kadhaa wamezifanyia umafia kwa Propaganda za uchumi mara hazikopesheki,

Hata kipindi fulani enzi za JPM walishaanza kuwa na mgogoro na Gov kuhusu ukuaji wa uchumi

Kiuhalisia sekta ya Fedha hapa Tanzania bado inakua, Haijafikia maturity kama Kenya

Ripoti za IMF na WB na indicator zao na vigezo vyao tuwaachie wenyewe, Let's build our own Financial culture system

Moja ya kigezo hovyo cha WB na IMF ni hiki cha kuchukua Total income/Population=Per capital income

Kigezo cha GDP ndio kina mashaka zaidi na kuna ubishani mwingi sana

Kuna nchi wana maisha bora sana na Per capital income WB na IMF wanasema ni ndogo

Mkuu mbona unayumbayumba sana 🤣 🤣 🤣 -Locus stand yako ikwapi kama msomi? wewe mwenyewe kwenye post za nyuma unaamini serikali inapika data (rejea post yako #24),alafu hapa unawapinga IMF wanaposema takwimu zinazotolewa na serikali siyo reliable-Sasa tukuamini kwa lipi? Halafu kuna mahali nimesema principles of offical statistics zimetolewa na IMF?
 
Mkuu mbona unayumbayumba sana [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] -Locus stand yako ikwapi kama msomi? wewe mwenyewe kwenye post za nyuma unaamini serikali inapika data (rejea post yako #24),alafu hapa unawapinga IMF wanaposema takwimu zinazotolewa na serikali siyo reliable-Sasa tukuamini kwa lipi? Halafu kuna mahali nimesema principles of offical statistics zimetolewa na IMF?
Yes Data zilipikwa sana wakati ule, Na sisi ndio tuliokuwa tunaeneza Propaganda Uchumi unakua na Ajira kedekede huku tukifahamu mambo magumu, Tulifahamu vijana wana hali mbaya na elimu wanayopewa haipo OK kupambana na mazingira ya teknolojia

Siasa ni tofauti na uhalisia, Siasa zinaendeshwa na watu wenye nguvu, Kama unapenda kuishi lazima uchague upande wenye usalama na maslahi

Wale wabunge unaowaona sio wote pale wapo kusimamia story za majimbo, Wengine ni chambo wa kusukuma agenda za wafanyabiashara na agenda za mtawala husika kwa wakati huo,

Umeambiwa Nenda kasifie tozo zina leta Maendeleo utampinga aliyekutuma, Hata wewe utajisikiaje mwanao Unamwambia aseme Baba na Mama wanafaa Yeye akasema hawafai, Lazima achague kuhama nyumba au aunge mkono

Unaamini shule za Private zinazidiwa elimu na shule za kata? Propaganda za kutaka watu wa amini shule za kata zina elimu bora

Je? Kuna mtoto wa wanasiasa na mawaziri wanasoma shule za kata

Propaganda Propaganda na hii ni kazi ngumu na hatari sana

Angalia Waziri wa afya na Gwajima yanayotokea sasa, Waziri wa afya alifanya Propaganda ya Covid wakati ule, Asingefanya ingekula kwake, Leo amegeuka. Ndio siasa lazima uchague upande

Tulisema na kupiga kelele kutetea maslahi na nilishaomba msamaha hapa JF

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom