Tuache tabia ya kusimamisha abiria mabasi ya mikoani

Tuache tabia ya kusimamisha abiria mabasi ya mikoani

Babeli

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2015
Posts
6,702
Reaction score
3,272
JF .

Imeniwia vigumu kukaa kimya lakini Nina hakika nitakuwa nimetoa mchango wangu kwa kulisaidia Taifa

Trafik wapo mabarabarani lakini mabasi yanapita tu na abiria wamesimama abiria anasimama mpaka masaa manne ni ajabu wenye mabasi wakifika karibu na police block wanaambiwa wakae chini kwenye korido. Wakishapita wanasimama auwanaendelea kukaa.

Sasa sijui wanamdanganya nani..trafiki wanajua mchezo huu na nimeona mabasi mengi ya mikoani yakifanya mchezo huu ni hatari sana kwa usalama wa abiria.

Serikali ilishapiga marufuku lakini binadamu sijui mpaka wafwanywaje inatia hasira. Sasa kero kubwa kwa abiria ambao wamekaa kwenye viti. Wakati mwingine Wanaminywa vilivyo sipendi kuyataja mabasi lakini mjue wananchi wanafikia mahali wanachoka.

Sasa wanapochoka mnajua wenyewe impact yake, tafadhali wajameni polisi msijisahau..simamieni hili ni wajibu wenu sio mpaka mkumbushwe

Asalaam Alaikum.
 
Kibongo bongo kawaida tu kusaidiana.

Gari ipo moja tu na unataka kuwahi ndiyo usichukuliwe maana gari imejaa!!?

Ngoja nakuongezea na hii ili ukasirike vizuri >>> tukifika kwenye mzani vioo vinafungwa vizuri tunazidi upande mmoja kisha tunarudi tena upande mwingine baada ya hapo ni gia kwa kwenda mbele
 
Kibongo bongo kawaida tu kusaidiana...

Gari ipo moja tu na unataka kuwahi ndiyo usichukuliwe maana gari imejaa!!?

Ngoja nakuongezea na hii ili ukasirike vizuri >>> tukifika kwenye mzani vioo vinafungwa vizuri tunazidi upande mmoja kisha tunarudi tena upande mwingine baada ya hapo ni gia kwa kwenda mbele
Unavyoongea kwa majivuno kama vile kuna mtu unamkomoa. Kusimamisha abiria hasa masafa marefu ni hatari mno.

Panapotokea ajali, abiria aliesimama yupo kwenye hatari zaidi ya kudhurika yeye na kusababisha athari kwa waliokaa pia.
 
Juzi nilivoenda mwanza hii issue nimeiona nilishangaa sana mtu anawezaje kutoka shinyanga hadi Dar amesimama???? Wakikaribia kwenye mzani wanashushwa kwanza

Nadhani ni Hali ya maisha tu hawatoi nauli kamili.
 
Unavyoongea kwa majivuno kama vile kuna mtu unamkomoa. Kusimamisha abiria hasa masafa marefu ni hatari mno.

Panapotokea ajali, abiria aliesimama yupo kwenye hatari zaidi ya kudhurika yeye na kusababisha athari kwa waliokaa pia.
Nasikia ikitokea ajali ya kugongana uso kwa uso ,abiria waliosimama wanachomoka kurushwa mbele kwa kasi ya risasi.
 
Nasikia ikitokea ajali ya kugongana uso kwa uso ,abiria waliosimama wanachomoka kurushwa mbele kwa kasi ya risasi.
Ni kweli na sio kuchomoka tu wanaweza hata kuwaangukia na kuumiza wengine pakitokea mshtuko aidha wa ajali au kusimama ghafla.
 
Wakati. Mwingine maagent wanazingua, Gari imejaa anakuuzia tuu, hata afanyi mawasiliano na Kondakta.

Siku moja nawahi Mwanza nakimbia Baridi la Iringa. Nimefika pale stendi nikakatiwa tiketi gari zinazotoka Mbeya.

Gari inafika iko full, ikabidi tufaurishwe gari nyingine, nayo tulisimama.nNilikuja kupata Siti tulipofika Singida.

All in all kusimama sio poa ni kero na hatari kwa Abiria wengine na wewe mwenyewe.
 
Serikali ilishapiga marufuku hii tabia kwanini inajirudia...Kuna watu sehem zao hawatimizi majukumu yao,. Na kwa Hilo ni Traffic police..Wala hatuwaonei aibu kuwaambia..jipangeni mkomeshe tabia hii...lazima watu wafuate taratibu zinazowekwa
 
unasimama kama vipi usipande basi lisilo na siti ya kukaa.
 
Dawa faini ni kwawote, abiria alisimama na wenye gari
 
Haa mabasi ya songea dar. Tena hawa ndio hawaogopi trafiki kabisa, anapita mbele ya trafiki na vioo viko wazi abiria wamesimama wengine wamekaa kwenye korido. Trafiki mwenyewe hathubutu kuingia ndani ya basi.
 
Pia super feo ya kutoka mtwara kwenda mbeya kupitia songea inasimamisha Sana abiria ikifika masasi na wanachukulia kawaida TU hawaogopi ht askar
 
Mabasi ya chaka hayo sio mkoa to mkoa au ruti haina magari mengi
 
Hivi kweli serikali ikiweka faini kubwa kwa kosa ambalo umelifanya makusudi unadhani hilo tatizo litajirudia.
 
Pia super feo ya kutoka mtwara kwenda mbeya kupitia songea inasimamisha Sana abiria ikifika masasi na wanachukulia kawaida TU hawaogopi ht askar
Na mimi ndio nawazungumzia hayo hayo. Kuna siku nimeshuhudia spfo ya Songea Dar abiria wamesimama kutoka njombe hadi iringa.
kuna mwingine akalala kwenye korido kutoka iringa hadi Morogoro.

Katika safari nzima hakuna trafiki aliyeingia kukagua. Lakini kuna siku nimepanda basi ambalo halina jina kubwa kutoka DSM hadi Kyela, kutoka mbezi haadi Makambako tu hapo trafiki waliingia ndani ya basi mara 2 na uhamiaji mara moja.
 
Back
Top Bottom