Tuache tabia ya kusimamisha abiria mabasi ya mikoani

Tuache tabia ya kusimamisha abiria mabasi ya mikoani

JF .

Imeniwia vigumu kukaa kimya lakini Nina hakika nitakuwa nimetoa mchango wangu kwa kulisaidia Taifa

Trafik wapo mabarabarani lakini mabasi yanapita tu na abiria wamesimama abiria anasimama mpaka masaa manne ni ajabu wenye mabasi wakifika karibu na police block wanaambiwa wakae chini kwenye korido. Wakishapita wanasimama auwanaendelea kukaa.

Sasa sijui wanamdanganya nani..trafiki wanajua mchezo huu na nimeona mabasi mengi ya mikoani yakifanya mchezo huu ni hatari sana kwa usalama wa abiria.

Serikali ilishapiga marufuku lakini binadamu sijui mpaka wafwanywaje inatia hasira. Sasa kero kubwa kwa abiria ambao wamekaa kwenye viti. Wakati mwingine Wanaminywa vilivyo sipendi kuyataja mabasi lakini mjue wananchi wanafikia mahali wanachoka.

Sasa wanapochoka mnajua wenyewe impact yake, tafadhali wajameni polisi msijisahau..simamieni hili ni wajibu wenu sio mpaka mkumbushwe

Asalaam Alaikum.
Super feo ya Songea Masasi Mtwara ni shida...kuanzia Namtumbo hadi Tunduru full abiria kusimama...abiria wengine wanatoka shambani na mikungu ya ndizi wanaenda kijiji cha mbele nauli ya buku yani hakuna tofauti na daladala kila kjj ni kushusha na kupakia
 
Ikitokea ajali hawa wanaosimama nadhani ndio wanaokufa. Haya mabasi maarufu ndio abiria wanajaa hadi kusimama na hawaogopi trafiki.

Kuna siku nilikuwa naenda zangu njombe kwa bahati mbaya nimechelewa, nikajipandia zangu KYELA hadi Makambako then nikadandia ABC hadi Njombe.

Ingawa hatukupewa vitafunwa na siti zimechakaa, lakini safari ilikuwa nzuri na huduma nzuri. Na kuna siti zilienda empty hadi Makambako.
Wanapenda selous na super feo asikuambie mtu, hayo magari mengine siti zinakuwa empty lkn hawapandi,
 
Super feo ya Songea Masasi Mtwara ni shida...kuanzia Namtumbo hadi Tunduru full abiria kusimama...abiria wengine wanatoka shambani na mikungu ya ndizi wanaenda kijiji cha mbele nauli ya buku yani hakuna tofauti na daladala kila kjj ni kushusha na kupakia
Nipo zangu Tunduru nikakata tiket ya feo masasi to songea,,gari imeingia Tunduru imejaa hatari,

Nikamwambia konda nilikotoka ni mbali sana siwezi kusimama, konda akazama ndani ya bus akamchomoa mnyonge na akamuuliza unashukia wapi? akasema namtumbo,

akamwambia hii siti ni ya huyu dada Simama akae mwenye siti yake[emoji23],akasimama nikakaa zangu,kufika songea gari ikashusha,nikasuubiri feo ya mtwara to mbeya nikadandia hadi shule ya Tanga, nikasubiri feo inayotoka mbeya to mbinga nilipata siti tena ya dirishani mwenyewe alishuka kushangaa[emoji23]alivyorudi ndani ya gari kakuta nimekaa,akasimama hadi mwisho was safari

Kwanza niseme tu super feo/selous nazipenda,najua nikiwepo huku kusini popote nitakapokwenda feo inanifikisha.
 
Abiria wanatakiwa wajitambue,kuna siku nilipanda basi toka Wilaya moja ya mkoa wa Morogoro kuja Dar,kufika mizani wanatuambia tutoke siti za nyuma tuje mbele ili kubalance mizani...nikagoma,nikawaambia kama ni faini mpigwe ili mjifunze,..siwezi lipa nauli then nipate usumbufu.
Umenikumbusha mwaka 2018 nilipanda Buti la Zungu Dar Lindi, kufika mizani ya kule mbele wakatuambia abiria wa kule nyuma watuchukulie bodaboda tukapandie mbele kwa vile eti watapigwa faini kwa ajili ya uzito, halafu wanatuambia kirahisi tu.

Kuna abiria walianza kukubali lakini mimi niliwawashia moto nikasema kwanza hicho kipengele kwenye tiketi hakipo pili mimi abiria sina hasara au faida kama wao wakililipishwa faini kwa ajili ya uzito, hivyo kama wanataka kukwepa hilo watulipe hela au watupunguzie nauli.
Abiria wenzangu wakaniunga mkono, mwisho wakaamua kushuka wao halafu baadhi ya abiria wakasogea mbele
 
Usumbufu wa kijinga sana,

yaani ukiwakazia wanakuwa wapole balaa,kama abiria ni mnyonge utapelekeshwa balaa[emoji23]
 
Back
Top Bottom