Tuache tabia ya kusimamisha abiria mabasi ya mikoani

Haa mabasi ya songea dar. Tena hawa ndio hawaogopi trafiki kabisa, anapita mbele ya trafiki na vioo viko wazi abiria wamesimama wengine wamekaa kwenye korido. Trafiki mwenyewe hathubutu kuingia ndani ya basi.
Hawez ingia ndani sababu anajua basi limefulika...na labda chochote kitu ameshatanguliziwa....
 
Ina maana trafik wanajua wanachokifanya..gari jipya linakuwa halijapata network ya mchongo,. Hilo lazima walisumbue mpaka liingie kwenye 18 likae mguu sawa...hahaha..Askari wetu oneni aibu Basi tekelezeni wajibu wenu..tunawapenda mnachapa kazi Ila kwa haya Mambo ni aibu...Mambo yanakuwa holela tu Sasa mbona huko nyuma mlikuwa mmenyooka..
 
Dar to mwanza wana hii tabia
Baadhi ya basi haziingii stend ya manyoni uhuni uhuni tuu

Hao abiria walio simama ni hela ya dereva na kondakta
 
Kuna baadhi ya mambo tunasababisha sisi abiria wenyewe unapokeaje tiketi haina namba ya gari haina namba ya siti haina mawasiliano ya mtoa tiketi Abood na new force za Dar to Morogoro nishawazingua sana

Nimewahi ubungo nataka nipate siti nirelax wapiga debe wakanipakia kwenye Abood juu juu nafika mle gari imejaa hadi mlangoni hapo gari ishatoka ipo juu kwenye interchange za ubungo nikamfata msimamizi nikamwambia nitakupa elfu 6 tu hadi Morogoro kama hutaki nishushe mbezi kalalamika weee kufika mbezi nikamwambia nishushe akasema hawasimami mbezi na mimi nikamjibu nitakupa elfu 6 kufika chalinze nikamlipa elfu 6.

Newforce ya dar to Morogoro walininyima tiketi halafu nikae ile siti ya pale mbele mlangoni nikaanzisha vagi kumbe ile siti haina tiketi nikashitaki kwa trafiki yupo anacheka tu nikadai nauli nikashuka baada ya dk 5 nikadaka gari nyingine wakanipa siti na tiketi
 
wewe acha kimbelembele sisi wenyewe tuna enjoy cha msingi niende na muda hakuna sehemu imeandikwa kwamba ukisafir lazima ukae.

huo usalama kama upo upo tu acha kimbelembela kijana ...
 
Wakati mwingine inatokea tu hebu jaribu kufikiri umetoka zako labda home kwa wazazi na ulienda sababu ya matatizo kupata gari ni mpaka uunganishe. Unafikiri utasubiri upate seat ndo uondoke?
Sina uhakika kama wengi wa wasafiri wanapenda ila issue ni umuhimu wa hizo safari na muda ndo maana watu wnaasimama.
 
Dawa faini ni kwawote, abiria alisimama na wenye gari
Huyo faini ya abilia wengi wataishia jela maana wengine hata hela yakula njiani hana! Labda akikosa pesa yakulipa apewe viboko
 
Naunga mkono hoja.
 
Newton’s first law states that if a body is at rest or moving at a constant speed in a straight line, it will remain at rest or keep moving in a straight line at constant speed unless it is acted upon by a force ina maanisha kwa mfano ikiwa gari inakimbia km 80/hr halafu ikashika break ghafla wewe uliesimama kwa speed ile ile utajipiga piga sasa imagine my point is there you can gues anyway.
 
wewe acha kimbelembele sisi wenyewe tuna enjoy cha msingi niende na muda hakuna sehemu imeandikwa kwamba ukisafir lazima ukae.

huo usalama kama upo upo tu acha kimbelembela kijana ...
Ndio maana hatuendelei..mawazo gani mbinuko haya
 
Haa mabasi ya songea dar. Tena hawa ndio hawaogopi trafiki kabisa, anapita mbele ya trafiki na vioo viko wazi abiria wamesimama wengine wamekaa kwenye korido. Trafiki mwenyewe hathubutu kuingia ndani ya basi.
Hivi ni kwanini[emoji23]

Songea mbeya abiria wamesimama hata hewa hakuna,trafik akawa anakunua tu na kusema hii too much,mie nilijua watashushwa,,trafik akasema tu safari njema[emoji23]
 
Pia super feo ya kutoka mtwara kwenda mbeya kupitia songea inasimamisha Sana abiria ikifika masasi na wanachukulia kawaida TU hawaogopi ht askar
Kwa super feo hii ni kawaida sana na hawafanywi kitu,

Shida ni abiria wenyewe,magari mengine yapo hawapandi,wanataka super feo tu,
 
Hivi ni kwanini[emoji23]

Songea mbeya abiria wamesimama hata hewa hakuna,trafik akawa anakunua tu na kusema hii too much,mie nilijua watashushwa,,trafik akasema tu safari njema[emoji23]
Ikitokea ajali hawa wanaosimama nadhani ndio wanaokufa. Haya mabasi maarufu ndio abiria wanajaa hadi kusimama na hawaogopi trafiki.

Kuna siku nilikuwa naenda zangu njombe kwa bahati mbaya nimechelewa, nikajipandia zangu KYELA hadi Makambako then nikadandia ABC hadi Njombe.

Ingawa hatukupewa vitafunwa na siti zimechakaa, lakini safari ilikuwa nzuri na huduma nzuri. Na kuna siti zilienda empty hadi Makambako.
 
Ndio maana hatuendelei..mawazo gani mbinuko haya
😀😀😀 kwamba mawazo mbinuko ?

sasa wewe unataka tuendelee kwenda wapi ?

kuendelea ni kusafir umekaa au mimi ndio sielewi ?
 
Abiria wanatakiwa wajitambue,kuna siku nilipanda basi toka Wilaya moja ya mkoa wa Morogoro kuja Dar,kufika mizani wanatuambia tutoke siti za nyuma tuje mbele ili kubalance mizani...nikagoma,nikawaambia kama ni faini mpigwe ili mjifunze,..siwezi lipa nauli then nipate usumbufu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…