Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,256
- 44,597
Ni makosa makubwa kukataa kinachoendelea kwa sababu Samia ni Mzanzibari. Ukikubali hili unataka kusema kama kingefannywa na "Mmatumbi" mwenzetu basi kisingepingwa. Ni ufyatu kusema kuwa haya yote yangefanywa na mgombea wa CCM toka Bara basi watu wasingelalamika na kuasi mioyoni.
Yaani, itokee tufike kwa kukunjana mashati hadi 2030 basi tukiwa na mgombea wa CCM toka bara basi na akafanya haya tena watu waseme huyu ni "mbara"!
Kinachopingwa na kukataliwa ni CCM na makuwadi wake. Hakihusishi ndugu zetu Wazanzibari na tuwakatalie wale wote wanaotaka kuangalia hili kwa minajili ya Ubara na Uzanzibari. Tusiruhusu wazanzibari walioko bara walengwe ati kwa vile wanatoka sehemu moja na Samia..huu ni ufyatu!!
Samia na wale wanaomwezesha wakatiliwe kwa sababu ya sera, mipango na uongozi wa hasa kwa makosa makubwa manne waliyoyafanya na wanayoendelea kuyafanya hadi sasa. Maana ukishaangalia hili kwa Ubara na Uzanzibari utajikuta unauangalia kwa udini. Hili likataliwe.
MMM