Tuache Unafiki: Bashe alichukua hatua sahihi kumaliza tatizo la sukari. Hongera Dr. Tulia kwa kumlinda na kulinda maslahi ya nchi

Tuache Unafiki: Bashe alichukua hatua sahihi kumaliza tatizo la sukari. Hongera Dr. Tulia kwa kumlinda na kulinda maslahi ya nchi

Hivi mna ukichaa????? .

Mnadhani Late JPM, alipoamua kufufua vya kwetu Hakua na akili??.
We ndio kichaaa, kwani huyo JPM alipowapa jeshi na TIB tender ya kuuza korosho alitangaza tender lini na wapi? Ila cha ajabu JPM mnasema ni mzalendo ila kitu hiko hiko akifanya bashe ni ufisadi.

Hata JPM angekua hai angefanya hiko hiko alichofanya Bashe
 
Nayajua majibu ya hayo maswali yote. Narudia tena, nimefanya kazi Kilombero sugar, Mtibwa sugar na Kagera Sugar. Wewe unasimuliwa hayo mambo, mimi nayajua kwa undani.

Uhaba wa sukari ulitengenezwa na wazalishaji wa sukari wenyewe wakitegemea ku exploit fursa ya wao kuwa waagizaji pekee wa sukari toka nje kwa ajili ya kufidia pengo lililopo kwenye uzalishaji.

Kwahiyo watu hao hawawezi kuwa part ya solution. Kuhusu nini kitatokea baada ya kujaza sukari ya bei nafuu kwenye soko ni hao wazalishaji kujifunza na kutorudia ujinga huo.

Some people can only learn the hard way. Walitegemea super profit sasa wanakwenda kula hasara. Hawatarudia ujinga huo next time. Na waziri kawaambia waziwazi, warudie waone.

Huyo Mpina hawezi kuwasidia. Waache konakona wafanye wajibu wao, kama umewashinda basi waachie hivyo viwanda wapewe wengine wenye uwezo wa kuendesha.
Mkuu unaposema viwanda vinatengeneza uhaba wa sukari, unamaanisha viwanda VINAACHA kuzalisha sukari au vinazalisha sukari then vinaificha?

Keeping in mind kwamba viwanda vyote vinatuma report zake za uzalishaji serikalini kila wiki?
 
We ndio kichaaa, kwani huyo JPM alipowapa jeshi na TIB tender ya kuuza korosho alitangaza tender lini na wapi? Ila cha ajabu JPM mnasema ni mzalendo ila kitu hiko hiko akifanya bashe ni ufisadi.

Hata JPM angekua hai angefanya hiko hiko alichofanya Bashe
Points zinaenda vizuri lakini pia usidanganye, Jwtz haijawahi kuuza korosho, Bali walisimamia uuzaji na usambazani. Ahsante
 
Tukisema nyuma ya hizo kampuni uchwara, Kuna Fedha HARAMU za watu wachache , tutakua tumekosea?.
Fedha haramu alafu wakipewa tender wauze kwa bei ndogo? Sasa wanafidiaje walichohonga? Kuna watu akili hamna kabisa.

Yaani sukari kilo moja elfu 8 ghafla watu eti wahonge ili wauze kilo moja elfu 3.5?? Sasa hiyo rushwa ina faida gani?

Kuna claims ni upuuzi tu, suppliers wakiwa wengi bei hushuka sababu demand hupaa. Sasa unahonga wakati huwezi break even maana sukari ni nyingi kuliko walaji?

Mimi ningeamini kuna rushwa kama Bashe asingeagiza sukari ili tuendelee kuuziwa elfu 8!!
 
Ok, wewe unayeijua sekta hii vizuri tusaidie ufafanuzi wa hoja hii,

Wazalishaji wa sukari walimtaarifu waziri kwa barua juu ya uhaba wa sukari tangu mwezi novemba kutokana na uwepo wa elnino. Wakamkumbusha tena Desemba, akatoa vibali Februali akitaka sukari iwe imeingizwa ndani ya siku 14 jambo ambalo anajua haiwezekani. Hoja,

1.Je kati ya waziri na wazalishaji nani alisababisha uhaba wa sukari?

2. Kwa nini alichelewa kutoa vibali na baadae akavitoa akijua kwa muda huo wazalishaji hawataweza kuingiza sukari na badala yake akatengeneza kampuni zake za mfukoni zisizo na sifa kinyume na Sheria na kuzipa tenda ya kufanya biashara ambayo hawaijui na hawajawahi kuifanya?

3. Kwa nini hata kiwango cha sukari iliyopendekezwa na bodi kuingizwa tani laki 3 waziri alizidisha na kuingiza tani laki 4.1

4. Kwa nini Waziri mwenye vyombo vya dola alishindwa hata kutangaza rasmi na kusimamia bei elekezi hadi sukari hiyo hiyo iliyoagizwa kwa vibali vyake ikauzwa sh 10,000 kwa kg huku akiwa ametoa msamaha wa kodi kwa makampini hayo ya mfukoni hayo? Ni hasara kiasi gani taifa limepata au fedha kiasi gani hayo makampuni ya mfukoni (utakatishaji) wameifisidi serikali?

5. Je wewe unaonaje hali ya usalama kwa taifa kwa mtu asiyejua UBORA wa kitu chenyewe kupewa kazi hiyo hata bila kuthibitishwa na vyombo husika, kampuni za simu, stationary, store, nk zenye usajili tata na mtaji usiozidi 1,000,000. Huu ni utakatishaji wa fedha ulio dhahiri.
Luhaga Mpina hana point ni wakala wa matajiri wahodhi sukari tu. Sisi tunataka sukari iwepo kwa bei rahisi bila kujali imekujajaje. Hata wewe denoo JG mwenye leseni ya kusuka nywele ukileta sukari tunanunua. Bashe shikilia hapo hapo mpaka hawa sukuma gang wa mwendazake wanyooke
 
Ndugu kwanza mi siyo sukuma gang, fuatilia vizuri maoni yangu ktk nyuzi mbalimbali utanifahamu.

Kusema tu kuwa Mpina hana point haiondoi uzito wa hoja zake hata kama atakuwa ametumwa, weledi ni kuleta hoja nziito kinzani dhidi yake.

Inawezekana wazalishaji wa sukari walikuwa na nia ya kutengeneza uhaba wa sukari ili wajinufaishe, ktk nia hiyo ya wazalishaji inaonyesha upo uwezekano mkubwa wa waziri kuwa naye alitumia nafasi hiyo hiyo kuwa "win" na kujinufaisha.

Wewe unayesema ilimradi tu sukari umeipata bila kujali imepatikanaje, nina wasiwasi na wewe kuwa hata haujui maana ya utakatishaji fedha, uhujumu uchumi lakini pia hauna uchungu na Kodi za wananchi maana ktk hii serikali imepoteza kiasi kikubwa cha Kodi.
 
Kwamba Mtu ambaye shughuli zake zote ni Sukari, ashindwe kuingiza Sukari, badala yake mtu wa STATIONARY mwenye mtaji wa million Moja, Aweze kuleta Sukari Tani na matani??.
Shida iko wapi mwenye leseni ya Stationery kapewa kibali cha kuleta sukari na kaleta sukari?

Huyo DIKTETA wenu mbona aliwapa USD 50 Million kwa ajili ya kununua mashine za kiwanda cha sukari cha Mkulazi?

Bashe katoa vibali tu kwa Itel ila hela ni za kwao. Lakini Magufuli mnayemuona ni wa maana alitoa hela za Serikali kwa TANROADS kununua mitambo ya sukari. Are you CRAZY?
Screenshot_20240623_213731_Chrome.jpg
Screenshot_20240623_213840_Chrome.jpg
Screenshot_20240623_213610_Chrome.jpg
 
Shida iko wapi mwenye leseni ya Stationery kapewa kibali cha kuleta sukari na kaleta sukari?

Huyo DIKTETA wenu mbona aliwapa USD 50 Million kwa ajili ya kununua mashine za kiwanda cha sukari cha Mkulazi?

Bashe katoa vibali tu kwa Itel ila hela ni za kwao. Lakini Magufuli mnayemuona ni wa maana alitoa hela za Serikali kwa TANROADS kununua mitambo ya sukari. Are you CRAZY?
View attachment 3024113View attachment 3024114View attachment 3024115
Hapa ndipo nazidi kuona kuwa una tatizo la uelewa,

1. Sheria na kanuni za manunuzi kazisome uone tatizo lilipo.

2. Kifanyika kwa kosa moja hakuleti uhalali wa kufanyika kwa kosa lingine, kwamba eti kwa kuwa Magu alifanya kosa basi na Bashe naye hata akifanya iwe ni sawa tu. Hii ni kwa watu wakinga tu.
 
Ukweli mtupu, watanzania ni watu wa ushabiki kwenye kila jambo. Ukitazama hii issue bila kuwa biased Bashe alichukua hatua sahihi kulinusuru taifa.
Hapa issue sio kuwa biased, issue ni je kile ambacho Mpina kakiweka kwenye nyaraka kina ukweli gani??

Na je msema uongo ambatanishe mpaka nyaraka?!

Facts huwa zinaenda kwa facts,
 
Hapa ndipo nazidi kuona kuwa una tatizo la uelewa,

1. Sheria na kanuni za manunuzi kazisome uone tatizo lilipo.

2. Kifanyika kwa kosa moja hakuleti uhalali wa kufanyika kwa kosa lingine, kwamba eti kwa kuwa Magu alifanya kosa basi na Bashe naye hata akifanya iwe ni sawa tu. Hii ni kwa watu wakinga tu.
Wewe unadhani wananchi wanataka hizo sheria zako? Wananchi wanataka sukari ya bei rahisi, period. Hizo siasa zenu na longolongo peleka huko
 
2. Kifanyika kwa kosa moja hakuleti uhalali wa kufanyika kwa kosa lingine, kwamba eti kwa kuwa Magu alifanya kosa basi na Bashe naye hata akifanya iwe ni sawa tu. Hii ni kwa watu wakinga tu.
Kuhusu Magufuli hapa ni kwa kuwa Carlos The Jackal amesema eti Magufuli asingeweza kufanya kuzipa vibali vya kuleta sukari kampuni ambazo hazi deal na sukari. Nimi nikaamua kumkumbusha na kumpa uozo wa Magufuli
 
Back
Top Bottom