Tuache ushabiki na unazi, benchi la ufundi Simba lijitathmini kabla mambo hayajaribika

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Leo tumeshinda kwa mikwaju ya penati lakini ukweli lazima usemwe, timu yetu haichezi mpira unaovutia, ni ukweli usiopingika kuwa kikosi chetu kina watu wa kazi hasa ambao wana uwezo wa kuleta mataji ya kila aina lakini mfumo anaoutumia Robertinho unaikosesha Simba mabao.

Hivi kweli Simba hii ni ya kucheza mechi 2 bila kufunga goli? Robertinho aaambiwe kama wachezaji hawana uwezo apendekeze, kwanini Kanoute apungue makali wakati tuna Abdallah Hamis?

Timu haichezi mchezo mzuri kabisa, mpira tumeelemewa na Yanga mwanzo mwisho Leo.
 
Kwa kweli uwezo wake wa kupanga wachezaji nani acheze kwanza na nani aingie baadae ni mdogo sana.

Mifumo yake ya uchezaji ni duni sana na kwa kweli naona umuhimu Juma Mgunda kurudi kwenye benchi.

Leo Simba imeshinda lakini Yanga ndiyo wamecheza kimfumo bora zaidi.

CC

Scars
 
Simba leo katetewa na mungu tu
Cc. Bahatiyao
 
Simba amechukua UBINGWA Bila KUFUNGA goli lolote.

Nimesikitishwa sana Na uchezaji WA Simba.

Nimekuwa nikilalamika Kila siku hapa Jukwaani kwamba Simba IMESAJILI HOVYO MNO.

Kukosa Kiungo WA MAANA Katikati No 6
Kutawagharimu mno.
NGOMA ANATAKIWA atafutiwe kiungo WA kucheza nae., HUYO kanute HAMNA KITU.
 
Kwa kweli uwezo wake wa kupanga wachezaji nani acheze kwanza na nani aingie baadae ni mdogo sana.

Mifumo yake ya uchezaji ni duni sana na kwa kweli naona umuhimu Juma Mgunda kurudi kwenye benchi.

Leo Simba imeshinda lakini Yanga ndiyo wamecheza kimfumo bora zaidi.

CC

Scars
Huyu kocha hii falsafa yake imefeli,tunacheza mipira ya kubutua na siyo kumiliki na kutengeneza movement,kwa hii falsafa yake tutakuwa na draw nyingi kwenye ligi
 
Mtamlaumu bure kocha ila tatizo lipo kwa uongozi kusajili mawinga wengi wakati hawana viungo wenye uwezo. Mzamiru na Kanout hawana sifa ya kuchezea Simba, viungo hawana uwezo Wa kukaa na mpira wala kupiga pasi. Kuna mapungufu kwenye beki ya kati pia.
 
Leo tumeshinda kwa mikwaju ya penati lakini ukweli lazima usemwe, timu yetu haichezi mpira unaovutia, ni ukweli usiopingika kuwa kikosi chetu kina watu wa kazi hasa ambao wana uwezo wa kuleta mataji ya kila aina lakini mfumo anaoutumia Robertinho unaikosesha Simba mabao.

Hivi kweli Simba hii ni ya kucheza mechi 2 bila kufunga goli? Robertinho aaambiwe kama wachezaji hawana uwezo apendekeze, kwanini Kanoute apungue makali wakati tuna Abdallah Hamis?

Timu haichezi mchezo mzuri kabisa, mpira tumeelemewa na Yanga mwanzo mwisho Leo.
Kwa hiyo waliyofunga siyo magoli?Hama hiyo hoteli ya kuitwa Milembe.
 
Sio goli tu hata kuleta hatari kwenye lango la mpinzani napo changamoto.

Kwasasa watakuelewa wachache kwasababu ya Ubingwa ila toka Simba day tunalisema hili.
Mapenzi upofu!!

Ila Mgunda alikuwa Bora sana kuliko huyu. Sema wanasema Mgunda hana "international Games exposure".

Ukiona wanaanza kuongea kizungu ndiyo ujue hutakiwi au unazuia dili za watu.
 
Leo tumeshinda kwa mikwaju ya penati lakini ukweli lazima usemwe, timu yetu haichezi mpira unaovutia, ni ukweli usiopingika kuwa kikosi chetu kina watu wa kazi hasa ambao wana uwezo wa kuleta mataji ya kila aina lakini mfumo anaoutumia Robertinho unaikosesha Simba mabao.

Hivi kweli Simba hii ni ya kucheza mechi 2 bila kufunga goli? Robertinho aaambiwe kama wachezaji hawana uwezo apendekeze, kwanini Kanoute apungue makali wakati tuna Abdallah Hamis?

Timu haichezi mchezo mzuri kabisa, mpira tumeelemewa na Yanga mwanzo mwisho Leo.
Kweli KABISA
 
kocha ana tatizo kubwa la upangaji Timu ukiangalia mechi ya Leo yanga walikuwa wanajituma zaidi wakati wachezaji wengi wa Simba walikuwa wakisubiri mpira ufike mguuni.

Mpira wa Leo ulikuwa wa Kasi lakini aling'ang'ania kukaa na wachezaji wasio na Kasi kama Saidoo na Boko ambao pia umri umeenda.
 
Halafu wamechukua sinia la ubwabwa.
 
Back
Top Bottom