Tuache ushabiki na unazi, benchi la ufundi Simba lijitathmini kabla mambo hayajaribika

Tuache ushabiki na unazi, benchi la ufundi Simba lijitathmini kabla mambo hayajaribika

Sio mara zote timu mtazokutana nazo zitapoteza nafasi za kufunga kama Yanga. Yanga alifanya kila kitu hadi zinapatikana nafasi za one on one na kipa anapoteza. Ushabiki Matokeo usifanyaje ushindwe kuona mapungufu ya timu yako.
Kosa ambalo halina madhara siyo kosa.
 
Simba amechukua UBINGWA Bila KUFUNGA goli lolote.

Nimesikitishwa sana Na uchezaji WA Simba.

Nimekuwa nikilalamika Kila siku hapa Jukwaani kwamba Simba IMESAJILI HOVYO MNO.

Kukosa Kiungo WA MAANA Katikati No 6
Kutawagharimu mno.
NGOMA ANATAKIWA atafutiwe kiungo WA kucheza nae., HUYO kanute HAMNA KITU.
Kiungo pekee DM mwenye uwezo hua ni Bangala, Ndala na Aucho ndio Natuarl DM za maana kwa hapa
 
Kama huo ndio mpira mlioenda pre season Uturuki [emoji28][emoji28][emoji28] nawaambia kwenye ligi kwa yanga hii mtamlilia Sana GSM anatoa bahasha.
Hao Yanga wenyewe nao butu hawana wafungaji, labda waimorove siku za usoni kidogo.
Ingekua ile Yanga ya mzee wa kutetema hapo sawa.
 
Huwa nachukia sana Mishabiki Mipumbavu kama Wewe na wale Waliokuamini kwa hii Hoja yako ya Kipumbavu.

Yaani hujui kuwa Shindano la Timu Nne ina maana kuwa hiyo ni hatua ya Nusu Fainali?

Hivi katika hatua ya Nusu Fainali muhimu ni Timu Kufunga Goli ndani ya dakika 90 au ni Kushinda kwa namna yoyote ile na Kuingia Fainali ili ibebe Ubingwa?

Kama Hoja yako ni Kuidhihaki Simba SC kwa kuwa Bingwa kwa Mikwaju ya Penati basi idhihaki pia na Argentina ya akina Messi kuwa Bingwa wa Kombe la Dunia kwa Kuwafunga akina Mbappe na Ufaransa yake.

Ushindi wa Penati ni wa Kikanuni FIFA hivyo Kuudhihaki na Kuwadhihaki pia Wanamichezo wote ndani na nje ya Tanzania.

Namalizia kwa Kukuuliza Swali je, Simba SC leo ingefunga Goli ndani ya dakika 90 kama utakavyo kisha Yanga SC nao Wakafunga na kutulazimu kwenda katika Mikwaju ya Penati na Simba SC Kufungwa na Kuukosa huu Ubingwa ungefurahi na ungeridhika?

Kipaumbele Kikuu cha Simba SC kilikuwa ni Kumfunga Singida Big Stars FC kwa Ushindi wowote uwe wa Michezoni dakika 90 au wa Penati na kuingia katika Mikwaju ya Penati kisha tufike Fainali na tubebe Ubingwa wa Ngao ya Jamii na tubebe Ubingwa kama ambavyo tumebeba leo kwa Kuwafunga Yanga SC.
Argentina alishnda mech zote za mtoano kw penat broo??
 
Back
Top Bottom