Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Hili ni bandiko la wito wa Tuacheni Ramli Chonganishi Kuhusu Mhusika wa Shambulizi la Risasi kwa Mhe. Tundu Lissu, kupotea kwa mwana jf maarufu Ben Saanane, kupotea kwa mwanahabari Azory Gwanda, kuibuliwa kwa miili yenye majeraha kwenye viroba, au vitendo vingine vyovyote vya ukatili na umwagikaji damu kunalofanywa na watu wasiojulikana, hivyo kupelekea watu fulani fulani kuhisiwa kuhusika!, linapotokea jambo baya lolote, mtu unaruhusiwa kumhisi mtu yoyote kimawazo, ila huruhusiwi kumtaja wala kumuandika popote, huko ni kipiga ramli chonganishi. Ukimhisi mtu, usimtaje bali mfuatilie tuu nini kitamkuta, karma ndio itamshughulikia. Hivyo natoa wito wangu ni "Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. Tuiachie "Karma" Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!"
Kwanza Tuendelee Kumuombea Lissu Uponyaji wa Haraka
Nimenote katika baadhi ya mitandao ya kijamii, kumeibuka makundi ya watu kujenga nadharia mbalimbali kuhusu chanzo cha tukio hili, na hayo matukio mengine ya kupotea kwa Ben Saanane, Azori Gwanda na miili ya kwenye viroba, aliyepanga na aliyetekeleza, na wengine hadi kufikia kupiga ramli chonganishi kuwa aliyepanga mpango huo ni fulani, na kumtaji hadi majina!, mara ni fulani, mara ni fulani, alimradi kunyooshea watu vidole!, hili sio jambo jema hata kidogo!
Kwa sisi wa imani ya Kikristu, dini yetu inatufundisha, "Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!". Tena kwenye ile kesi ya mwanamke kahaba aliyeshikwa ready handed, Bwana wetu Yesu Kristo akawaambia, "Na asiye na dhambi, awe wa kwanza kutupia jiwe!", hakuna aliyethubutu!
Vivyo hivyo kwenye hili tukio la Lissu kupigwa risasi, na hayo mengine, maadam aliyelipanga ni binadamu, na watekelezaji ni wanadamu, tangu dunia hii kuumbwa, haijawa kutokea hata mara moja, uovu ukashinda wema, au uongo kuushinda ukweli, damu ya mwanadamu asiye na hatia, aliyeumbwa na Mungu, haiwezi ikamwagika bure bila kufidiwa, kila anayefanya uovu katika dunia hii, lazima atalipwa kwa uovu na malipo ni hapa hapa duniani, na kila anayetenda mema atalipwa mema.
Japo alichofanyiwa Lisu ni uovu mkubwa, mbaya na ukatili wa ajabu, na kwa hao wengine waliopotea, hakuna anayejua hatma yao ilikuwaje, you can just imagine!, lakini hakuna haja, wala sababu ya kuanza kunyoosheana vidole, tuviache vyombo husika kufanya uchunguzi na kutupatia majibu ya kina, kuhusu hao watu wasiojulikana, waliofanya ukatili huo, na endapo hivyo vyombo husika ndio wahusika na tukio hilo, bado kuna chombo kikubwa kuliko vyote kinachoitwa karma, ambacho ndicho pekee hutoa hukumu ya haki kwa kila kinachofanyika hapa duniani!
Tumuombee Lissu to get well soon, arejee nyumbani salama akiwa bukheri wa afya, tuombe muujiza wa Ben Saanae na Azori Gwanda, waibuke wakiwa hai toka huko mafichoni walikofichwa!
Mungu yupo, kama alivyokusimamia Lissu hadi sasa bado uko hai, yeye ndiye pekee kupitia karma, atawahukumu watesi wako wako na watesi wa wengine hao!
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa
Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao
Paskali

Hakuna kitu chochote ni kipya chini ya mbingu, hakuna bahati nzuri wala bahati mbaya, hakuna jambo lolote linalotokea kwa kujitokea tuu, au kwamba limetokea ghafla tuu, au kwa bahati mbaya, or just a coincident!, no way!.
Kila jambo linalotokea, linatokea kwa sababu na lilikuwa destined kutokea hivyo hivyo lilivyotokea, yaani everything is a premeditated move, caused by our actions or inactions!.
Vile vile ukikutwa na majanga yoyote na mabalaa yoyote, yapokee kwa mikono miwili, kwa hoja kuwa majanga hayo yalikuwa destined kukutokea, namna hiyo hiyo yalivyotokea, yaani premeditated moves, huku ukijihesabu sababu ya hayo majanga ni moja kati ya mambo matatu haya.
Moja: Majanga hayo ni ama ni majaribu au mitihani ya Mwenyezi Mungu kukupa mitihani ni kwa kiasi gani wewe ni mcha Mungu, hivyo kukuletea majaribu ili kujihirisha uwepo wake na uwezo wake kwa kukuwezesha kuyashinda, kama alivyowafanyia wana Israel wakiwa utumwani Misri.
Pili: Majanga mengine ni kazi ya mwovu shetani, amekuletea majanga makubwa zaidi ambayo aliyapanga ikiwemo kukuangamiza kabisa wewe, familia yako na ukoo wako wote mfutike kutoka kwenye uso wa dunia, lakini Mungu ameyazui hayo makubwa na mabaya ambayo yameelekezwa kwako, na katika vita vya kukukinga na kukuokoa, then hayo yaliyokukuta, ni kushukuru Mungu, ndio nafuu yake ukilinganisha na yale yaliyozuiliwa au kuepushwa yasikufike, kama Mungu alipomuepusha Lutu na ile Sodoma na Gomola, japo Lutu alimpoteza mkewe kwa kugeuka jiwe la chumvi, na aliwalala mabinti zake bikira,na kuwapa ujauzito, yote hayo ni madogo ukilinganisha na kilitokea Sodomana Gomora.
Tatu: Majanga hayo ni mavuno ya karma ya ulichokipanda, ni fidia ya kufidia malipo ya ulichokifanya au walichokifanya wazazi wako, hivyo una obligation ya kuepuka kufanya matendo maovu, uli usihukumiwe na kuwaachia watoto wako mizigo ya kukulipia madeni ya uovu wako wakati wewe haupo duniani!.
NB. Kitu kizuri kuhusu hii karma, ukiisha adhibiwa, au kupata mapigo ya karma, deni likiisha, au kuisha fidiwa, adhabu inamalizika, ila pia kwa kujitambua, ukifanya jambo baya, ukaomba msamaha kabla karma haijaanza kukushughulikia, then una weza ku reverse bad karma isikutokee, au hata kuizuia kabisa kwa kufanya mema mengi zaidi kuliko uovu!.
Tukipata mema na mafanikio, tuseme asante, na tukipata balaa na majanga, pia tuseme asante, kwa sababu hata kama ni majanga, majanga mengine ni blessing in disguise, kama ilivyo kwa Yesu, japo ni Yuda ndio alimsaliti Yesu, na Yesu aliteswa kwa usaliti wa Yuda, lakini kumbe tukio lote, lilikuwa pre meditated siku nyingi nyuma, litokee vivyo hivyo lilivyotokea na kuonekana kama ni janga kwa Bwana wetu Yesu Kristo kuteswa hadi kufa kwa kifo cha aibu cha kuwambwa msalabani,, kumbe kwa yote hayo yamefanyika ili Mungu aonyeshe utukufu wake kwa Yesu kuyashinda mauti, na kule kuteswa kwake was a blessing in disguise, kwa sababu ni kwa kuteswa kwake, sisi tuliponywa!.
Nawatakia Jumapili njema!.
Paskali
Kwa ufahamu zaidi kuhusu haya mambo ya powers, tembelea nyuzi hizi,
Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo Bila Kujitambua!,
"Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu ya Miujiza Ya Uponyaji kwa Imani!. Kila Mtu Anazo!.