Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani!

Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani!

Mhusika wa ufyatuaji RISASI anajulikana , siku ya tukio hakuwepo kituo chake cha kazi, baada ya tukio alikimbilia Morogoro, tunajua anavyokingiwa kifua lakini muda utaamua. Nimalize kwa kusema sina muda wa kuombea wale wanaotaka kuombewa. Nitamuombea Lissu kwa sasa apone haraka.
Naomba sana Polisi wamchukue na kumfuatilia huyu jamaa anaonekana shahidi muhimu sana katika sakata hili . Tusifanye mzaha kwenye vitu serious .
 
"An eye for an eye", or the law of retaliation, is the principle that a person who has injured another person is to be penalized to a similar degree,
 
Pascal Mayalla

Let's do some Hegelian dialectic analysis here.

Kama hutaki kuhukumu, unaelewa kwamba kuandika tuache ramli chonganishi ni kuhukumu?

Kama karma tu inatosha, kuna haja gani ya kuandika?

Ukishasema "tusihukumu, tusije tukahukumiwa" ushahukumu wanaohukumu, ushahukumu kwamba kila mtu anaogopa kuhukumiwa, ushahukumu kwamba kutokuhukumiwa ni bora kuliko kuhukumu.

Contradictions kibao.
 
Albadir ndio karma halisi,tusipende kutetea uovu kisa waliofanya uovu ni watu wetu,acha kupitia dua ya albadir,mwenyezi mungu muweza yote atoe majibu yake,albadir ndiyo jibu la maovu yote
 
mbona wananchi ndio wanaosema Magufuli ana squad ya mauaji kwa kupitia makonda hujayasikia au umeyasikia kwa mara ya kwanza mbona unajifanya husikii wala huoni wewe Paskali Mayalla unafuruhia katika nchi hii serikali kuendesha mauaji ya wale wanaowakosoa unafuruhia nchi yetu kuingia kwenye lindi la damu unafurhia watu wanauwawa damu zao zinachuruzika kwenye lindi la bahari na kuelea kufa vifo vya aibu kama wahalifu wakati tuu wametoa maoni yao wewe paskali mayalla tukutambuwe kama mmoja wa wauaji kwa nini mambo yote huwa unakemea na kusaidia kunyoosha agenda ya nchi lakini hilli la wananchi kuuwawa na watu wakubwa kutajwa kama Magufuli na Makona kutajwa hukemei au kwa sababu ni wasukuma wenzako kwa hiyo unabariki uovu huu Paskali jitahidi kukemea haya mambo ya ishe leo ameanzwa lissu kesho nitakuwa mimi mwisho utakuwa wewe mbaya sana kubariki umwagaji wa damu unaofanywa.I miss the best Paskali Iknew from the Kiti Moto show you are as well an evil this days
Mkuu Froida, posti yako hii imeniumiza, hebu soma hapo nilipo bold, kama umeelewa, kama hujaelewa, nitakufafanulia.
Wanabodi,
Kwa sisi wa imani ya Kikristu, dini yetu inatufundisha, "Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!". Tena kwenye ile kesi ya mwanamke kahaba aliyeshikwa ready handed, Bwana wetu Yesu Kristo akawaambia, "Na asiye na dhambi, awe wa kwanza kutupia jiwe!", hakuna aliyethubutu!.

Vivyo hivyo kwenye hili tukio la Lissu kupigwa risasi, maadam aliyelipanga ni binadamu, na watekelezaji ni wanadamu, tangu dunia hii kuumbwa, haijawa kutokea hata mara moja, uovu ukashinda wema, au uongo kuushinda ukweli, damu ya mwanadamu asiye na hatia, aliyeumbwa na Mungu, haiwezi ikamwagika bure, kila anayefanya uovu katika dunia hii, lazima atalipwa kwa uovu na malipo ni hapa hapa duniani, na kila anayetenda mema atalipwa mema.

Japo alichofanyiwa Lisu ni uovu mkubwa, mbaya na ukatili wa ajabu, hakuna haja wala sababu ya kuanza kunyoosheana vidole, tuviache vyombo husika kufanya uchunguzi na kutupatia majibu ya kina, kuhusu hao watu wasiojulikana, waliofanya ukatili huo, na endapo hivyo vyombo husika ndio wahusika na tukio hilo, bado kuna chombo kikubwa kuliko vyote kinachoitwa karma, ambacho ndicho pekee hutoa hukumu ya haki kwa kila kinachofanyika hapa duniani!.

Lissu Get Well Soon, Mungu yupo, kama alivyokusimamia uko hai mpaka sasa, yeye ndiye pekee kupitia karma, atawahukumu watesi wako!.

"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa ...
Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao ...
Paskali
Paskali
 
Mkuu Froida, posti yako hii imeniumiza, hebu soma hapo nilipo bold, kama umeelewa, kama hujaelewa, nitakufafanulia.

Paskali
sawa kama sikukuelewa lakini mimi nalia sana ninapoona mambo ya kuuwana yanaongezeka na hofu nchi yangu pendwa isije ikaingia kwenye vita vya wenyewe,tangu Nyerere Mwinyi Mkapa Kikwete wananchi tumekuwa tukipishana maoni lakini hakukuwa hata mara moja katika historia mtu mmoja anamiminiwa risasi 40 kwenye eneo la wazi na usalama inauma sana kwa kweli
 
Wewe unalia kwa sababu ya Lissu tuu, angalia sisi tumeanza kulia lini?.
IGP Kamanda Sirro, Usiruhusu Vifo Vya Uzembe Kama Huu Kuchafua ...
ACJ na Mhimili wa Mahakama, Kemeeni Tabia Ya Jeshi la Polisi ...
Ombi Muhimu Kwa Jeshi Letu La Polisi."Nyinyi ni Wenzetu, September ...
Mauaji ya Polisi: Gazeti la Jamhuri Laibua Chanzo Cha Ajabu ...
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ...
IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality!.
Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know!
Waziri Nchimbi na IGP Mwema, Mnasubiri Nini Kujiuzulu?
Ili Nchi iwe na amani, Simon Sirro awe Mkuu wa Jeshi la Polisi ...
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa ...
Mauaji ya Polisi Wetu ni Ujambazi au Ugaidi au Retaliation?. Nini ...
TISS ni Watekaji, Watesaji na Wauaji!. Wasijadiliwe na Bunge bali ...
Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For ...
Mhe.Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu ...
Hivi polisi wameruhusiwa kuua wakihisi fulani ni mhalifu ...
Kama haya Mauaji ni kweli, Waziri Mwigulu, na IGP Mangu Walipaswa ...
P.
 
Hoja ni nzuri na watanzania wote tunapaswa kuishi hivyo kwa kujua tunawajibu wa yote yanayotutokea.

Ila kaka baadaye umechanganyachanganya mavitu baada ya kuleta habari za majaribu ya Mungu ama Shetani.

Hoja kuu ni "law of cause and effect" hivyo hapo hakuna cha majaribu ya Mungu wala shetani.
 
Pascal Mayalla
Let's do some Hegelian dialectic analysis here.
Kama hutaki kuhukumu, unaelewa kwamba kuandika tuache ramli chonganishi ni kuhukumu?
Kama karma tu inatosha, kuna haja gani ya kuandika?
Ukishasema "tusihukumu, tusije tukahukumiwa" ushahukumu wanaohukumu, ushahukumu kwamba kila mtu anaogopa kuhukumiwa, ushahukumu kwamba kutokuhukumiwa ni bora kuliko kuhukumu.
Contradictions kibao.
Mkuu Aluwatani, kwa vile mimi sio mtaalamu wa Hegelian dialectic analysis, I can't argue much on this, ila sijahukumu popote wala hakuna hakuna contradiction yoyote, ila nakiri uwezekano wa contradictions katika uelewa!, yaani erratic perception hata kitu very straight, mtu mwenye erratic perception atakiona kimepinda kama ilivyo kwa reflection, refraction na parallax vission kwenye light.

Neno usihukumu ni ushauri, ikimaanisha ukihukumu, utahukumiwa, na huko kuhukumiwa endapo utahukumu, hautahukumiwa na mimi nilikupa angalizo la usihukumu, bali utahukumiwa na karma ya hukumu uliohukumu wewe!.

Ni kama kukuonya kuwa sumu haipimwi kwa kuilamba, ukiilamba utakufa, kisha wewe ukaijaribu kwa kuilamba!,kitakachokutokea, utasema ni mimi nimekulambisha?!.

Maadam karma ipo and is for real, hatuna haja ya kuhukumu ili tusihukumiwe, kazi ya kuhukumu, aachiwe Hakimu Mkuu, karma.

Paskali
 
PASKALI vyombo vinatuhumiwa haviwezi kutenda haki. Na kwa trend ya haya yanayofanywa na mamlaka, ni wazi kuna jambo kubwa limejificha
Mbele ya karma, hakuna kujificha, wala karma haijali nani ni nani, mbele ya karma all human beings are equal, wafalme na beggars are treated equally, hakuna uheshimiwa!.

P.
 
Mkuu Aluwatani, kwa vile mimi sio mtaalamu wa Hegelian dialectic analysis, I can't argue much on this, ila sijahukumu popote wala hakuna hakuna contradiction yoyote, ila nakiri uwezekano wa contradictions katika uelewa!, yaani erratic perception hata kitu very straight, mtu mwenye erratic perception atakiona kimepinda kama ilivyo kwa reflection, refraction na parallax vission kwenye light.

Neno usihukumu ni ushauri, ikimaanisha ukihukumu, utahukumiwa, na huko kuhukumiwa endapo utahukumu, hautahukumiwa na mimi nilikupa angalizo la usihukumu, bali utahukumiwa na karma ya hukumu uliohukumu wewe!.

Ni kama kukuonya kuwa sumu haipimwi kwa kuilamba, ukiilamba utakufa, kisha wewe ukaijaribu kwa kuilamba!,kitakachokutokea, utasema ni mimi nimekulambisha?!.

Maadam karma ipo and is for real, hatuna haja ya kuhukumu ili tusihukumiwe, kazi ya kuhukumu, aachiwe Hakimu Mkuu, karma.

Paskali
Hakuna ambaye hahukumu.

Ukisema "usihukumu" tu ushahukumu kwamba fulani kahukumu au anaweza kuhukumu.

Badala ya kujikita kwenye "usihukumu", tujikite kwenye "usihukumu vibaya".

Unapoamka asubuhi tu na kuchagua shati la bluu na kuliacha jekundu ushahukumu kwamba la bluu ni zuri zaidi kulivaa.

Kama umeoa huyo mke wako uliyenaye maana yake ushahukumu wengine hawafai ukaona yeye anafaa.

Sasa utatuambuaje tusihukumu?

Ukitaka kutohukumu hata hela za kwenye akaunti yako itabidi uzigawe. Kwa sababu ukibaki nazo wewe utakuwa umehukumu kwamba zitakufaa wewe zaidi ya wengine.

Na hata ukizigawa utakuwa umehukumu. Utakuwa umehukumu kwamba zitawafaa wengine kuliko zitakavyokufaa wewe.

Kwa hiyo hatuwezi kuepuka kuhukumu.

Tujikite kwenye kuhukumu vizuri na kwa haki.
 
Back
Top Bottom