Wanabodi,
Hili ni bandiko la wito wa Tuacheni Ramli Chonganishi Kuhusu Mhusika wa Shambulizi la Risasi kwa Mhe. Tundu Lissu: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. Tuiachie "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!.
Kwanza tuendelee kumuombea Lissu uponyaji wa haraka.
Nimenote katika baadhi ya mitandao ya kijamii, kumeibuka makundi ya watu kujenga nadharia mbalimbali kuhusu chanzo cha tukio hili, aliyepanga na aliyetekeleza, na wengine hadi kufikia kupiga ramli chonganishi kuwa aliyepanga mpango huo ni fulani, na kumtaji hadi majina!, mara ni fulani, mara ni fulani, alimradi kunyooshea watu vidole!, hili sio jambo jema hata kidogo!.
Kwa sisi wa imani ya Kikristu, dini yetu inatufundisha, "Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!". Tena kwenye ile kesi ya mwanamke kahaba aliyeshikwa ready handed, Bwana wetu Yesu Kristo akawaambia, "Na asiye na dhambi, awe wa kwanza kutupia jiwe!", hakuna aliyethubutu!.
Vivyo hivyo kwenye hili tukio la Lissu kupigwa risasi, maadam aliyelipanga ni binadamu, na watekelezaji ni wanadamu, tangu dunia hii kuumbwa, haijawa kutokea hata mara moja, uovu ukashinda wema, au uongo kuushinda ukweli, damu ya mwanadamu asiye na hatia, aliyeumbwa na Mungu, haiwezi ikamwagika bure, kila anayefanya uovu katika dunia hii, lazima atalipwa kwa uovu na malipo ni hapa hapa duniani, na kila anayetenda mema atalipwa mema.
Japo alichofanyiwa Lisu ni uovu mkubwa, mbaya na ukatili wa ajabu, hakuna haja wala sababu ya kuanza kunyoosheana vidole, tuviache vyombo husika kufanya uchunguzi na kutupatia majibu ya kina, kuhusu hao watu wasiojulikana, waliofanya ukatili huo, na endapo hivyo vyombo husika ndio wahusika na tukio hilo, bado kuna chombo kikubwa kuliko vyote kinachoitwa karma, ambacho ndicho pekee hutoa hukumu ya haki kwa kila kinachofanyika hapa duniani!.
Lissu Get Well Soon, Mungu yupo, kama alivyokusimamia uko hai mpaka sasa, yeye ndiye pekee kupitia karma, atawahukumu watesi wako!.
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa ...
Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao ...
Paskali