Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani!

Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani!

Asante kwa uzi huu... Nina swali kidogo kuhusu Karma. Tumeelezwa kuwa Karma inatabia kama ya tukio la ' what goes around comes round' ...pia tumeelezwa kuwa karma ni sawa na sheria za Newton za Every action there is equal and opposite reaction. Swali lenyewe sasa....Mkuu, Ni wakati gani tunatambua kuwa Sasa Karma 'is going around' ama 'is coming around'....Na pia ni wakati gani tunaweza kusema sasa Karma is an ACTION na siyo REACTION?
Kwa kifupi, ni wakati gani ama ni vigezo vipi tunatumia kutambua kuwa sasa Karma inaanzisha duara na ama sasa KArma inafunga duara?
===
Kwa haraka haraka ninajua kabisa umelielewa swali langu barabara. Nasubiri majibu Mkuu.
Mkuu Tujitegemee, majibu ya hili yako kwenye the main thread ya karma.
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako! - JamiiForums

P
 
View attachment 1472626
View attachment 1472650

Salaam,

Taarifa nilizozipata hivi punde toka chanzo changu kinanihabarisha kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman A. Mbowe amevamiwa na kikundi cha watu wasiojulikana akielekea nyumbani kwake usiku huu na kupigwa na wamemuumiza.

Tukio hili limetokea majira ya saa 6-7 usiku.

Mhe. Mbowe amekimbizwa Hospitali ya Ntyuka iliyopo jijini Dodoma.

Kamanda Muroto amesema wamepata taarifa kuwa kavunjwa mguu wa kulia na amelazwa Wodi namba 4 hospitalini hapo. Amesema taarifa zaidi zitafuata

MAONI YANGU:
Mhe. Mbowe kuvamiwa na kupigwa eneo la Area D, jijini Dodoma, Mtaa wa Sengia; linalotajwa kuwa na ulinzi wa kutosha, kama ilivyotokea kwa Lissu kunaacha maswali mengi, je, hili linaweza kuwa limechochewa na Lissu kutangaza nia ya kugombea Urais wa JMT October 2020? Ni hasira au kitu gani? No one knows.

Bado najiuliza; hivi kama Taifa kwa tabia hizi za kihuni tunaelekea wapi? Hawa wanaojichukulia sheria mikononi kila siku wanafanya hivyo kwa kutumwa na nani? Matendo haya yataendelea kwa viongozi wa upinzani mpaka lini?

We need to wake up, better late than never.
Duh...!.
Hii ni hatari sana!.
Hata shambulio hili la Mhe. Mbowe, limefanywa na watu wasiojulikana, hivyo nawaomba sana tusihujukumu, kwa kupiga ramli chonganishi ili na sisi tusihukumiwe!.
Pole sana Mhe. Mbowe,
Get well soon.
P
 
Ubashiri peke yake bila nyongeza yoyote ya nguvu zilizo nje ya mamlaka ya Mungu siyo ramli bali ni utabiri! Ramli ni ubashiri unaoambatana na matumizi ya nguvu nyingine za nyongeza ambazo hazitokani na mamlaka ya Mungu. Kwenye utabiri Mungu huwa anashiriki 100% ila kwenye ubashiri mchango wa Mungu ni 0%
Mwanzo wa Mungu ndio ule ule wa shetani, kabla ya kuwa ibilisi shetani, Lucifer was the 2nd in command baada ya Mungu, na hata baada ya usi alitimuliwa peponi na kutupwa Duniani with all the powers zikiwa intact.

Mungu anazungumza na watu wake kwa maono na utabiri, shetani pia does the same. The dividing line between nguvu za Mungu na nguvu za shetani ni very thin!. The only difference ni nguvu za Mungu ni unconditional, zinakuja by grace from the Lord, lakini nguvu za shetani zinaandamana na conditionalities.
P
 
Uko sahihi kabisa. Nguvu za shetani kwa kuanzia unapewa bure uzitumie kwanza, na baada ya kuzitumia ndiyo unapewa bei na masharti yake. Za Mungu ukiona unazitumia, ujue tayari ulishazilipia kwa kufanya kazi kwenye kile ki-portion kidogo mno ambacho Mungu huwa anakitoa kama assignment kwako, kabla hajakuamini na kuchukua uamuzi wa kukutunuku mamlaka hayo. However, over 99.99% ya nguvu za Mungu ambazo huwa anawatunuku wanadamu ili wazitumie, zinatokana na neema ya Mungu tu na si vinginevyo. Huwa nawashangaa mno wale ambao huwa wanapenda kujiingiza kwenye mambo ya hatari ya ku-deal na shetani!
 
Uko sahihi kabisa. Nguvu za shetani kwa kuanzia unapewa bure uzitumie kwanza, na baada ya kuzitumia ndiyo unapewa bei na masharti yake. Za Mungu ukiona unazitumia, ujue tayari ulishazilipia kwa kufanya kazi kwenye kile ki-portion kidogo mno ambacho Mungu huwa anakitoa kama assignment kwako, kabla hajakuamini na kuchukua uamuzi wa kukutunuku mamlaka hayo. However, over 99.99% ya nguvu za Mungu ambazo huwa anawatunuku wanadamu ili wazitumie, zinatokana na neema ya Mungu tu na si vinginevyo. Huwa nawashangaa mno wale ambao huwa wanapenda kujiingiza kwenye mambo ya hatari ya ku-deal na shetani!
Naunga mkono hoja
P
 
Final Update
Tundu Lissu leo amerejea nyumbani Tanzania, hivyo naomba kuthibitisha humu kuwa Tundu Lissu ni Jasiri na Shujaa Kuliko Nelson Mandela.

Hivyo sasa, kufuatia kurejea huku, ule ushauri wangu nilioutoa kwake kabla hajashambuliwa, sasa utekelezwe.

Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!

Shujaa Kamanda Tundu Lissu, karibu nyumbani.
Mungu ni mwema amekutendea muujiza, hivyo endelea kutimiza ndoto yako, Mungu aliyekuponya ni Mungu mwenye uwezo, anaweza kabisa kulifanya "Jiwe Walilolikataa Waashi, Likafanywa Jiwe Kuu la Pembeni"

I wish him all the best.
Paskali
 
Na kwa kesi kama hizi ukiwa kama wakili msomi, mawakili watakutetea bure kabisa ili wapate thawabu.
 
Mkuu Paukwa, Pakawa, with due respect, tuko wote humu jf kwa zaidi ya miaka 10!, hujazijua tuu thumbs up zangu?.
Nakuomba sana, usiwawazie wengine mabaya, ni kama kuwahukumu na kuwanyooshea vidole, ikitokea hawana huo ubaya ulioudhania, karma ya maumivu ya ubaya unaowadhania its upon you!.
Usihukumu usije ukahukumiwa!.
P
 
Wanabodi,
karma.jpg

Hili ni bandiko la wito wa Tuacheni Ramli Chonganishi Kuhusu Mhusika wa Shambulizi la Risasi kwa Mhe. Tundu Lissu, kupotea kwa mwana jf maarufu Ben Saanane, kupotea kwa mwanahabari Azory Gwanda, kuibuliwa kwa miili yenye majeraha kwenye viroba, au vitendo vingine vyovyote vya ukatili na umwagikaji damu kunalofanywa na watu wasiojulikana, hivyo kupelekea watu fulani fulani kuhisiwa kuhusika!, linapotokea jambo baya lolote, mtu unaruhusiwa kumhisi mtu yoyote kimawazo, ila huruhusiwi kumtaja wala kumuandika popote, huko ni kipiga ramli chonganishi. Ukimhisi mtu, usimtaje bali mfuatilie tuu nini kitamkuta, karma ndio itamshughulikia. Hivyo natoa wito wangu ni "Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. Tuiachie "Karma" Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!".

Kwanza Tuendelee Kumuombea Lissu Uponyaji wa Haraka.
Nimenote katika baadhi ya mitandao ya kijamii, kumeibuka makundi ya watu kujenga nadharia mbalimbali kuhusu chanzo cha tukio hili, na hayo matukio mengine ya kupotea kwa Ben Saanane, Azori Gwanda na miili ya kwenye viroba, aliyepanga na aliyetekeleza, na wengine hadi kufikia kupiga ramli chonganishi kuwa aliyepanga mpango huo ni fulani, na kumtaji hadi majina!, mara ni fulani, mara ni fulani, alimradi kunyooshea watu vidole!, hili sio jambo jema hata kidogo!.

Kwa sisi wa imani ya Kikristu, dini yetu inatufundisha, "Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!". Tena kwenye ile kesi ya mwanamke kahaba aliyeshikwa ready handed, Bwana wetu Yesu Kristo akawaambia, "Na asiye na dhambi, awe wa kwanza kutupia jiwe!", hakuna aliyethubutu!.

Vivyo hivyo kwenye hili tukio la Lissu kupigwa risasi, na hayo mengine, maadam aliyelipanga ni binadamu, na watekelezaji ni wanadamu, tangu dunia hii kuumbwa, haijawa kutokea hata mara moja, uovu ukashinda wema, au uongo kuushinda ukweli, damu ya mwanadamu asiye na hatia, aliyeumbwa na Mungu, haiwezi ikamwagika bure bila kufidiwa, kila anayefanya uovu katika dunia hii, lazima atalipwa kwa uovu na malipo ni hapa hapa duniani, na kila anayetenda mema atalipwa mema.

Japo alichofanyiwa Lisu ni uovu mkubwa, mbaya na ukatili wa ajabu, na kwa hao wengine waliopotea, hakuna anayejua hatma yao ilikuwaje, you can just imagine!, lakini hakuna haja, wala sababu ya kuanza kunyoosheana vidole, tuviache vyombo husika kufanya uchunguzi na kutupatia majibu ya kina, kuhusu hao watu wasiojulikana, waliofanya ukatili huo, na endapo hivyo vyombo husika ndio wahusika na tukio hilo, bado kuna chombo kikubwa kuliko vyote kinachoitwa karma, ambacho ndicho pekee hutoa hukumu ya haki kwa kila kinachofanyika hapa duniani!.

Tumuombee Lissu to Get Well Soon, arejee nyumbani salama akiwa bukheri wa afya, tuombe muujiza wa Ben Saanae na Azori Gwanda, waibuke wakiwa hai toka huko mafichoni walikofichwa!.
Mungu yupo, kama alivyokusimamia Lissu hadi sasa bado uko hai, yeye ndiye pekee kupitia karma, atawahukumu watesi wako wako na watesi wa wengine hao!.

"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa ...

Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao ...


Paskali
P
 
Back
Top Bottom