Wanabodi,
Hili ni bandiko la wito wa Tuacheni Ramli Chonganishi Kuhusu Mhusika wa Shambulizi la Risasi kwa Mhe. Tundu Lissu, kupotea kwa mwana jf maarufu Ben Saanane, kupotea kwa mwanahabari Azory Gwanda, kuibuliwa kwa miili yenye majeraha kwenye viroba, au vitendo vingine vyovyote vya ukatili na umwagikaji damu kunalofanywa na watu wasiojulikana, hivyo kupelekea watu fulani fulani kuhisiwa kuhusika!, linapotokea jambo baya lolote, mtu unaruhusiwa kumhisi mtu yoyote kimawazo, ila huruhusiwi kumtaja wala kumuandika popote, huko ni kipiga ramli chonganishi. Ukimhisi mtu, usimtaje bali mfuatilie tuu nini kitamkuta, karma ndio itamshughulikia. Hivyo natoa wito wangu ni "Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. Tuiachie "Karma" Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!"
Kwanza Tuendelee Kumuombea Lissu Uponyaji wa Haraka
Nimenote katika baadhi ya mitandao ya kijamii, kumeibuka makundi ya watu kujenga nadharia mbalimbali kuhusu chanzo cha tukio hili, na hayo matukio mengine ya kupotea kwa Ben Saanane, Azori Gwanda na miili ya kwenye viroba, aliyepanga na aliyetekeleza, na wengine hadi kufikia kupiga ramli chonganishi kuwa aliyepanga mpango huo ni fulani, na kumtaji hadi majina!, mara ni fulani, mara ni fulani, alimradi kunyooshea watu vidole!, hili sio jambo jema hata kidogo!
Kwa sisi wa imani ya Kikristu, dini yetu inatufundisha, "Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!". Tena kwenye ile kesi ya mwanamke kahaba aliyeshikwa ready handed, Bwana wetu Yesu Kristo akawaambia, "Na asiye na dhambi, awe wa kwanza kutupia jiwe!", hakuna aliyethubutu!
Vivyo hivyo kwenye hili tukio la Lissu kupigwa risasi, na hayo mengine, maadam aliyelipanga ni binadamu, na watekelezaji ni wanadamu, tangu dunia hii kuumbwa, haijawa kutokea hata mara moja, uovu ukashinda wema, au uongo kuushinda ukweli, damu ya mwanadamu asiye na hatia, aliyeumbwa na Mungu, haiwezi ikamwagika bure bila kufidiwa, kila anayefanya uovu katika dunia hii, lazima atalipwa kwa uovu na malipo ni hapa hapa duniani, na kila anayetenda mema atalipwa mema.
Japo alichofanyiwa Lisu ni uovu mkubwa, mbaya na ukatili wa ajabu, na kwa hao wengine waliopotea, hakuna anayejua hatma yao ilikuwaje, you can just imagine!, lakini hakuna haja, wala sababu ya kuanza kunyoosheana vidole, tuviache vyombo husika kufanya uchunguzi na kutupatia majibu ya kina, kuhusu hao watu wasiojulikana, waliofanya ukatili huo, na endapo hivyo vyombo husika ndio wahusika na tukio hilo, bado kuna chombo kikubwa kuliko vyote kinachoitwa karma, ambacho ndicho pekee hutoa hukumu ya haki kwa kila kinachofanyika hapa duniani!
Tumuombee Lissu to get well soon, arejee nyumbani salama akiwa bukheri wa afya, tuombe muujiza wa Ben Saanae na Azori Gwanda, waibuke wakiwa hai toka huko mafichoni walikofichwa!
Mungu yupo, kama alivyokusimamia Lissu hadi sasa bado uko hai, yeye ndiye pekee kupitia karma, atawahukumu watesi wako wako na watesi wa wengine hao!
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa
Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao
Paskali