Tuacheni ujinga, unafiki na mihemko. Afande Sele aachwe asisumbuliwe kabisa

Kuna clip inaonuesha Sheikh anaomba Sele afe ndani ya siku saba, nimemshangaa sana......sijawahi ona wala kusikia dini inaombea mtu afe hata kama ametenda dhambi gani......
Hebu fikiria huyo Sheikh ndio afe hapo cheo cha ushekhe tutampa Sheikh Afande Sele
 
Unataka mpaka umuone kwa macho yako?
Kwa nini unafikiri hivyo? Kipi kimekufanya uamini hilo mpaka kuuliza swali hili?

Unajua kusoma kwa ufahamu na kufuatilia mantiki?

Mtu anayebishia uwepo wa Mungu kwa kuangalia mantiki na proof by contradiction kwa nini unafikiri anahitaji kumuona Mungu?

Una uwezo wa kufuatilia mantiki?

Kwani nikisema kimantiki ya hesabu square root ya mbili haiwezi kuwa kubwa zaidi ya mbili, ni lazima niione hiyo square root ya mbili?

Unajua kusoma kwa ufahamu?
 
Afande kaomba msamaha na kawaambia mashehe nao waombe msamaha kwa sababu wanampangia Mungu kazi.
Mungu hapangiwi cha kufanya.
Mashehe kwa nini wanataka yeye afe ili awaache watoto wake yatima?
 
Na wengi wanaoshupalia Afande Sele akamatwe wengi wao walikuwa wanakufuru kwa kusifu na kuabudu mtu asiyekuwa Mungu
 
Hata nikiunganishwa, hilo halitathibitisha Mungu yupo.

Thibitisha Mungu yupo.
Wew jamaa kazi zake huzioni kama bahari,mito watu aina tofauti mazao wanyama majira mbona vitu ni vingi tu kaumba vinaonekana...
 
Wew jamaa kazi zake huzioni kama bahari,mito watu aina tofauti mazao wanyama majira mbona vitu ni vingi tu kaumba vinaonekana...
Unajuaje hivyo vyote ni kazi za Mungu kweli na habari kwamba ni kazi zake si hadithi za kutungwa na watu tu?
 
Kwanza Kwa nini anaitwa Afande wakati siyo askari? Tukomalie hapo kwanza, hayo ya Mungu mtaendelea wenyewe
 
Kosa la Afande Sele ni kutumia lugha ya matusi na kurusha mitandano basi.

Kila mtu ana uhuru wa kuabudu anachopenda, kama Sele haamini uwepo wa mungu hilo ni swala lake binafsi asiingiliwe.

Kama, kwa hakika, Mungu yupo basi atamuwajibisha mwenyewe badala ya kusaidiwa na wanadamu.

TZ ina atheists (wasio amini uwepo wa mungu) kibao ila wanaogopa kujitokeza sababu ya kushambuliwa na watu badala ya mungu mwenyewe.
 
Nina imani kuwa, Sele angemtukana yule MTUME "M", waalaaaaa jamaa wasingesubiri… eti mpaka Mwenyezi Mungu amuadhibu! Wangeshamuadhibu! Jamaa hawana utani kwa MTUME wao!
Hawana akili kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…