Katiba Inayopendekezwa inataja kipengele cha kuwajali Wasanii katika Ibara ya 59, ambapo haki hizi muhimu kwa wasanii zinajumuisha Haki-miliki ambazo zitawasaidia kulinda kazi zao za ubunifu, utafiti na hatimaye kukuza sanaa, taaluma, ubunifu na ugunduzi kwa manufaa yao binafsi na taifa kwa jumla. Ifahamike kuwa, kundi hili ni muhimu katika kukuza fursa za ajira kwa vijana na kuiletea sifa na heshima nchi yetu kwa kutumia sanaa na ubunifu wao, hivyo ni kundi ambalo lina uwezo mkubwa wa kuitangaza nchi ya Tanzania katika Nyanja mbalimbali zikiwemo za kiuchumi, kiutamaduni na kijamii.
Kwa kipindi kirefu kumekuwa na kilio kikubwa kwa kundi hili kukosa ulinzi wa kazi zao, hivyo Katiba Inayopendekezwa inajenga mazingira mazuri ya kundi hili kuthaminiwa, kuendelezwa na kulindwa. Katiba Inayopendekezwa, imeweza kuonyesha ni kwa jinsi gani hakimiliki ya msanii (Intellectual property) itakavyolindwa na Katiba, jambo ambalo litasaidia kwa kiwango kikubwa kuinua maisha wa wasanii wengi nchini na kukuza vipato vyao. Kwa mujibu wa takwimu za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Wasanii wanafikia karibu milioni Sita kati ya Watanzania milioni 45, kwa vyovyote kutambuliwa huku kutawasaidia wasanii.
Wasanii wengi nchini wameonekana kuridhishwa na kitendo cha haki zao kuingizwa kwenye Katiba Inayopendekezwa kwasababu hali hiyo itawasaidia kupambana na watu wanaoiba kazi zao. Ni wazi kuwa kutambuliwa huku kutasaidia nchi kunufaika kutokana na mchango wa sekta hiyo ya sanaa na umma utafaidika kwa kiasi kikubwa. :rain: