Tuambie kama ungeweza kuzirudisha siku nyuma, ungetamani urudi kipindi kipi na ungelifanya nini?

Tuambie kama ungeweza kuzirudisha siku nyuma, ungetamani urudi kipindi kipi na ungelifanya nini?

Nataman irudi mwaka 2009 nilipoiacha scholarship yangu ya kwenda nje kuongeza Elimu kwa sababu ya mapenzi,
 
May 2012 matokeo yangu ya form six yalipotoka nimepata div 1 ya 9 i would have made better choices
 
2008 nilivyochukua mkopo wa pesa na kuchanga na mpenzi wangu ili tufanye biashara...


Baada ya miez miwili akakata mawasiliano na mimi.. Nilihangaika sana kurejesha lile deni..

Mungu mkubwa nilimaliza cha ajabu jamaa hakufanya kitu cha maana zaid ya kuhonga hawara zake... Duuuu kweli mwanaume sio ndugu yako..
Dah pole sana, ila usichukulie wote wapo hivo
 
Natamani muda urudi nyuma nione zile nyimbo za ccm zilivyo kuwa zinaimbwa kwa mbwembwee! !!
 
...Natamani kingerudi kile kipindi nilichokua na baba na mama wakiniambia fanya hichi, na mimi nafanya kile kwakuona kuwa mimi ni bora kuliko wao, kwakweli ningewasikiliza kila lililo jema kwao na kulitekeleza bila kuhoji,...!

Na wewe je... ? Maana wanasema majuto ni mjukuu!.


Duh! Watu mna Moyo, maisha haya ni ya kuombea kurudia kuishi? Mimi hata nusu Sekunde sirudishi nyuma, nikiondoka nimeondoka inatosha, hapa Duniani siyo kabisa!
 
Back
Top Bottom