Tuambie kitu cha utundu sana ulichofanya utotoni na hutakisahau maisha yako yote

Tuambie kitu cha utundu sana ulichofanya utotoni na hutakisahau maisha yako yote

Nakumbuka nipo sekondari ilikua kila jumanne tuna siku ya club..siku hiyo katika group letu hakuna alietaka kushiriki tukaamua kutoroka .kufika getini mlinzi huyo kavimba hataki kuturuhusu alafu ni mbabu bongeee..tukaanza kukimbizana pale getini Mimi ndio kiongozi hapo..tukamuangusha yule Babu alafu alikua mgonjwa wa miguu jamani...sisi hao tukafungua geti ile tunatoka tu kuna ticha mnoko akatuona..si akaanza kutukimbiza bana...ile siku sihisahau tulikua tunavuka barabara kama wehu..tukicheki nyuma Mwalimu huyo anatukimbiza ..tukaamua kugawanyika hapo kila mtu akamatwe kivyake..Mimi nilikimbilia njia ya msimbazi tukaja kutana Kariakoo kila mtu hoi.
 
Dah...kitambo... nikiwa na best yangu M ambaye sasa ni mchungaji...tulichoma malori mawili ya jeshi wakati tunajaribu "molotov cocktail" yetu...ilikuwa taabu sana[emoji41]
 
Tulikuwa tuna sehemu yetu ya kucheze bens yaan maharage yaliyo banguliwa vipande vinne, sasa kulikuwa jamaa mbabe sana hapo palikuwa na shina LA mti ilio katwa ndio kili kuwa kiti chake , cku moja nikachukua miida nika izamisha kwenye lile shina jamaa alipo kuja kwa kujiamin akalia like shina kilicho mpata anasimulia mpaka Leo, kwa maana alishindwa kumalizia kukaa wala kurudi juuu
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Aisee ungeua mtuu
Yea...nilisikia kwa watu..siku kaka alivyonikera huku anaongea nikamfunikia akaanza kusaga miguu
 
Mi nlikua bingwa wa manati, masaa yote ipo kiunoni kama bastola, nlikua mpaka nalala nayo usiku.. nshapiga sana watu za vichwa, ila kuna siku nlimpiga jamaa muuza nyanya, alinikimbiza akanipa bonge la banzi(kibao) halafu akanimalizia na konzi zito kweli, kwanza nlizunguka kama mara saba pale pale kabla ya kukimbia.... Sintosahau

😆😆😆😆😆😄 🙌🙌🙌
 
Mimi mchezo wa kombolela ndio ulikuwa wangu[emoji3]kuanzia saa 12 na nusu jion kale kagiza giza ka kuingia magharibi ndio tunaanza kucheza[emoji3]
Dadeki tunaenda sehem kama kujibanza ivi nipo mimi na kidada cha mtaani kwetu,,hapo hapo tunaanza kudandiana eti huku unalia kwa raaha,aassh aasshh aasssh,!!![emoji3][emoji3]fasta tu kama kuku vile tushamaliza,tunaendelea na kombolela[emoji3]
 
1. Wakati nipo darasa la 7, nilishawishi wanafunzi wote wa kiume darasani tusije kwenye kipindi cha jioni ili tukacheze mpira na shule ya jirani bila ruhusa wala taarifa ya shule, ticha kaja jioni kakuta wasichana tu kuuliza anaambiwa tumeenda kucheza game, kesho yake staff nzima ilihamia darasani, tulichezea fimbo zisizo na idadi, kesho yake tukamvizia ticha usiku tukamtoa ngeu, wakaitwa wazazi wakayamaliza kiutu uzima na headmaster tukamaliza shule.
2. Niliwahi kuwa nampenda mtoto wa mkuu wa wilaya tukiwa darasa la 3, ilikua dawati langu nyuma lake mbele, nikikaa pembeni naye atakaa pembeni , nikikaa katikati naye hivyo hivyo, ilikua lazima tukae sambamba, sasa kuna mtoto mmoja wa tajiri alianza kumshobokea mtoto, kwa sababu alikua na ushawishi, wapambe wake wakawa wanabadilisha dawati letu linapelekwa nyuma afu la kwao wanaweka nyuma ya dawati la yule mtoto wa mkuu wa wilaya, nikaona isiwe kesi baada ya week nikajichanga visent, nikaenda kununua mnyororo na kufuli, Jumatatu nikaja shule saa 12 kasoro nikachukua dawati letu na la demu nikalitia mnyororo na lock ya kufuri kisha nikaenda kutupa funguo jalalani ili kupoteza ushahidi, masela walinimind kinoma ila niliwakomesha. Kinachoniuma nikikumbukaga huu ujinga ni kwamba sa hivi huyo demu sijui hata yuko wapi.
 
Iyo ya darasa la tatu mkuu ni chai yani chaii
 
Iyo ya darasa la tatu mkuu ni chai yani chaii
Chai iko wapi hapo? unafikiri sisi tumesoma enzi za hizi za school bus?, shule za serikali zamani tulikua tunasoma na watoto wote wa viongozi, na tulikua tunakalia madawati ya watu watatu kila dawati.
 
Back
Top Bottom