Beeb
JF-Expert Member
- Aug 18, 2018
- 29,394
- 59,069
Nakumbuka nipo sekondari ilikua kila jumanne tuna siku ya club..siku hiyo katika group letu hakuna alietaka kushiriki tukaamua kutoroka .kufika getini mlinzi huyo kavimba hataki kuturuhusu alafu ni mbabu bongeee..tukaanza kukimbizana pale getini Mimi ndio kiongozi hapo..tukamuangusha yule Babu alafu alikua mgonjwa wa miguu jamani...sisi hao tukafungua geti ile tunatoka tu kuna ticha mnoko akatuona..si akaanza kutukimbiza bana...ile siku sihisahau tulikua tunavuka barabara kama wehu..tukicheki nyuma Mwalimu huyo anatukimbiza ..tukaamua kugawanyika hapo kila mtu akamatwe kivyake..Mimi nilikimbilia njia ya msimbazi tukaja kutana Kariakoo kila mtu hoi.