Tuambie kitu cha utundu sana ulichofanya utotoni na hutakisahau maisha yako yote

Bwawa la Bonyea Bonyea kijijini kwetu.

Enzi hizo kijijini, tulikuwa group la watoto kama 20 hivi wa age 8-9; kulikuwa na bwana kubwa nje ya kijiji lililoota nyasi za ukoka kwa juu, sasa tunachofanya tunapanga line moja tunashikana viunoni kisha tunaanza kuvuka with condition hakuna kumwachia mwenzako kabisa.

Tunaanza kuvuka hilo bwawa tukipita kwa juu, zile nyasi za ukoka zinabonyea bonyea bonyea kama mawimbi vile sasa hiyo ndiyo starehe yetu - sasa kama mmoja wetu akitaka kutumbukia ndani ni lazima tumvute, style yetu ilikuwa tunajitupa ubavu wote then tunamvuta miguu tunamtoa - tunachekaa kisha tunaendelea tena na mchezo wetu wa bonyea bonyea.

Bwawa lilikuwa refu sana na kama ukitumbukia basi wewe ni marehemu; huu mchezo ulikuwa hatari sana na wazazi wetu wote hawakujua, tulikwenda kwa siri.

Huwa nikikumbuka huu mchezo nasema Mungu ana ulinzi mkubwa mno hasa kwa watoto.
 
uporaji (nikiwa mwanafunzi) pale mitaa ya upanga adi kariakoo..... kumpora Freaky Tah wa Lost Boys pale Diamond Dubilee hall jewellery (mkufu 1 na vito 2),
 
Nilikuwa na tabia 'mbaya' pindi nikitoka tu shule mchana, naishia sebuleni natupa begi langu then badala ya kukagua ma-hot pot mimi naenda jikoni moja kwa moja, naigusa plate ya jiko la umeme ( kama ni mkaa basi nadumbukiza mkono kwenye sufuria ya majivu ya kuhifadhia moto).
Nikihisi ujoto joto kwa mbaaaali basi najua chakula kipo so naenda chumbani kula (chakula tulikua tunawekewa chumbani moja kwa moja) na nikihisi ubaridi basi najua chakula hamna ko nafanya maarifa ya kumenya viazi mapemaa kabla ya kuingia room.

Sasa kuna siku nimerudi tu nyumbani kama kawaida nikafanya 'kamchezo kangu', mama weeeee kumbe jiko limetokwa kuzimwa muda si mrefu, kiganja chote kiliungua kikawa flat, prints zote za kwenye viganja zilifutika kikawa kama kichwa cha 'mjusi kafiri'. Daaaah, sijui nilikuwa nawaza nini mjinga mimi
 
1
nakumbuka niliwahi mkata jembe la utosi damu iliruka nikakimbia sehemu ambayo nilipotea nikaa siku tatu nyumba ya wasamaria.
2 siku wamekuja mademu zetu nashkaji wangu alikuwa na ghetto tukaiba dume la bata na kulitengeneza supu mwenye nalo analitafuta kesho yake tukala na mademu zetu
 
Haki nimecheka sana eti mjusi kafiri
 
Nakumbuka kuku wa jirani aliingia uani na vifaranga
Tukawapiga na mmoja akavunjika mguu hapo ndio mimi na mdogo wangu tukawa madokta wa dharura
Tukachukua mijiti 2 na uzi na kuanza kumfunga yule kifaranga
Kwa kweli tangu umri huo nikawa mkarimu sana kwa viumbe wote mpaka sasa

Kwa kweli siwezi kusahau
 
Aisee nimecheka sana[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
nilikuwa napita sana madirishani kama tumefungia ufunguo ndani(madirisha yenye nondo) siku moja wakati naingia kichwa kilipita vizuri sehemu ya mwili iliyobaki iligoma ikabidi niwaze kutoka kwanza, wakati nataka kutoa kichwa nacho kikagoma kutoka nilihangaika siku hiyo mpaka baba alipokuja akatoa msaada kipindi hicho masikio yalishachemka kama tecno ukiitumia kwenye chaji😀
 
Nakumbuka tulikuwa tunaishi maeneo ya Soweto uwanja wa ndege Moshi,so siku moja jion katika harakati za michezo nikampiga ngwara rafiki yangu huku na huku si akavunjika mkono,nakumbuka baada mshikaji kuwekewa p.o.p dada zake waliwaka na mm,kwani nilikuwa natoka nje?....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…