Tuambie sababu iliyokupelekea ukawa unatumia hiyo ID yako hapa JF

Tuambie sababu iliyokupelekea ukawa unatumia hiyo ID yako hapa JF

Diazepam ni dawa inayotumika kumtuliza mtu na akalala(valium). Siku nafungua hii ID nilikuwa nimempa mgonjwa hii dawa alikuwa na kelele na fujo kibao ila baada ya kupata diazepam akalala chap no kelele

so nikasema mimi ntakuwa mtuliza ghasia ndio nkajiita diazepam. Kuhusu hiyo avatar zile meme zilikuwa zinafurahisha sana wakati jamaa ametrend.
 
kuna Mkuu mmoja atapita hapa mda sio mrefu..anajiita cocastic ila mimi najua kwanini anajiita hivyo..najua hatatoboa hiyo siri ila ngoja niwaibie siri yake.

siku moja miaka mingi kidogo imepita mimi nayeye tukiwa wanafunzi kutoka shule mbili tofauti mkoani Dsm tulikutana sehemu kwa mdahalo maalumu wa wanafunzi. Wakati namalizia mchango wangu kwenye lule mdahalo, nilimalizia kwa maneno haya 'thank you so much organizers for the fantastic debate'.... Sasa ilipofika zamu ya huyu mkuu nae ikabidi apige chabo kidogo akasema 'I feel so lucky to participate in this cocastic debate'...Ukumbi mzima ulivunjika mbavu.

Basi ameona ndio iwe ID yake hiyo..​
Bwana maneno mengi unataka kumla huyo G huna lolote.
 
Niliandika majina mengiiiii
Naona yote wameshawahi

Niliandika hadi neno Antarctica nakuta watu wamewahi hilo jina


Nikafikiriaaa weee
Anyway enzi hizo lil pump ndo alitoaga huo utopolo wa gucci gang
Kwa hasira nikaandika gucci gang alafu nikasend nikijua itarudi kwamba limeshatumika....
Ndo mpaka leo mimi naitwa gucci gang
Sio kwamba nalipenda jina
Ila ni bahati mbaya tu
Na frastueshen zangu😂😂
 
Niliandika majina mengiiiii
Naona yote wameshawahi

Niliandika hadi neno Antarctica nakuta watu wamewahi hilo jina


Nikafikiriaaa weee
Anyway enzi hizo lil pump ndo alitoaga huo utopolo wa gucci gang
Kwa hasira nikaandika gucci gang alafu nikasend nikijua itarudi kwamba limeshatumika....
Ndo mpaka leo mimi naitwa gucci gang
Sio kwamba nalipenda jina
Ila ni bahati mbaya tu
Na frastueshen zangu😂😂
Siubadiri jina limekaa kifamba sana mpaka Avatar ya kikolo
 
Hili jina Chakorii nililipata kutoka kwenye movie ya kihindi inayoitwa Udaan kama sijakosea.

Main character aliitwa Chakor..ila mimi niliongeza ii mbele kwa kuwa watu wa kanda ya kaskazini hupenda kuongeza herufi kwa mbele.

mfano:
pita-pitaa
Vero-veroo
Rama-ramaa

Yani hivyo tu
Inaonekana unapenda movie za kihindi Hata hivyo umepatia mulemule .. For more information

Chakori is a Girl/Female baby name and origin is Arabic, Assamese, Gujarati, Hindu, Indian, Kannada, Malayalam, Marathi, Muslim, Oriya, Sanskrit, Sikh, Sindhi, Tamil, Telugu.
 
Kunguru

Sababu ya ,wizi ukabaji,ujanja kwa sana , uwongo, kutumia bangi enzi za foolish age si unajua kunguru ni ndege wa hovyo ila wajanja ukimbiza mbawa zao


Manzese

Location nitokayo mimi ni mtoto wa Manzese hardcore uniambii kitu unionei hovyo kwenye mwili sikosi mialama ya ugomvi


Hivyo unapata kunguru wa Manzese na ndo kwenye attendance sign sheet chuo nilikua naliandika halafu katika huko naandika langu halisi

Lecture anauliza huyu ni nani hajui hio prank nilikua naipenda sana
 
Shabiki,
Nilikuwa natembelea forum bila kuregister kwa miaka 2 ,
Kisha Nikavutiwa na mijadala,
Halafu kukawa na kamjuano ka watu wa MMU na Chitchat (Hii ni miaka ya 2012), wale watu wanacoment kwa kujuana, ukizamia post na yako wataipita kama hawaioni. Mpaka uwe maarufu. Ndio chanzo ya kuanzishwa makapuku forum baadae.

Nikaona sio lazima wote tucheze. Wengine tunaweza baki kuwa mashabiki tu. (Hata guru la falsafa Afande sele alishalisema hivyo kwenye mtazamo.
 
Inaonekana unapenda movie za kihindi Hata hivyo umepatia mulemule .. For more information

Chakori is a Girl/Female baby name and origin is Arabic, Assamese, Gujarati, Hindu, Indian, Kannada, Malayalam, Marathi, Muslim, Oriya, Sanskrit, Sikh, Sindhi, Tamil, Telugu.
Si muangaliaji wa movie za kihindi.hiyo niliiangalia kwa kuwa sikuwa na cha kufanya na mkononi ninakisimu cha tochi.

Mwanzo niliipenda mno lakini sikufanikiwa kuimaliza.ni ndefuuu
 
Back
Top Bottom