A
Anonymous
Guest
Kilio kifike kwa Serikali, kuna changamoto kubwa ya uhamisho wa sisi Watumishi katika sekta ya Ualimu, hasa tunaofanya mchakato wa kuhama ili kuwafuata wenza wetu, wapo pia wanaoomba uhamisho kwa sababu nyingine tofauti.
Tunaelekezwa kuwa tutumie mfumo wa ESS, wengi wetu tumezingatia hilo lakini kinachotokea ni kuwa kwenye mfumo maombi yetu au ‘status’ zinaonesha yako TAMISEMI lakini kimyaaa hakuna kinachoendelea.
Tumesubiri takribani mwaka mzima kimya, hakuna majibu, yaani ni kama vile tuliambiwa tutumie mfumo huo ili tuwapunguzie usumbufu wa kuwauliza wahusika na wao wasingizie kila kitu kinafanyika online.
Pia soma ~ Tangu Mwaka 2017 naishi Mkoa tofauti na mke wangu sababu ya kukosa uhamisho kazini, ndoa yangu ipo shakani
Tukipiga simu kutaka kupata majibu tunaambiwa subirini mpaka Katibu Mkuu apitishe lakini ni mwaka sasa hatusaidiwi, ukienda Ofisi za Makao Makuu kuulizia wanakujibu hovyo na kukukatisha tamaa, wakati mwingine wanakufukuza.
Please Serikali itusaidie kama wahusika wanahitaji tuwalipe waseme ni sh ngapi ili tuhamishwe, maana kinachouma zaidi ni kuwa Watu wenye ndugu zao tunapata taarifa wanawalipa hao wakubwa halafu wanahamishwa. 😭😭😭😭
Pia soma:
~ Bila rushwa wala konenisheni sahau kuhusu uhamisho mfumo ni kiini macho
~ Mfumo wa uhamisho kwa watumishi mwaka 2023 umekuwa kero kubwa