Hiyo ni kwa mujibu wa tasnifu ya kiwanuka si Mimi, hembu rejea tena uthibitishe. Na lengo langu katika hilo ni kuonesha kuwa wapo watuwanaounga mkono matukio kama haya.
Na ndio maana katika moja ya posts zangu hapo juu nikasema kuielewa historia ya Zanzibar (in fact ya Tanzania kwa ujumla) ni lazima mtu atumie multiple sources kwa sababu imejaa biases nyingi sana!!
Mfano mzuri, hadi kesho Wanazi wa CCM kutoka ASP bado wanamuita SAS kama Mwarabu kwa sababu alikuwa ZNP! Wakati huo huo wanasahau au hawataki kuisema kweli kwamba SAS huyo huyo pamoja na kuwa ZNP ("Chama Waarabu"/Hizbu), ni yeye na wenzake "Waarabu" walijitoa ZNP na kuunda Umma Party kwa ajili ya kupambana na serikali iliyokuwa chini ya Sultan!!
Ni "Waarabu" hao hao kutoka kundi la SAS/Umma ndio miongoni mwao walienda Cuba kuchukua mafunzo ya kijeshi ili kuja kupambana na serikali ya Sultan:-
Na wala hawataki kusema jinsi mmoja wa hao "Waarabu" anayeenda kwa jina la Abdulrahman Babu jinsi ambavyo ofisi yake ilivamiwa na polisi wa Sultan na kisha Babu kutupwa jela baada ya kukutwa documents zilizo-highlight namna ya kufanya mapinduzi ya Serikali ya Shamte iliyokuwa chini ya Sultan!!
Hawa akina Hanga na akina Babu, mwanzoni ingawaje walikuwa vyama tofauti (Babu na wenzake Umma Party, Hanga na wenzake ASP) lakini wote walikuwa na nia moja ya kuondoa kwa nguvu Utawala wa Kisultani!!
Ukweli ni kwamba, Mzee Karume alikuwa anawaogopa sana Wasomi wa ASP na wale waliokuwa Umma Party na ndio maana mwanzoni kabisa mwa utawala wake, karibu wote aliwaweka mbali na SMZ kama vile wengine kuwapeleka ubalozi kama vile akina SAS na Omari Sharrif, na wengine kuwapeleka Bara kwenye Serikali ya Muungano kama ilivyokuwa kwa Babu na Hanga!
Kwa upande mwingine, mtu kama Babu alikuwa haaminiki hata na Nyerere na bila shaka kutokana na misimamo yake ya kimapinduzi/kikomunist!
Ukaribu wa Hanga na Oscar Kambona na wenyewe ulishakuwa red alert kwa Mwalimu hasa baada ya Kambona kuanza kupinga sera za Mwalimu na hatimae kukimbilia UK!
Kwahiyo madai kwamba ilikuwa ni kwa ajili ya usalama wa taifa ni porojo tu za Team Karume!!!