Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Katibu Mkuu wa CCM leo tarehe 13 Septemba 2024 aliitisha kukao cha dharura na waandishi (selected) wa habari kuelezea msimamo wa CCM kuelekea maandamano ya amani ya Wananchi kupitia CHADEMA.
Amekutaka chama cha CHADEMA kusitisha maandamano iliyoyaitisha. Pia ikiwataka vyama vikae mezani kuendeleza mazungumzo ya maridhiano. Pia amesisitiza kuwa vyombo vya haki kutenda haki na kutopendelea upande wowote.
Ninawaomba wanajukwaa tuchambue msimamo wa CCM kwa maeneo haya.

- Je ilibidi kitokee kifo cha cha namna ya marehemu Kibao ili CCM ijitokeze kukemea? Tangu miaka 3 nyuma watu wanatekwa huku kila dalili inaonesha vyombo vya dola vinahusika lakini wenye dhamana hawakuchukua hatua
- Nape na DC wa Longido wamekiri uhusika wa CCM kunajisi demokrasia na usalama wa taifa kupitia kauli zao. Inakuwaje CCM inawastaafisha bila hatua stahiki kuchukuliwa?
- Mazungumzo ya maridhiano baina ya vyama yana nafasi gani kwetu wananchi tusioamini hivyo vyama?
- Kwa nini leo Nchimbi anaonesha hofu ya waziwazi na asitoe msimamo wa kuungamkono maandamano ya amani ya kukomesha mauaji yanayosababishwa na polisi, TISS, UVCCM?
- Nchimbi hajazungumzia uwajibikaji wa wahusika hususan Masauni, IGP, DGIS na DCI? Najua hawezi kuzungumzia SAMIA MUST GO maana ni mfupa mgumu kwake
- Sheria ya TISS iliyorekebishwa Bungeni 2025l4 imechangia pakubwa haya mauaji. Alikwepaje hii kasoro kubwa inayolalamikiwa nchi nzima?