mwanyaluke
JF-Expert Member
- Jan 22, 2015
- 904
- 2,987
Nipo mikoa yanda za juu kusini, nafanya study ya bei ya vyakula kwa mwaka huu nikilinganisha na bei ya vyakula mashambani kwa mwaka jana , bei zinanitisha sana , mfano kwa mkoa wa mbeya, sehemu inayolima mahindi mwaka Jana bei ilikuwa 6000, mwaka huu ni 12 to 16000 , songwe - mbozi mwaka Jana mahindi yalikuwa 3000, mwaka huu 9000, bei ya mchele mwaka Jana 30000, saizi 4000 kwa debe , being ya nyama ilikuwa elfu tano kwa maeneo mengi , saizi 7000, bei ya ndizi mkungu 2000,3000, saizi elfu nane kwenda juu, kinachonitisha zaidi kipindi ndicho kipindi cha mavuno, na kawaida kwa mikoa yetu hii ukitoa ndizi , na viazi hakuna zao lingine lonalovyunwa kuanzia mwezi wa nane, je huko tuandako bei itashuka au itapanda, je mzunguko wa fedha utaongezeka au utabaki hivi, naona hatari ya tuliowengi badala ya kutafta fedha ya maendeleo tutakuwa tunpigania chakula