UTANGULIZI
Inatazamiwa kuwa zaidi ya asilimia 75% ya jamii iliyopo kusini mwa jangwa la sahara ni vijana,ikiwa nusu ya hii asilimia 75% wana umri chini ya miaka 25 na hali ya elimu katika nchi hizi zilizopo kusini mwa jangwa la sahara imezidi kuongezeka siku hadi siku.Mfano Nchi ya Tanzania inatoa wahitimu wa vyuo vikuu Zaidi ya 50,000 kila mwaka kutokana na taarifa ya jarida la vitalstats la TCU ambalo utolewa kila mwaka.
Ongezeko hili la wahitimu(jambo zuri sana kwa mstakabari wa maendeleo ya nchi zetu)limekuwa tishio kubwa sana katika soko la ajira, kwani uwiano kati ya ajira zinazo zalishwa katika serikali na secta binafsi ni ndogo kuringanisha na wahitimu wanao ingia katika soko la ajira kila mwaka na inatazamiwa kuwa mara mbili zaidi kufikia mwaka 2050.Hili inapelekea ongezeko la ukosefu wa ajira kadri miaka inavyozidi kusonga nakusababisha utegemezi uliokithiri kwa vijana katika jamii zetu.
Mpaka muda mwingine katikati ya jamii inaonekana wale wenye elimu kuwa hawana msaada(loser) na wale wasio na elimu kuwa ndio watu wanao angaliwa na jamii kama kioo( icon) sababu mambo wanayo yafanya yanaonekana , na kizazi kinachozaliwa kuona na kuamini kwenda shule nikama kupoteza muda tuu.
DHUMUNI LA ANDIKO
Dhumuni la andiko hili nikuhamasisha jamii hasa wazazi kuwaandaa vijana wao kukabiriana najanga au wimbi hili linalozidi kuwa kubwa na tatizo katika nchi zetu.Nasema wazazi kwasababu elimu yetu tunayoipata mashuleni kwa bahati nzuri au mbaya haimuandai kijana huyu kuwa nachaguo lingine pindi asipo bahatika kupata ajira bali imejikita Zaidi kuwaandaa watu wa kuajiriwa .Natukisema kuubadili mfumo wa elimu sio jambo la kufanyika siku moja.vijana wengi wanapata tabu pindi wanapo kosa ajira kwa sababu hawana ujuzi mbadala aidha wa kibiashara au Sanaa au namna nyingine ili kujikwamua kiuchumi.Hivyo nijukumu la wewe mzazi kumuandaa mtoto kisaikolojia tokea akiwa mdogo wa namna gani anaweza kukabiliana na mazingira yake,wazazi wengi hawawaelekezi watoto wao njia wanazozifanya kupata ridhiki zao za kila siku mfano unamkuta mzazi ni fudi magari lakini hata siku moja hampeleki mtoto wake ofisini kwake au kumwelekeza.Hii nitofauti sana nawenzetu wenye asili ya asia ambao mara nyingi wamekuwa wakiwarithisha vizazi vyao yale mambo ya kiuchumi wanayo yafanya.
Pili nikuwahamisisha wahitimu kutumia fursa iliyopo ya utandawazi kuuza ule ujuzi walioupata mashuleni ili kupunguza utegemezi wa ajira,mtu mmoja aliwahi kuniambia yakuwa “ mtu aliye elimika niyule ambaye anaweza kutatua changomoto zinazo mzunguka katika mazingira yake kwa kutumia elimu aliyonayo” hivyo kama elimu uliyoipata kwa muda mrefu na haikusaidii kuna haja ya kujitafakari.Toka lilipo kuja janga la corona dunia imebadilika sana makampuni na waajiri wengi kote duniani wanawazia kupunguza garama za uendeshaji wa makampuni yao hivyo wana amua kutumia watu walio nje ya biashara zao (freelancer)kwasababu ni garama nafuu na pili wanafanya kazi kwa uhakika hivyo unaweza kuamua kuwa moja ya watu hao(freelancer) kwa kupitia majukwaa mbalimbali yaliyopo mitandaoni na ukaweza kujipatia kipato kupitia huko,tena wahitimu inatupasa kukuza vipaji vyetu binafsi aidha kwa kuongeza ujuzi au kwa kutumia kile tulichonacho kukabiliana na hali hii.
HITIMISHO
Tunaweza kuilalamikia serikali juu ya ajiri zetu,lakini jambo moja la kujua nikuwa mabadiliko yanaanza nawewe binasfi hivyo badiika sasa kwa mstakabari wa maisha yako.nakutakia mipango mizuri juu ya uchumi wako.

Upvote
0