SoC04 Tuanze na kilimo cha Pamba GMO isio kuwa na hatari kiafya, Ili kukuza zao hilo mikoa ya Kanda ya Ziwa

SoC04 Tuanze na kilimo cha Pamba GMO isio kuwa na hatari kiafya, Ili kukuza zao hilo mikoa ya Kanda ya Ziwa

Tanzania Tuitakayo competition threads

MURUSI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
4,537
Reaction score
8,824
Tanzania ni moja ya wazalisahi wa Pamba hapa Africa ikiwa sambamba na chi kama Benin, Ivory coast, Burkina Faso, Cameroon, Sudan, Mali, na Nigeria na South Africa.Tanzania inatajwa kuazlisha tani 26,000 mwaka 2023 kutoka tani 16,000 mwaka 2021/2022.

Ukilinganisha na miaka ya nyuma, kilimo cha pamba kinaenda kikififia hapa Tanzania, na hivyo kuhatarisha uchumi wa wakulima wengi hasawa Kanda ya Ziwa na Magharibi mikoa kama Simiyu, Geita, Tabora, Kigoma, Singida, Mwanza Shinyanga na Mara. Sababu ziko nyingi sana ikiwemo Bei, Ghrama za Pembejeo na Mabadiliko ya Tabia nchi.

1716471182070.png

Mmoja ya wakulima wa Pamba, kanda ya ziwa. Picha kwa mujibu wa Mitandao

GMO nini nini?

GMO ni uhandisi jeni wa mimea au ni sayansi ya kubadilisha vinasaba vya kiumbe hai kwa kutumia uhandisi jeni. GMO inaweza kuwa kwa mmea, wanyama ndege na hata bakiteria, GMO hufanyika kutambulisha sifa inayo hitajika kwenye kiumbe kama vile matunda makubwa, kustahimi ukame au kustahimili magonjwa.

Mjadala wa GMO upo sana hata hapa Tanzania, na mara nyingi unaambatana na habari mbaya tupu na za kutisha sana na za kuogofya pia.Ingawa hadi leo hakuna ushahidi wa kisayansi unao weza sema wazi kwamba GMO ni mbaya ila ni vizuri kuchukua hatua.

Kilimo Cha GMO Africa.
1716470802370.png

Picha kwa mujibu wa BBC

Hadi sasa ni nchi sita hadi saba pekee kwa Africa ambazo zinaruhusu kilimo cha GMO , na Africa ikiwa ndio kinara, hadi sasa mazao yanayo zalishwa kwa GMO Africa ni Pamba, Mahindi na Maharagwesoya.

Nchi zilizo ruhusu GMO Africa ni; Africa Kusini,Eswatini,Malawi,Sudani, Nigeria,Ethiopia na juzi juzi hapa Kenya.

Kilimo cha GMO kwenye Pamba.

Pamba ni moja ya zao ambalo linachangamkiwa sana na nchi zinazo ruhusu kilimo cha GMO, kwa nchi za Africa ukiitoa Africa ya Kusini, nchi zinazo salia zote zimeruhusu kilimo cha GMO kwenye Pamba pekee yake.
1716470632549.png

Picha kwa mujibu wa BBC

Pamba ya GMO inaitwa Pamba ya Bt na kuna kasi kubwa sana ya wakulima kuhama kutoka kutumia mbegu za awali na kuanza kulima GMO pamba. India mzalishaji mkuu wa Pamba Duniani imeruhusu kilimo cha pamba GMO pekee yake. India anazalisha tani million 5.9 kwa mwaka, ikiwa inalima pamba ya GMO kwenye hekita 21 milion, hii ikiwa ni asilimia 14 ya aridhi yote inayo lima GMI kwa sasa Duniani.

India pekee asilimia 80 ya pamba inayo zalisga ni inatokana na GMO, huku Duniani kukiwa na asilimia 75m hivyo kuifanya India kuwa juu ya asilimia za Dunia nzima kwenye kilimo cha Pamba za GMO.

Faida za kilimo cha Pamba ya GMO kw India
1716471418349.png

Mkulima wa Pamba ya GMO India, Picha kwa mujibu wa mitandao ya kijamii

India ikumbukwe ina miongo 2 sasa tangu ianze kilima pamba ya GMO na kwa tafiti mbalimbali hadi sasa imewezesha kupunguza matumizi ya madawa kwenye kilimo cha pamba kwa asilimia 37,na kuongeza uzalishaji kwa asilimia 22 na huku ikiongeza faida kwa wakulima kwa asilimia 68.

Kwa nini mataifa Mengi yamekimbilia kilimo cha Pamba cha GMO?
Ikumbukwe kwamba India ndio mzalishaji mkuu wa pamba ya GMO akifuatiwa na Marekani pamoja na China.Faida kubwa ni kwa sababu Pamba sio chakula, hailiwi kama mazao mengine mfano Mahindi na Soya, Pamba sana inalimwa kwa ajili ya kutengeneza nguo na matumizi ya hospital, Tanzania ni wanunuzi wakubwa sana wa hizo nguo ambazo zinazalishwa na pamba ya GMO.

Nchi kama India hauruhusu kilimo cha GMO kwa mazao mengine isipo kuwa pamba pekee ambayo wanajua fika kwamba sio chakula cha binadamu wala wanyama.

Pamba ya GMO inaweza sana kuhimili sana wadudu waharibifu wa Pamba,magonjwa na pia kuwa na uwezo kubwa sana wa kuhimili ukame.

Kilimo cha GMO Tanzania kinawezekana kwa sasa.
Ukweli ni kwamba Tanzania ni muagizaji kubwa sana wa nguo, asilimia 99 ya nguo tunazo vaaa tunaagiza kutoka nje hasa huk China na mitumba kutoka Marekani ambako ndio mabingwa wa kilimo cha pamba cha GMO.

Kiwango cha pamba tunacho zalisha kwa Tanzania hakitoshelezi kabisa mahitaji, na ukienda maeneo kama Shinyanga wakulima wengi sana wameacha kabisa kulima Pamba na sababu kubwa ni gharama za kuhudumia kilimo cha Pamba zisizo lingana na bei wanayo uzia Pamba, na pia pamoja na gharama kuwa kubwa bado ukame ni tatizo kubwa sana kweli kilimo cha Pamba.

Ni wakati sasa kwa Serikali kuanza kuangalia uwezekano wa kuanza kulima Pamba ambayo ni GMO ili iweze kutusaidia hata kwenye viwanda vya nguo vya ndani ya nchi ambavyo inalazimika kuagiza Pamba nje ya nchi, na vingine vingi vikiwa vimefungwa kabisa.

Pamba tunazo tumia mahospitalini ni zimeagizwa kutoka nje kweny nchi kama Pakistani na India, swala ambalo ni la aibu kubwa sana ukilinganisha na ukweli kwamba tuna aridhi ya kutosha kuzalisha Pamba.

Kilimo cha Pamba kikiruhusiwa kitakuwa na faida nyingi kwa wakulima wa kanda ya ziwa kama vile;

Vipato vya wakulima; Kanda ya ziwa na Magharibi ambako ni ukanda wa pamba kuna kiwango kikubwa sana cha umasikini kwa sasa na sababu kubwa ni ikiwa ni kushuka kwa kilimo cha pamba ambayo miaka ya nyuma ilikuwa ni zao kuu la biashara ukiachana na samaki wa Ziwa Victoria ambao nao kwa sasa wanaihilia.tunaweza punguza umasikini kwa kuruhusu kilimo cha Pamba GMO.

Vipato vitaokenana na ukweli kwamba pamba ya GMO inastahimili ukame na pia ina kinga dhidi ya magonjwa mengi yanayo shambulia pamba.

Pato la taifa; Pamba mbali na kusaidia uchumi wa wakulina ila pia inaweza saidia pato la taifa kwa kuuza pamba nje ya nchi, na kuongeza pato la taifa.

Pamba sio Chakula.; Pamba sio chakula kwamba italeta madhara ya kiafya kwa watumaiji, pamba sio kiumbe hai hivyo hakuna mdhara kwa Serikali kuanza kuruhusu kilimo cha Pamba ya GMO.

Reli ya SGR itapa mizigo ya kubeba; hadi sasa sijujua SGR itabeba nini mbali na abiria, na kumbuka Uganda pia inaunganishwa na reli ya SGR ya Kenya, hivyo kilimo cha Pamba GMO kwa kanda ya ziwa na Magharibi kitaongeza hata upatikanaji wa mizigo ya kubebwana reli ya SGR itakapo kamilika.

KARIBU KWA MASWALI
 

Attachments

  • 1716471153603.png
    1716471153603.png
    578.7 KB · Views: 12
Upvote 1
Faida kubwa ni kwa sababu Pamba sio chakula, hailiwi kama mazao mengine mfano Mahindi na Soya, Pamba sana inalimwa kwa ajili ya kutengeneza nguo na matumizi ya hospital, Tanzania ni wanunuzi wakubwa sana wa hizo nguo ambazo zinazalishwa na pamba ya GMO.
Hapa kuna mantiki nzuri tu, kwa kweli pamba kiwa GMO haikatosi haikatai kabisa. Labda tu watu wa fallacy watakuambia tukiruhusu pamba basi mazao mengine yoote pia yatafuata. Lakini tusimame imara tusiyumbishwe na mantiki mbovu pamba kuwa GMO inalipa.

KARIBU KWA MASWALI
Andiko limeshiba, ila nikipata swali ntakurudia mtaalamu.
 
Back
Top Bottom