Tubadili majina ya Daraja la Mfugale na Kijazi

Tubadili majina ya Daraja la Mfugale na Kijazi

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
13,417
Reaction score
23,310
Karibu majina ya mitaa au viwanja vya ndege huwa yanatolewa na watu waliopo kuwaenzi watu fulani kwa michango yao. Mfano uwanja wa Benjamin Mkapa ulipata jina baada yya Rais wa awamu ya pili kufariki mwaka jana. Ila ndiye aliyeazimia kuujenga.

Aidha hata uwanja wa JK Nyerere International Airport ulipata jina hilo miaka kadhaa baada ya Nyerere kufariki mwaka 1999. Yeye ni Baba wa Taifa ingawa wakati wa uhai wake alikataa sana kutukuzwa kwa namna hiyo.

Namna ambavyo Eng Mfugale na Eng Kijazi wamepewa kumbukumbu ya majina yao kwenye daraja la Tazara na la Ubungo kwa kweli hairidhishi. Mimi natambua wao walikuwa wafanyakazi wa Serikali waliokuwa na majukumu ya ku-design na kumsimamia ujenzi. At end of the day walikuwa wanalipwa mshahara kwa kazi yao.

Ila yule Rais Marehemu alikuwa anajiamulia tu kutoa majina kwa washirika wake.

Mbona kuna Mashujaa wengi tu ambao wangepewa heshima hiyo. Nashauri kwa sasa tuyaite Tazara Overhead bridge na Ubungo interchange tu.
 
Tuheshimu mamlaka yaliyokuwepo na kutoa majina hayo kwa lengo la kutambua mchango wa watu hao katika ujenzi wa nchi.

Bado tunaendelea kujenga miundombinu mbalimbali kuna siku tutaishiwa majina na tutaita baadhi ya barabara Sarpong High Way (Relax)
 
Tuheshimu mamlaka yaliyokuwepo na kutoa majina hayo kwa lengo la kutambua mchango wa watu hao katika ujenzi wa nchi.

Bado tunaendelea kujenga miundombinu mbalimbali kuna siku tutaishiwa majina na tutaita baadhi ya barabara Sarpong High Way (Relax)
Kwani hiyo miundombinu tutajenga angani si kuna majina yake ya asili?
 
Naunga mkono hoja, kuna majina mengi tu ya Watanzania wanaopigania HAKI za Binadamu Tundu Lissu, Sheikh Ponda,Askofu Mwamakula,Mashekhe wa Uamsho ni Watanzania waliojitolea sana na Huu ni wakati muafaka kuwaenzi.

Maria Sarungi Tsehai
 
Hawa Mfugale na Kijazi (RIP), Chamuriho na Deus Kakoko yasemekana walikuwa ndiyo wasiri wa Jiwe kwenye deals za mikataba mikubwa. Wengi ameanza nao akiwa Wizara ya Ujenzi na TANROADS.

Hata mimi sioni mantiki ya kuyaita madaraja kwa majina ya watu ambao walikuwa waajiriwa wa Serikali. Hii ni kuuenzi UFISADI wa Jiwe na genge lake. IBADILISHWE TU
 
Dhambi ya ubaguzi mwisho wake ndiyo mwanzo wake.
 
Mambo ya kiswahili hatuna mada ya maana!? Tuthamini vyetu hao Watanzania wenzetu ni jambo jema.
 
Back
Top Bottom