SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Kumekuwa na huu utaratibu wa muda mrefu wa timu za Simba na Yanga kuhakikisha nahodha na wakati mwingine nahodha msaidizi ni Watanzania. Sijajuaga dhana hii ilijengwa kwa sababu gani ila naona ilishapitwa na wakati.
Kuna vigezo inabidi tuvizingatie katika kuchagua nahodha wa timu, kikubwa kuliko vyote thamani yake katika timu (awe MVP wa timu). Hapa simaanishi mshahara bali mchango au utegemezi wa timu kwa mchezaji huyo. Hapa tunazungumzia wachezaji kama Diarra, Mayele, Inonga na Chama.
Pa ufahamu mzuri wa lugha mojawapo ya kimataifa inasaidia hasa katika mashindano ya kimataifa. Pale mchezaji anapokuwa na changamoto katika lugha ya kigeni kunampunguzia kujiamini na matokeo anashindwa kuitetea timu dhidi ya waamuzi au wachezaji wa timu pinzani.