Tubadilishane mawazo juu ya QNET Business

Tubadilishane mawazo juu ya QNET Business

Huwezi nunua eti saa milioni tatu halafu eti uwatafute wakuwauzia hiyo saa au kuwaunga kwenye mnyororo wako. Utahangaika sana mimi nawafahamu watu kadhaa waliojiunga wakaishia kulia baada ya kununua bidhaa ambazo hawawezi kuuza.

Kuna mdada alikuwa anafanya kazi bureau de change, sijui alidanganywa na nani akaacha kazi baada ya kuaminishwa kwamba atakuwa tajiri ndani ya muda mfupi. Akajiunga huko Q-net na kuchukua mkopo ndo akawekeza huko.

Kilichompata mpaka leo hana hamu hadi alihama jiji maana ni makubwa yaliyomkuta.
Hizi biashara za pyramid scheme ni hatari sana sana,,,, Kuna hawa wengine wanajiita phyto science nao waliowahi wamekula sasa wanaokuja huku chini wanaliwa hatari ...
 
Nafaka,
Mie jirani yangu kaacha kaz decent dec kaingia na mkewe huko wametoa 10m..shoga anashinda kwangu akinishawishi...amefikia hatua anasema nitoe 2m then 2 tuingie kitaa tukope niingie😅😅! Mara aninunie mara arudi😂😂😂
 
Haaaa kaa mblai watapata tabu sana hasa kpndi hiki cha corona
 
Wakishakutapeli ndio utajua dunia ikoje

Humu jf Kuna nyuzi mbalimbali zinazungumzia hiyo Qnet kwa mapana na marefu ,na Kuna shuhuda za kutosha kabisa jinsi watu walivyotapeliwa

Wewe unakuja kusema Ni biashara Inayoweza kukutoa kimaisha?

Pole sana
 
Mkuu achana na qnet
Njoo tufanye biashara ambazo ni realistic.. Hasa kipind hiki cha mavuno...faida uhakika 10% ya mtaji wako kwa mwezi, uhakika badala ya kutupa pesa huko 5m kununua mikufu na filter za maji.

Ndani ya miezi sita ijayo utakuja kuleta mrejesho hapa wa biashara yetu( Mimi na wewe). Risk more in calculated risk below age 35 yrs ukishafika 40+ yrs utaanza kujuta taratibu kwanini hujachukua hatua za hatari kujaribu biashara fulani...au uwekezaji wowote,baada ya 50+ majuto yanazidi ..ni kujifyonza na kulaumu tu, at the 60+ ni huzuni,na lawama kwa watoto...na kusingizia kurogwa,..n.k

Njoo PM mwenye mtaji 1 million hadi 200million uhakika 10% faida kila mwezi. Uoga wako ndo umasikini wako.na akili nyingi huondoa maarifa na busara za kufanya jambo.

Havache!
 
Hivi mtu unashawisjikaje? Mimi walishaniita kwwnye zile ofisi zao ziko pale Mwenge niliwakatalia palepale. Nikawambia sina hela za kuchezea maana sioni mikinufaika kutoka katika mzunguko huo. Hawajawahi kunipigia simu tena na nilimwambia jamaa alonipeleka pale kwamba siku nyingine akinipigia simu awe na mada zingine sio hiyo. Alikoma
 
Napenda tubadirishane mawazo juu ya biashara hii ya QNET inayoineka inaweza kuwa msaada wa kujiingizia kipato mbadala na kujikwamua kiuchumi.
Rafiki yangu 1 tumeshafanya kazi nyingi sana, halafu tunaheshimiana sana, alinipigia akaniambia ana shida ya kuonana na mimi anipeleke mahali muhimu sana, sikumkatalia nikaenda. Nilipofika na kukutana na mambo ya Goodmorning ile saa 1 usiku, na habari nyingine ambazo sijawahi kuzisikia. baada ya kufika nyumbani, nikafikiria yule mshikaji wangu alinifikiriaje? Mpaka leo huwa nashindwa kupata jibu lake. na hata yeye sikumuuliza tena aliendeleaje. Mana alinunua saa takribani Tshs Milioni 4.
Duniani, hasa kwenye utafutaji wa pesa, kuna mambo mengi sana yanayoendelea.
 
Hao Qnet na ndugu zake ni utapeli tu nina demu wangu katumia karibu mwaka mzima kunilazimisha niende kwenye semina pale Makumbusho-Dar majibu niliompa mungu tu anajua maana karibu uhusiano uvunjike, tena mbaya zaidi wanakuwa wabishi hata ukiwaambia unakwenda kupigwa tu huko hutafanikiwa chochote, namwangalia sasa nasema tu hihiii maana nisipompa vocha hawezi kuwa hewani hata mwezi wakati wanajifanya ni milionea.Kuwa makini kijana wajinga ndo waliwao.
 
Jibu kalipata
 
Habari wadau wa JF,

Mada tajwa yajieleza, kutokana na kuwa na Mlipuko wa ugonjwa wa Corona na kupelekea kwa baadhi ya watu kutpoteza vyanzo vyao vya fedha na kama wanapata fedha sio kama hapo awali.

Napenda tubadirishane mawazo juu ya biashara hii ya QNET inayoineka inaweza kuwa msaada wa kujiingizia kipato mbadala na kujikwamua kiuchumi.
images
Goodmorning!!!
 
Mkuu achana na qnet
Njoo tufanye biashara ambazo ni realistic.. Hasa kipind hiki cha mavuno...faida uhakika 10% ya mtaji wako kwa mwezi, uhakika badala ya kutupa pesa huko 5m kununua mikufu na filter za maji.

Ndani ya miezi sita ijayo utakuja kuleta mrejesho hapa wa biashara yetu( Mimi na wewe). Risk more in calculated risk below age 35 yrs ukishafika 40+ yrs utaanza kujuta taratibu kwanini hujachukua hatua za hatari kujaribu biashara fulani...au uwekezaji wowote,baada ya 50+ majuto yanazidi ..ni kujifyonza na kulaumu tu, at the 60+ ni huzuni,na lawama kwa watoto...na kusingizia kurogwa,..n.k

Njoo PM mwenye mtaji 1 million hadi 200million uhakika 10% faida kila mwezi. Uoga wako ndo umasikini wako.na akili nyingi huondoa maarifa na busara za kufanya jambo.

Havache!
GAKA jingine hili hapa.a.k.a mkenge
 
Nadhani umesoma comments zote, uamuzi ni wako. Ila kumbuka hao walio-comment sio wajinga.
 
Back
Top Bottom