sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Haijalishi ni Ukristo au uislamu, hizi dini sio kwajili ya wazungu na waarabu kama watu wengi wanavyodhani, hizi dini ni kwajili ya mtu yoyote sehemu yoyote duniani.
kumekuwa na mazoea mabovu tangu zamani ya wanaoabudu hizi dini kwa kudhani kwamba ili kuabudu dini ya kiisalamu inabidi uige ige vya waarabu na ili kuabudu ukristo inabidi ufanye vile wanavyofanya wakristo wazungu.
MAJINA - Mnyakyusa wa Mbeya unamkuta anaitwa Steven, kaacha majina yake ya kinyakyusa kama Atupele, Atuganile, n.k.
Mnyamwezi kapata binti anampa jina la Ashura, kaacha jina zuri la asili kama Minza, tena mbaya zaidi hata jina la ukoo limebadilishwa kuwa la kiarabu Mohammed, hapo mtoto ataitwa Ashura Mohammed.
NDOA - Mkristo atavaa suti kama wazungu, mke atavaa shela, viapo ni vile vile ila vimetafsiriwa, honey moon, n.k. yani ni copy paste. hakuna chembe yoyote ya kutamaduni kwa asili labda kuweka mziki wa kikabila kwajili ya burudani ukumbini.
Muislamu wa bongo kwenye kuoa nako ni hivyo hivyo, ili ndoa ifane atakifuga jambia kiunoni kama muarabu, atavaa kama muarabu, n.k.
MISIBA - hapa napo ni yale yale tu.