Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
UKIPEWA SH.10000 UMFUKUZE KANGA KATAA, HUTAMPATA
Tanzania inatajwa kama taifa linaloongoza kwa kuwa na mbuga pamoja na wanyama wengi duniani.
Itapendeza iwapo tutakuwa tukizielewa tabia za wanyama tuliona pamoja na vituko vyao ambavyo huwa ni burudani kwa binadamu na watalii kutoka nje.Na vile vile kusoma tabia zao kunaongeza akili na kufikiri kwa binadamu.
Mimi leo nitaanza na ndege aina ya kanga ambaye anaishi misituni na majumbani.Ukitaka kumchinja awe kitoweo chako inabidi uwahi mapema kabla hawajatoka kwani akiwa nje si rahisi kumkamata kwa kumfukuza kama kama kuku.
Ukipewa shilingi elfu kumi umshike basi samehe,utaumia bure na hutompata. Ile kufukuzwa na kukimbia yeye ndio furaha na mchezo wake.Kama umemfukuza na hutomkamata basi huenda huko aendako na baadae kukurudia pale ulipo kama kwamba anakwambia tuanze tena..
Hebu kama na wewe una mkasa wa mnyama, ndege au mdudu mwengine lete hapa tuvutie utalii wa ndani na nje. Ukiunganisha na video uliyopiga mwenyewe itakuwa msaada zaidi. Ukikosa ya kwako hata ya watalii itatosha.